Wanajamii, hebu tupeane elimu kidogo, kwanini tunasema "profit and loss na siyo profit or loss" au "kufa na kupona badala ya kufa au kupona" kwasababu kinachotokea ni kimojawapo na si vyote viwili kwa pamoja! Mwenye kujua zaidi tafadhali.
Ukitaja mfano "profit and loss account " haimaanishi Kuwa vinatokea vyote viwili Kwa wakati mmoja . Mleta mada usitafsiri kingereza kwenda Kiswahili Moja Kwa Moja hautapata maana halisi . Profit and loss account Ina maana kwamba ni report ambayo inaweza kuonesha profit au ikaonesha loss na si Kwa wakati mmoja Kwa maana unapoanza kuisoma kuanzia juu unakuwa hujui Kama Mwisho kuna loss au profit