Fahamu zaidi kuhusu brachymetatarsia

XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
4,293
6,956
Habari wakuu,

Brachymetatarsia ni hali inayo sababisha vidole vya miguu kuwa vifupi (itaitwa brachymetapody kama itakuwa ni zaidi ya kimoja ). Ni hali ambayo hurithiwa kutoka kwa mzazi, kwa kawaida hakuna anaye zaliwa na hii hali bali hujitokeza pale ambapo mara nyingi mtoto anapokua amefikisha kuanzia umri wa miaka 7 - 9.

Kwa asilimia kubwa hali hii huwakumba sana wanawake japo kuwa hata wanaume pia hupata hili tatizo. Tatizo hili hutokea pale ambapo growth plates kwenye mifupa ya vidole kufunga kabla ya muda wake na kusababisha kidole au vidole kuacha kukua huku vingine pamoja na mguu vikiendelea kukua.

Asilimia kubwa ya watu wenye tatizo hili huepuka sana kuvaa open shoes wakihofia ku expose miguu yao kwa watu wengine, huku wengine wakishindwa kuvaa aina fulani ya viatu kwa sababu ya maumivu (kwa wale ambao vidole vyao hupanda juu).

NB: Tatizo hili linaweza kutibika kwa surgery, njia maarufu zinazotumika ni pamoja na external fixator, bone graft surgery etc .. View attachment 1852885
images%20(1).jpg


Sent from my itel W5002 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom