JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Utafiti unaonyesha kuwa mbegu ya parachichi inakiwango cha asilimia 65 cha amino acids na pia ina kiwango kikubwa cha fiber ukilinganisha na vyakula vingine.
FAIDA ZA MBEGU YA PARACHICHI
1- Inapambana na tatizo la arthritis, sababu mbegu ya parachichi ni anti-inflammatory ( inatabia ya kupambana na vichochezi)
2- Mbegu ya parachichi inaondoa gesi tumboni na kuvimbewa, husaidia kukata kuharisha. Mbegu hii hutumika kutengeneza madawa yanayopambana na infections kwenye mwili wa binadamu na matatizo ya matumbo.
3- Utafiti pia unaonyesha inapotumiwa huongeza viwango vya collagen, hivyo hupambana na kuzeeka kwa kuifanya ngozi yako kuwa imara na isiyo na mikunjo.
4- Inaimarisha kinga ya mwili, hivyo husaidia kuzuia magonjwa yasikupate.
5- Ni effective sana katika kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini ( fat burning), na inachangia kupunguza uzito kwa haraka zaidi.
6- Ina kiwango cha juu cha nguvu ( energy) hivyo mtumiaji atakuwa kamili na ng'a ng'ari siku nzima.
7- Mbegu ya parachichi inazuia vivimbe ( tumors) sababu inakiwango cha Flayonol.
Pia mbegu ya parachichi inatoa sumu mwilini na ina tibu vidonda vya tumbo ANGALIZO: Ikiwa wewe ni allergic na mbegu za matunda ama parachichi, tafadhali wasiliana na daktari wako Kabla ya kutumia.