saidi bunduki
Member
- Mar 10, 2018
- 24
- 23
Kutoka mtandao wa
www.mrbunduki.com
Kama kuna orodha ya vitu vinavyochukiwa zaidi na Watanzania basi ni kusoma vitabu. Sijui ni kwasababu gani hasa.
Ingawa watu wengi hawapendi kusoma lakini ifahamike kuwa kusoma ni jambo ambalo huimarisha sana ubongo katika kufikiri, kuzingatia na kuelewa. Unajisikiaje unaposoma kitu hasa kinachokuvutia kama mfano wa makala hii nzuri?😜😜😜
Unaposoma mara nyingi akili yako inakuwa katika kile ambacho unakisoma. Basi hivi huufanya ubongo wako kuwa makini zaidi kuliko yule ambaye haushughulishi. Kwakuwa wanafunzi wanahitajika kuhimizwa zaidi katika kusoma ili kukuza bongo zao, nawe mtu mzima mwenzangu ni vema ukaanza kidogo kidogo kuuzoesha ubongo wako.
Utajiri wa lugha na misamiati
Haijalishi unachokisoma kipo katika lugha gani. Kama ni lugha ya Kiswahili basi utapata maneno mapya ambayo huenda hukuwa unayajua na kama ni lugha yoyote ya kigeni ndio utapata maneno mengi zaidi. Na muda wa kuwa unachokisoma ni chenye kuvutia hivyo ni rahisi zaidi kutafuta kamusi na kujua mengi zaidi.
Kupunguza msongo wa mawazo
Kama tulivyosema hapo awali, unaposoma huwa akili yako inaelekea katika kile unacho kisoma zaidi hivyo hupunguza mawazo na kujisikia huru katika akili yako. Na baadaye unaweza kupata suluhisho la kile ambacho kilikuwa kinakusumbua.
Kuimarisha uwezo wa uandishi
Si lazima uwe muandishi wa vitabu ndio msomi wa vitabu, imarisha uwezo wako wa kuandika, kuzungumza, kufikirti kwa kusoma vitabu kwani pia ni sehemu ya kuongeza busara.
Kusaidia kulala
Kusoma hakukusaidii kulala ila kunasaidia kulala kuliko bora zaidi na kuufanya usingi wako kuwa wa amani. Pia kama unaona katika muda huo unataka kulala lakini huna usingizi basi chukua kitabu chenye hadithi nzuuuri na usome utaona matokeo yake. Hivyo kusoma husaidia pia kuvuta usingizi mnono na ndoto nzuuri kabisa.
Kuitia muangaza siku yako
Hivi umeshawahi kuwaza kuwa vitabu vinaweza kuleta furaha katika siku yako nzima? Hii hutokea pale ambapo umesoma stori nzuuri ambayo aidha imekuvutia ama imekufundisha kitu na hususan kikawa na manufaa kwako.
Kuongeza ubunifu
Kuna tofauti katika kusoma na kuangalia movie. Katika kusoma huwa unatumia akili niyngi zaidi kuliko pale ambapo unatazama. Ukitazama ni rahisi zaidi fikra zako kuhama na kufikiri jambo jingine tofauti na pale unapo soma akili yote hufikiri kile unachokisoma na kukielewa vizuri na bila shaka unaweza kupata mbinu mpya katika mambo yako. Hii ndio maana tukasema tunaongeza ubunifu.
TUSOME NINI?
Kila mtu ana vitu ambavyo vinamvutia kuvijua, lakini Kuna vitu ambavyo ni muhimu kwa wote. Kwa mfano vitabu vya dini na mafundisho yake n.k. Hapa viongozi wa dini wamefaulu kwa kiasi kikubwa Sana.
Lakini pia vipo vitabu muhimu vya mafunzo mbali mbali vyenye manufaa kwako Kama vitabu vya afya, hadithi za kale, sayansi n.k.
HIVYO BASI
www.mrbunduki.com
Kama kuna orodha ya vitu vinavyochukiwa zaidi na Watanzania basi ni kusoma vitabu. Sijui ni kwasababu gani hasa.
- Kuenea kwa teknolojia?
- Kazi nyingi?
- Uvivu?
- Hakuna watunzi wazuri?
- Hatujui umuhimu wake?
- Okeeey tuyaache hayo, najua si wote ambao ni wavivu katika hili. Lakini kama nawe ni miongoni mwa hao, leo nakuletea faida 7 tu za kusoma vitabu.
- huenda baada ya hapo utapata kitu ambacho kinaweza kukusaidia katika maisha yako ya kila siku.
***************************************
Kusisimua akili na kuupa ubongo mazoeziIngawa watu wengi hawapendi kusoma lakini ifahamike kuwa kusoma ni jambo ambalo huimarisha sana ubongo katika kufikiri, kuzingatia na kuelewa. Unajisikiaje unaposoma kitu hasa kinachokuvutia kama mfano wa makala hii nzuri?😜😜😜
Unaposoma mara nyingi akili yako inakuwa katika kile ambacho unakisoma. Basi hivi huufanya ubongo wako kuwa makini zaidi kuliko yule ambaye haushughulishi. Kwakuwa wanafunzi wanahitajika kuhimizwa zaidi katika kusoma ili kukuza bongo zao, nawe mtu mzima mwenzangu ni vema ukaanza kidogo kidogo kuuzoesha ubongo wako.
Utajiri wa lugha na misamiati
Haijalishi unachokisoma kipo katika lugha gani. Kama ni lugha ya Kiswahili basi utapata maneno mapya ambayo huenda hukuwa unayajua na kama ni lugha yoyote ya kigeni ndio utapata maneno mengi zaidi. Na muda wa kuwa unachokisoma ni chenye kuvutia hivyo ni rahisi zaidi kutafuta kamusi na kujua mengi zaidi.
Kupunguza msongo wa mawazo
Kama tulivyosema hapo awali, unaposoma huwa akili yako inaelekea katika kile unacho kisoma zaidi hivyo hupunguza mawazo na kujisikia huru katika akili yako. Na baadaye unaweza kupata suluhisho la kile ambacho kilikuwa kinakusumbua.
Kuimarisha uwezo wa uandishi
Si lazima uwe muandishi wa vitabu ndio msomi wa vitabu, imarisha uwezo wako wa kuandika, kuzungumza, kufikirti kwa kusoma vitabu kwani pia ni sehemu ya kuongeza busara.
Kusaidia kulala
Kusoma hakukusaidii kulala ila kunasaidia kulala kuliko bora zaidi na kuufanya usingi wako kuwa wa amani. Pia kama unaona katika muda huo unataka kulala lakini huna usingizi basi chukua kitabu chenye hadithi nzuuuri na usome utaona matokeo yake. Hivyo kusoma husaidia pia kuvuta usingizi mnono na ndoto nzuuri kabisa.
Kuitia muangaza siku yako
Hivi umeshawahi kuwaza kuwa vitabu vinaweza kuleta furaha katika siku yako nzima? Hii hutokea pale ambapo umesoma stori nzuuri ambayo aidha imekuvutia ama imekufundisha kitu na hususan kikawa na manufaa kwako.
Kuongeza ubunifu
Kuna tofauti katika kusoma na kuangalia movie. Katika kusoma huwa unatumia akili niyngi zaidi kuliko pale ambapo unatazama. Ukitazama ni rahisi zaidi fikra zako kuhama na kufikiri jambo jingine tofauti na pale unapo soma akili yote hufikiri kile unachokisoma na kukielewa vizuri na bila shaka unaweza kupata mbinu mpya katika mambo yako. Hii ndio maana tukasema tunaongeza ubunifu.
TUSOME NINI?
Kila mtu ana vitu ambavyo vinamvutia kuvijua, lakini Kuna vitu ambavyo ni muhimu kwa wote. Kwa mfano vitabu vya dini na mafundisho yake n.k. Hapa viongozi wa dini wamefaulu kwa kiasi kikubwa Sana.
Lakini pia vipo vitabu muhimu vya mafunzo mbali mbali vyenye manufaa kwako Kama vitabu vya afya, hadithi za kale, sayansi n.k.
HIVYO BASI
- Baada ya makala hii fupi nimekauandalia baadhi ya vitabu ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinaweza kukupa faida katika maisha yako. jaribu kupitia hivi.
- Kitabu cha afya
- Kitabu cha matunda
- Afya ya uzazi