Faida utakayopata uki-date na wanawake wapiga mizinga

Faida utakayopata uki-date na wanawake wapiga mizinga

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
10,141
Reaction score
18,803
Mu hali gani Wana JF? Natumai mnaendelea vyema na pilka pilka za kuijenga nchi yenu ya Tanzania.Huku Kenya vyuma vimekaza Sana nawaza kuhamia huko Tz kwahyo naomba mniambie sehemu nzuri ya kufikia.

Moja kwa Moja acha niende kwenye mada husika.Lengo la kuleta huu Uzi Ni kutaka kuwaelimisha kidogo vijana wenzangu ambao ndo kwanza wameanza kudate mademu. Najua ukianzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu unaweza ukakumbana na Mambo ambayo yanaweza kuwa nje ya uwezo wako. Suala la pesa limekuwa Kama ndo uti wa mahusiano. Yaani ckuiz bila pesa Ni vigumu Sana kuenjoy penzi la mwanamke husika.

Siku hizi asilimia kubwa ya vijana wa kiume wameshindwa kuwatongoza wanawake kwa sababu wanajiona hawapo Vizuri kiuchumi kwahyo wanaogopa kupigwa mizinga na wanawake.Lakini Hawa wanawake wenye kupiga mizinga (kuomba omba pesa) Wana faida kubwa Sana kwa vijana wa kiume. Zifuatazo Ni baadhi ya faida zitokanazo na kudate na wanawake wapiga mizinga.

1. Wanakusaidia kugain experience ya kuihudumia familia yako siku ukioa. For instance tuseme umeoa mke afu hyo ndo mwanamke wa kwanza kbsa kwako wewe. This means hujawahi hudumia mwanamke yoyote aidha kwa kumpa hela ya matumizi,kumtoa out, kumpeleka saloon na kadhalika.

Sasa huyo mwanamke uliyeoa ndo wa kwanza na unatakiwa umhudumie Kama mmewe.Sasa wewe jamaa huna experience ya kutake responsibilities Kama mwanaume so mkeo akianza kumuomba hela ya saloon,ya kununulia mavazi na Mambo mengine utaona Kama anakuzingua coz ni vitu ambavyo hujavizoea ba hujawahi kumbana navyo maishani mwako.Hapa Sasa utataka mwenyewe ajihudumie.

2. Inakusaidia kuwa mpambanaji kiutaftaji. Kudate na wanawake wapiga mizinga kunamsaidia mtu atafute pesa kwa bidii maana anajua anytime anaweza akapigwa mzinga.Kwa hiyo jamaa anakuwa buze kutafuta michongo itakayomuingizia kipato na Wala habagui kazi kikubwa apate pesa za kumhudumia demu wake.

Vijana ambao hawapo kwenye r/ ships na wanawake Mara nyingi wanakuwaga idol Sana maana wanajua Hakuna mtu atakayewaomba hela.Hawa kazi yao Ni kuamka asubuhi kunywa chai ya mama yao na kwenda vijiweni kupiga story za Arsenal kushibishwa kuqualify kwenye UEFA champs.League.Hata wakiitiwa kazi hawataki kbsa.

3. Inamsaidia mtu kuimarika kiuchumi; Hii sababu in uhusiano wa Moja kwa moja na sababu ya 2.Kudate na Mwana anayeomba Sana pesa humwezesha mtu kuimarika kiuchumi coz probability ya kupigwa mzinga Ni 50% na probability ya kutokupigwa mzinga Ni 50% pia. Which means jamaa akitafuta pesa afu kwa Bahati nzuri asiombwe hyo pesa na mwanamke wake Basi Ana option ya kuiwekeza hyo pesa kwa project ambayo itamletea faida.

4. Inamjengea mtu heshima mtaani. Aisee Hakuna watu walioheshimika Kama wanaume wanaojua kuhudumia familia zao.Wanawake zao ndo huchukua jukumu la kuwaheshimisha kwa watu. Kwa hiyo kijana ukijua kumhudumia demu wako Basi bila Shaka atakuheshimu Sana na pia atakuheshimisha kwa ndugu,jamaa na marafiki zake kwa ujumla.

My Take Vijana wa kiume nawashauri msiogope kutongoza wanawake kwa kuhofia kupigwa mzinga maana watawasaidia Sana kwa Mambo niliyoelezea hapo juu.

I stand to be corrected where I seems to have gone astray.
 
Huu uzi kuna kufirisika ndani yake, tusiuchukulie siriazi.
 
Back
Top Bottom