Faida na hasara za michepuko

Faida na hasara za michepuko

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,565
Habari zenu wanajanvi.

Hakina kwenye kibaya pia kuna uzuri wake.
Nachelea kusema hivyo Baada ya kufanya uchunguzi mdogo usio rasimi katika suala la mahusiano hususani idara ya Michepuko.

Kuchepuka ni kitendo cha kupita sehemu isiyo rasimi kuelekea unakokwenda ili kuepuka msongamano au kupata njia fupi (shortcut) kufika mapema.

Kuchepuka katika suara la Mahusiano ni kitendo cha kutembea nje ya Ndoa au Mahusiano Rasimi.

Sasa katika hili kuna mambo mengi yanaibuka lakini leo nitaongelea Faida na Hasara za Kuchepuka/Michepuko.

HASARA

1. Kuambukizwa Magonjwa ya zinaa kama kinga haitatumika.
2. Kusahau/Kutelekeza Familia kama Mchepuko utakua na skills za kutosha.
3. Kuishi kwa hofu na mpenzi wako kwani nafsi inaksuta na hofu ya siri yako ya Mchepuko kuvuja.
4. Gharama zitapanda kugaramikia Familia na kuumaintain Mchepuko.
5. Kua na ratiba tight kwani unahitajika kwa Familia na kwa Mchepuko kwa wakati moja na hii ataleta stress/Msongo wa Mawazo.
6. Kutokua huru na Mpenzi wako kwani kuna kitu anaficha, na utakua hauko huru na Simu yako.
7. Kua mkali/kuboreka na Familia kwani atahisi wanakubana usijiachie na Mchepuko.
8. Kutokua huru kutoka OUT na Familia hususani kama Mchepuko utakua jirani au Location.
9. Kukwepa ibaada kwani Dhamila inakuhukumu.
10. Kutofurahi unyumba na Mpenzi wako hasa akiwa anazidiwa ufundi na Mchepuko na ndio hivyo Mara nyingi.

FAIDA
1. Inapunuza stress hasa kama Mpenzi wako hakujari.
2. Inadumisha mahususiano kwani inapunguza Wivu wa kijinga hasa kama wote Mnachepuka.
3. Inaleta uvumilivu kwenye Mapenzi huwezi kumuhukumu mpenzi wako harakaharaka kwani na wewe hauko Sawa
4. Kupata vionjo mbalimbali kwani Michepuko huwa inajituma sana.
5. Inaongeza Mori wa kazi hasa kama Mchepuko wako upo Hapo kazini.

Kifupi Hasara ni Nyingi japo wakati mwingine Michepuko inasaidia mutants Maisha yaende.
 
Hizo unazoita faida za mchepuko, zinapatikana pia kwenye njia kuu kwa ubora zaidi kwa mfano kwa kupitia members wengine wa familia yako aka watoto.
 
Kwa michepuko vumbi sawa lazima hasara ziwe nyingi, ila kwa michepuko rami akuuuuu.
 
Habari zenu wana JF
Naomba tujadili kwa kina kuhusu faida na hasara za mwanaume au mwanamke aliye kwenye ndoa kuchepuka
 
Habari zenu wana JF
Naomba tujadili kwa kina kuhusu faida na hasara za mwanaume au mwanamke aliye kwenye ndoa kuchepuka
 
Habari zenu wana JF
Naomba tujadili kwa kina kuhusu faida na hasara za mwanaume au mwanamke aliye kwenye ndoa kuchepuka
 
Back
Top Bottom