Faida ya kuzungukwa na watu wenye akili

Mimi nahitaji kuonana na Mzee wangu Rostam Aziz,yaaani kwa mawazo na ideas nilizo nazo hapo ndio mwanzo wa mimi kuwa Bilionea.Na naoana ni mtu mwema
 
Hawa wenye akili ya kuruhusu expatriates as many as per desire ya investors tuwaweke fungu lipi, hawa wakuruhusu wachuuzi wa Kenya waje kumiliki ardhi ya Tz wana akili za bata au mbayuwayu?

Ukikaa kipumpavu pumbavu kwenye nchi yako acha Wakenya waje wachukue nchi, sasa umekaa kijiweni unacheza bao halafu analalamika Wakenya kuja kuchukua nchi!
 
... kazi ya kwanza na ya msingi ya kiongozi ni kutengeneza team; more precisely, a winning team. Ni aina gani ya watu kiongozi atawaingiza kwenye timu yake ndicho kitakachoamua hatma ya unacho oongoza - success or failure!

Kama timu itakuwa na waimba mapambapio; wanaoogopa kukuambia ukweli hata pale unapokosea pengine kutokana na tabia yako that shall lead to failure. Daima kwenye timu weka wenye mawazo chanya na uwezo hata kama watakuzidi; ni hatari sana kiongozi kuogopa au kutotaka kukosolewa! Kuwa makini sana na "wanaokutukuza"; those a devils!
AMEN, AMEN
 
Na Thadei Ole Mushi.

Elon Musk ni Mtu maarufu Sana Duniani na Tajiri mkubwa Sana. Anamiliki kampuni la SpaceX ambalo huunda vifaa vya kuhama Orbit Moja kwenda nyingine au kwa Lugha rahisi huunda engine za Rocket zinazoweza kwenda anga za juu na kutua katika Sayari nyingine (aerospace). Kampuni Hili linamiliki technolojia ya hali ya Juu Sana.

Kwenye Ukurasa wake wa tweeter kaandika hivi:-

I don't have an aerospace degree. I've read a lot of books and talk to a lot of smart people and have a great team.

Kwa tafsiri ameandika kuwa hana degree ya kutengeneza hizo aerospace Bali kinachomsaidia ni Kuwa anasoma vitabu vingi na kuongea na watu Smart na kuwa na Timu nzuri.

NUTSHELL

February 2019 Rais Uhuru Kenyata alitoa kauli nzito sana, Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema:-

"Hatuwezi kuacha akili za Rais zizagae Mtaani, acha tuzitumie kwa maslahi ya Taifa"

Maana yake ni kuwa watu wote wenye akili kubwa, Fikra pevu na ambao ni Msaada kwa Taifa ni Mali ya Serikali na ni Mali ya Rais aliyepo madarakani.

Anapaswa kuzitumia ili zinufaishe taifa na Sio wazurure huko mtaani.

Kauli ya Uhuru inakwenda kushahibiana na kauli ya Aliyowahi kuitoa Kiongozi wa chama EFF (Economic Freedom fighter) Juliasi Malema aliyewahi kuulizwa swali kama ana Ndoto za kuja kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Jibu lake alilojibu alisema "Any Fool can be a president" Mjinga yeyote anaweza akawa Rais.Malema Aliendelea kwa kusema alimradi Rais azungukwe na watu wenye Akili kubwa.

Mama SAMIA Juzi karudi pale pale kuwa atateua yeyote awe mpinzani au CCM as Long as anaona anaweza kulisaidia Taifa lake.

Kuna faida Sana sio kwa viongozi tu hata katika maisha ya kawaida ku screen watu wanaokuzunguka.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Nionyeshe marafiki zako nijue tabia zako" ikiwa na maana kwamba wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana kukufanya ulivyo. Kama ukikaa na wenye tabia ya kukata tamaa na wewe utakuwa unakata tamaa kwenye mambo yako, ukikaa na wanaofikiria chini ya kiwango na wewe utakuwa unafikiria chini ya kiwango.

Niliwahi kuandika hapa kuwa angalia uhusiano uliokuwepo kati ya Socrates na Plato. Plato alikuja kuwa alivyo kutokana na ukaribu wake na Socrates kwa hiyo Plato ni zao la Socrates na Aristotle ni Zao la plato. Amini wanaokuzunguka wanakufanya ulivyo. Kama Plato angelizungukwa na Mvua Samaki na yeye angelikuwa mvua Samaki. Angezungukwa na wacheza kamari na yeye angelikuwa mcheza kamari.

Nani anamjua rafiki yake mkubwa Karl Max alikuwa nan? Kamsome mtu anayeitwa Fredrick Angels, Japokuwa walikuwa wanaishi mbalimbali ila mawazo yao ya kijamaa hayajawahi kutofautiana kwa kuwa hawa walikuwa marafiki wakubwa.

Marafiki wana nafasi kubwa Sana kwenye maisha yako, chagua vizuri watu wa kukuzunguka, amua Sasa Punguza wivu, na Kiburi kwa waliokuzidi, watumie Kama ngazi ya kufika unakotaka kwenda.

Leo hii tunashuhudia Biden kazi yake ya kuwa Rais wa Taifa la Marekeni ikiwa rahisi Sana kutokana na Rafiki aliyemzunguka. Katika Moja ya Bond Bora kabisa ya marafiki kwa Karne hii Basi huwezi kuitoa Bond ya Obama na Biden kwenye tatu Bora. Urafiki wao umekuwa gumzo kubwa wakiwa bado wanahudumu kwa pamoja White House na baada ya kustaafu na hata sasa wakati Biden akirudi Ofisini.

Hebu jioni hii fanya assessment ya wanaokuzunguka, je Wana kupush kwenda mbele au wanakutengeneza kuwa Nani,au wewe unawatengeneza kuwa Nani?.

Ole Mushi
0712702602

ndio maana Chadema imefariki maana Mbowe yeye mwenyewee kilaza amezungukwa na vilaza na mashabiki zake vilaza
 
Alizungukwa na wapumbavu,wakamjaza huo,kisha wakachungulia dirishani na kumwambia " hakika nchi yote imefurahi kwa jambo hili kubwa ulilolifanya sasa" (upumbavu) naye akiisha kusikia hivyo akawaita hao wapumbavu na kuwaambia "roho yangu imefurahi,basi na tufanye tena jambo lile(upumbavu) nao watu watanishangilia na kunisifu hata mbingu zisikie"
expand...
ndio maana Chadema imefariki maana Mbowe yeye mwenyewee kilaza amezungukwa na vilaza na mashabiki zake vilaza
 
Back
Top Bottom