Fahari ndio mama wa ujinga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,117
Takwimu zinaonyesha kuwa jengo letu la bunge linakamata nafasi ya pili au ya tatu Afrika kwa uzuri na ukubwa kwa maana hiyo hata gharama zilizotumika kulijenga ni kubwa pia!! Lakini wakati huohuo huu ndio uhalisia wa huduma muhimu za kijamii madarasa, walimu na vifaa vya kufundishia havitoshi, wagonjwa wanalala chini, dawa hakuna na vifaa tiba pia maji safi na salama ni kitendawili sehemu kubwa ya nchi ukosefu wa ajira na kipato unasababisha wazazi wengi washindwe kuwapeleka watoto shule

Ukija kuangalia bajeti ya kukarabati nyumba ya gavana wa benki kuu au ikulu yetu unajiuliza kama watoa maamuzi wetu ni watu na akili zao au ni wendawazimu?
 

Attachments

  • 1417928822176.jpg
    7 KB · Views: 742
Mkuu ukikaa kuyawazia hayo...unaweza ukawa hayawani....kwa kuwa sasa hivi wameshika mpini wacha makali yatuumize......
Lakini amini nakuambia siku yao yaja.....siku ambayo watalia na kusaga meno.......
Siku ambayo watalia kilio kikuu.....
Siku ambayo watatamani ardhi ipasuke watumbukie ndani........LET US WAIT....hakuna marefu yasiyo na ncha....TIME WILL TELL.....
 
Cccmmmm hoyeeee maboya yanaitikia hoyeee nyambafu kabisa
 
Cha ajabu zaidi..... Mawaziri wakisafiri nje hupanda 1st Class (Biznes Class) ambapo wenyeji waliowalika hupanda Economy class !! + Allowance+Hotyel Accomodations, Misc Free !! Lakini wao hapa nyumbani wanacash $ papohapo !!
 
bajeti ya mavx V8 kwa mwaka bajeti ya vitafunio maofisini ....!!!bajeti hizi zingerekebishwa na ziada ikapelekwa kwenye hizi huduma
 
Kwa mtaji wa ujinga na umasikini wa walio wengi, wataendelea kutawala tu. Na hii ni kwa kuwa wengi wenye huo umasikini na ujinga hawajitambui, waoga, inakuwa rahisi kwa anaemtawala kumgeuza popote anapotaka, na hii ni hali halisi kwa mataifa mengi ya Afrika. Mtu mmoja aliwahi kusema: 'Africa is like a virgin for anyone to penetrate'. Tukiwa na utambuzi kuwa viongozi walioko wadarakani ni sisi ndio tumewaweka/tumewachagua, tutakuwa na nguvu ya kuwawajibisha, tofauti na jinsi ilivyo.
 
mshan jr
Bado kila mwaka wanakarabati jengo mara mbili, Sasa njoo uone gharama zake....Mamawee !!!
 
Last edited by a moderator:

Yaani hapo ni sawa na kusema tusiweke lami mjini mpaka tukamilishe madaraja yote vijijini! Hayo mawazo mgando
 
mshan jr
Bado kila mwaka wanakarabati jengo mara mbili, Sasa njoo uone gharama zake....Mamawee !!!

Mara ya mwisho nakumbuka ukarabati wa ikulu uligharimu BILIONI KUMI na nyumba ya gavana BILIONI SITA
 
Last edited by a moderator:
Walimchaguaje?,hoja na point zake hazigusi moyo kabisa.
 
Yaani hapo ni sawa na kusema tusiweke lami mjini mpaka tukamilishe madaraja yote vijijini! Hayo mawazo mgando

Hatuwezi kuwaza sawa hata siku moja ndio maana linaitwa jukwaa huru
 
mshana jr hizi picha hata uzione kila siku hazizoeleki lazima itauma tu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…