Baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau kuhusu ugonjwa huu
Mimi nina tatizo la ugonjwa wa Vitiligo, lips ya chini imebadilika colour na nyekundu kama nakunywa pombe kali, na kichwani nimetokewa alama nyeupe kama kishilingi, na shingoni nina alama ya mba na usoni nina kidoti cheupe
Naomba msaada wenu wataalamu.
Asanteni kwa kutusaidia kupitia forum hii.
---
Habari wanajukwa,
Kama nilivyoeleza hapo juu, Naomba msaada waushauri wa kitaalamu either wa tiba za asili au za kisasa juu ya tatizo la vitiglo kwa ambao wamesha experience na kujua japo ata kwa kuuthibiti usisambae zaidi au kupunguza.
Natanguliza shukrani
Fahamu zaidi kuhusu tatizo la vitiligo
Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi ambao unasababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe kwa sababu ya kupoteza melanin. Vitiligo inaathiri watu wa rangi yoyote ya ngozi japo kwa watu wengine huwa inaonekana zaidi kutokana na rangi yake ilivyo sanasana kwa watu wenye ngozi nyeusi. Pia inatokea katika umri wowote mara nyingi katika umri chini ya miaka 40.Dalili zake ni zipi
Mgojwa wa vitiigo hapati dalili zozote bali mfano maumivu, kuwashwa au homa bali mwenye vitiligo huanza kuona mabaka meupe au madoa yakijitokeza katika ngozi yake
Nini Chanzo cha ugonjwa wa vitiligo?
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ngozi katika Hospitali ya Rufaa Temeke, Claud Mango, anasema ugonjwa huo ambao pia huitwa leukoderma husababishwa na ukosefu wa chembe zinazotokeza rangi ya ngozi.
“Rangi ya ngozi ya kawaida huwa inatengenezwa na chembechembe zinazojulikana kama ‘melanocyte’ ambazo mtu anazaliwa nazo, hivyo ukizikosa ngozi inapoteza rangi yake.
“Sababu zingine ni za urithi lakini maana hasa ya ugonjwa huu ni kwamba wale askari waliokabidhiwa mwili waulinde wanakuwa hawalindi badala yake wanautafuna,” anasema Dk. Mango.
Anasema ugonjwa huo hauna dalili yoyote, hausababishi maumivu na wala hauambukizwi bali mtu huanza kuona madoa na mabaka meupe kwenye ngozi.
“Ugonjwa huu hautabiriki, leo unaweza kuja na mabaka machache lakini kesho vikasambaa, unaweza kuwa nab aka upande mmoja, pande mbili au pembezoni. Mara nyingi huwa unapendelea sana kushambulia kwenye viungo kuliko sehemu zingine za mwili,” anasema.
Dk. Mango anasema pia yako baadhi ya magonjwa ambayo yana uhusiano na ugonjwa wa vitiligo na kwamba mtu mwenye moja ya magonjwa hayo akipata vitiligo huwa haishangazi sana.
Anayataja magonjwa hayo kuwa ni goita, upungufu wa damu, watu wenye vipara na pumu ya ngozi.
“Mfano ukiwa na ugonjwa wa pumu ya ngozi unaweza kukufanya upate vitiligo, ngozi inakuwa na vipele vinavyowashwa mfululizo na unawapata watu ambao kwenye koo zao kuna pumu,” anasema.
Vitiligo ni tatizo ambalo linatokana na kupungua au kupotea kwa chembechembe zinazoipa ngozi rangi yake zijulikanazo kama melanin.
Kwa nini chembechembe hizo hupotea au kupungua?
Hutokea kama seli zinazohusika na kuzalisha melanin zikifa au zikipungukiwa na ufanisi wa kufanya kazi. Melanin zinahusika na kuwezesha nywele, ngozi na macho kuwa na rangi yake.
kwa nini hizo seli zinafeli kuzalisha melanin
Sababu za moja kwa moja hazijulikani ila kuna mambo ambayo yanasemekana kuwa yanachangia kupata tatizo la vitiligo nayo ni kama yafuatayo;
Madhara gani mtu mwenye vitiligo atapata?
- Athari kisaikolojia kutokana na kufikiria namna gani watu wanaomzunguka wanavyomchukulia
- Hatari ya kuathiriwa na jua inaongezeka kiasi kwamba hatari ya kupata hata kansa za ngozi inaongezeka
- Pia hatari ya kupata matatizo ya macho inaongezeka
Matibabu hutegemea na makubaliano ya mtu mwenye tatizo na daktari wake.
- Dawa za kupakaa ili kusaidia kusaidia uzalishaji wa melanin
- Kuchora tattoo ili kuzuia kuonekana kwa sehemu zilizoathiriwa (skin camouflage)
- Kupunguza melanin maeneo ambayo hayajaathiriwa ili kuleta ufanano na sehemu zilizoathiriwa (depigmentation)
- Upasuaji pia hufanyika (skin grafting)
- Ukiwa na tatizo hili ni vizuri kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist) ili uweze kusaidiwa pia ukiona dalili za tatizo hili inashauriwa kujilinda na jua na kutochora tattoo ambazo haujashauriwa na mtaalam wa magonjwa ya ngozi.
Baadhi ya maoni na ushauri uliotolewa na Wadau wa Jf
---Pole sana mkuu,
Sitaki kukukatisha tamaa ya kupona lakini ukweli ni kuwa vitiligo, (mabaka meupe mno) haitibiki. Ni miongoni mwa magonjwa ya auto immune, yaani kinga ya mwili inashambulia cells zinazoitwa melanocyte ambazo ndio zinazotengeneza rangi nyeusi tuliyonayo.
Shida hii ni kasoro ya kuzaliwa na inafata ukoo japo si kila mtu katika ukoo aweza pata. Shida hii inawapata watu wa rangi zote.
Na ajabu ni kuwa pamoja na kuwa wazungu ni weupe but akiwa na vitiligo huwa inaonekana wazi (very conspicious) Dawa nyingi zimejaribiwa but hakuna iliyoibuka tiba.
Baadhi ya watu wakitumia prednisolone au hydrocortisone ya kupaka waweza pata nafuu but ni baada ya muda mrefu.
Tiba ya uhakika ni kuikubali hali hiyo, na kuipuuza kwa sababu haiumi, wala haiwashi. Otherwise nimeona watu wakipoteza fedha nyingi na hawakupona.
Kama unaishi karibu na hospitali kubwa kama Muhimbili, KCMC, Bugando au Mbeya waweza pata ushauri wa Dermatologist.
---VITILIGO NI NINI? DALILI, CHANZO NA MATIBABU.
Ugonjwa wa vitiligo, ambao pia huitwa leukoderma, husababishwa pale chembe hai zinazotengeneza melanin zinapokufa au kuacha kufanya kazi. Hilo husababisha madoa na mabaka meupe kwenye ngozi. Huathiri watu wote japo hali hii huonekana kwa haraka zaidi kwa watu weusi.
Ugonjwa huo hausababishi maumivu wala hauambukizwi. Ugonjwa huu si hatari au kutishia uhai japo husababisha msongo wa mawazo na mtu kujihisi vibaya au kujiona ana upungufu.
Hata hivyo, matibabu ya ugonjwa wa vitiligo huimarisha muonekano wa ngozi kuwa mzuri japo. Ugonjwa halisi hauwezi kupona na kutoweka.
Dalili za Vitiligo
Mojawapo ni kupotea kwa rangi halisi na kuota mabaka kwenye ngozi. Tatizo huanzia kujitokeza kwenye sehemu za mwili zinazopigwa na jua zaidi kama mikono, miguu, viganja, uso na midomo hasa ‘lipsi’.
Dalili zake ni ngozi kupoteza rangi halisi, kuwa na weupe au rangi ya kijivu (gray) sehemu ya ngozi ya kichwa, kope za macho au nyusi. Kupotea kwa rangi ya ngozi ya sehemu ya ndani ya mdomo au pua. Kubadlika kwa rangi ndani ya jicho. Pia kuwa na mabaka makwapani, kitovuni na sehemu za siri.
Vitiligo huanza katika umri wowote lakini mara nyingi ugonjwa huonekana kabla ya kufika miaka 20. Sehemu moja au chache za mwili ya vitiligo aina hii hutokea eneo moja tu la mwili. Hata hivyo, ni vigumu kujua kiwango cha kusambaa kwa hali ya kupoteza rangi ya ngozi. Wakati mwingine mabaka huweza kupona bila hata ya kutumia dawa au matibabu yoyote.
Aidha mara nyingi hali ya kupoteza rangi huendelea na husambaa maeneo zaidi ya mwili na mara chache sana ngozi hurejea katika hali ya awali.
Chanzo
Ugonjwa wa vitiligo hutokea pale chembe hai zinazozalisha melanin zinapokufa au kuacha kufanya kazi. Melanini huipa ngozi, nywele na macho rangi yake ya asili. Madaktari hawajaweza kufahamu sababu ya kufa au kushindwa kufanya kazi kwa chembe hai hizi lakini hali hii huweza kuhusishwa na mfumo wa kinga ya mwili kushambulia na kuharibu kimakosa chembe hai hizi ambazo huzalisha melanin.
Matatizo ya vitiligo
Watu wenye ugonjwa huu huwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na matatatizo ya kisaikolojia na msongo wa mawazo.
Huhisi kuungua zaidi na jua pamoja na saratani ya ngozi. Wana matatizio ya macho. Kadhalika kushindwa kusikia kikamilifu.
Pia hupata madhara yaletwayo na utumiaji wa madawa ya kutibu ugonjwa huu kama kukauka sana kwa ngozi pamoja na muwasho.
Matibabu
Yapo matibabu ya aina nyingi na ambayo husaidia katika kurejesha rangi ya awali ya pamoja na ubora wa ngozi japo matokeo ya matibabu hayo hutofautiana na ni vigumu kutabiri ufanisi. Badhi ya matibabu huweza kuwa na madhara makubwa kwa hiyo daktari wako huanza kwa kukushauri utumie dawa nyepesi za kujaribu kuboresha muonekano wa ngozi kama ‘make-up’.
Iwapo mgonjwa na daktari watakubaliana kuanza matibabu makubwa ya madawa basi uponyaji huweza kutumia miezi kadhaa kuonekana na wakati mwingine kutumia aiana nyingi za matibabu.
CRYSTAL CELL NA TRIPLE 3-MIRACLE INTENSE ESSENCE ni dawa zinazoweza kusaidia kuzuia vitiligo kuendelea kutokea yaani kupoteza kwa chembe zinazosababisha rangi halisi ya ngozi. Pia, huweza kuboresha muonekano wa ngozi ukawa mzuri.
kwa mawasiliano zaidi ya whatapp 0682315816.
Mgonjwa anapaswa kumwona daktari mara tu unapoona hali ya kupoteza rangi ya ngozi, nywele au macho. Ugonjwa wa vitiligo hauna tiba ila ukiwahi husaidia kuzuia au kupunguza hali ya ngozi kuharibiwa.
Matibabu hutegemea na makubaliano ya mtu mwenye tatizo na daktari wake.
1. Dawa za kupakaa ili kusaidia kusaidia uzalishaji wa melanin.
2. Kuchora tattoo ili kuzuia kuonekana kwa sehemu zilizoathiriwa (skin camouflage).
3. Kupunguza melanin maeneo ambayo hayajaathiriwa ili kuleta ufanano na sehemu zilizoathiriwa (depigmentation).
4. Upasuaji pia hufanyika (skin grafting). Ukiwa na tatizo hili ni vizuri kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist) ili uweze kusaidiwa pia ukiona dalili za tatizo hili inashauriwa kujilinda na jua na kutochora tattoo ambazo haujashauriwa na mtaalam wa magonjwa ya ngozi.
Pia soma
- Leleti Khumalo (Sarafina) Star anayeishi na gonjwa linalowasumbua wengi lisilo na tiba(Vitiligo)