Fahamu zaidi juu ya ndege Bundi

Fahamu zaidi juu ya ndege Bundi

Sio kusense kitu kinachoanza kuharibika mkuu,Bundi ana uwezo wa kusense dead cells za mtu anapokaribia kufa kwahiyo ndio maana wanamzushia kuwa akitua kwako kuna mtu ataondoka,ana uwezo wa kusense hata siku mbili au tatu kabla huyo mtu hajakufa...
bundi analia kwangu kivule msiba wa mjomba unatokea iringa,how this[emoji55][emoji55]
 
Swet-R, Utakuwa unapenda wanaume wenye saut nzito kama mm. Bundi ni ndege kama ndege wengine. Sema anauwezo wa kunusa dead sells. Kama kuna mahali kuna mtu mgonjwa mahututi seli zake zimeanza kufa, bundi anauwezo wa ku detect na kusogelea maeneo ya karibu akidhan anaweza kupata mawindo yake ambayo mara nyingi ni wanyama wadogo wadogo kama panya, popo na wengine wa jamii hiyo.
 
Dah hapo uliposema spider umenikumbusha movie moja hivi inaitwa spider man nliiangalia kitambo
Dah hapo ulipomalizia Falcon, umenikumbusha basi nililokuwa napanda enzi hizo naenda Nairobi, Falcon Bus....na mwenzie Spider
 
Ukikuta kataga Mayai yake chukua Boksi yaweke Kisha Funga na kufuri ondoka..... Akilejea Bundi atayatoa Mayai bila kuvunja Boksi wala Kufuri lako..... Ila juu ya Boksi lako utakuta Mzizi au mti ambao yeye ndio katumia..... Ni ndege Hatari sana......

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu niliwahi kupata hii stori lakini nilivyoipata mimi ilikua nikwa ndege anaeitwa Dudu mizi,

Kwamba kuna mti au kijiti ambacho wezi hukitafuta kwakua inasemekana kua kijiti hiki huweza kuunlock sehemu yoyote ile kwa kukigusisha kwenye hizo locks.

Na inesemekana kua ndege Huyu Dudumizi ndie pekee anaeweza kukipata huko maporini, sasa ili uweze kukipata

Inabidi mfanye jitihada zakutafuta niwapi dudumizi wanataga mayai yao na nakisha kusubiri atotoe hapo sasa mnakwenda kuvifungia vitoto vyake Kwa kamba yoyote ngumu palepale kwenye kiota chake nakisha kuondoka.

Sasa inasemekana kua anapokuja nakukuta wanawe wametaitiwa hutoka kwenda huko anapopajua mwenyewe nakisha anaporudi hurudi nahiko kijiti ambacho yeye hugusisha tu kwenye vile vifundo navyo huachia kisha kuchukua wanawe nakuhama.

Sasa anapomaliza kufungua inasemakana kua huachia hivyo kijiti maeneo yahapo hapo, ndipo Wale waliotega huja kukisaka kwaajili yakazi zao.

Hizi nistori tulizopewa nawakubwa zetu sijawahi kuzithibitisha.
 
Ni maswala ya imani tu. Nchi kama uingereza, bundi ni ndege wa bahati tofauti na kwetu ambapo ni ndege wa mikosi na nuksi. Pia baadhi ya makabila nchini hispania, bundi huchinjwa kama kitoweo kwa wageni wale wa heshima.

duuh kwa kwl apo ni imani
 
Sio kusense kitu kinachoanza kuharibika mkuu,Bundi ana uwezo wa kusense dead cells za mtu anapokaribia kufa kwahiyo ndio maana wanamzushia kuwa akitua kwako kuna mtu ataondoka,ana uwezo wa kusense hata siku mbili au tatu kabla huyo mtu hajakufa...

ohooooo apo nimkupata vyema
 
Aloo unanikumbusha tanga, wilaya ya pangani , kijiji cha Sange ,
Aisee hawa ndege wamejaa sana , alafu wanakiburi ile mbaya, unaweza mkuta juu ya mti na asikimbie mpaka umkaribie kabisa .
Kuna siku nilimkuta juu ya mkorosho nikajaribu kumlenga na kuni, alichofanya ni ameruka juu kwenye tawi kubwa na kuanza kuniangalia , nikamuacha
 
Kuna mtu mmoja wizara ya pesa alikua anajitia mnoko na mfitini sana. Basi kuna mtu kachukua bundi hai. Kamvunja miguu na mabawa akiwa hai na kumfunga kitambaa chekundu mguuni na kilemba cheusi kichwani halafu kwa siri kubwa akavitumbukiza kwenye droo ya mnoko. Mbona palichimbika bila jembe mpaka mnoko akah
Kuna mtu mmoja wizara ya pesa alikua anajitia mnoko na mfitini sana. Basi kuna mtu kachukua bundi hai. Kamvunja miguu na mabawa akiwa hai na kumfunga kitambaa chekundu mguuni na kilemba cheusi kichwani halafu kwa siri kubwa akavitumbukiza kwenye droo ya mnoko. Mbona palichimbika bila jembe mpaka mnoko akahamishwa idara.
😂😂😂😂
 
Huyo hapo
IMG-20191110-WA0006.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika moja ya kundi la viumbe hai walio wa ajabu zaidi; basi bundi hawezi kukosekana.

Bundi kama walivyo jamii nyingine ya ndege chimbuko lake ni yai. Mayai ya bundi huchukua mpaka siku thelathini mpaka kuja kutoa kifaranga. Katika utotoaji kifaranga wa bundi kawaida anaweza kuchukua mpaka masaa 48 tangu kutengeneza ufa katika ganda yai mpaka kujitotoa kabisa. Kifaranga atotolewapo huchukua mpaka siku tatu macho yake kufunguka na week 2 mpaka kupata uono wa kawaida.

Kifaranga kawaida anaweza kuanza kuifunza namna ya kuruka na kuwinda vitu vilivyo vidogo vidogo kama minyoo, panzi na kadhalika.

Bundi ni mmoja kati ya ndege hodari zaidi katika mawindo. Macho yake yaliyo na nguvu humsaidia katika kuona windo lake hata akiwa katika umbali mrefu au chini ya nyasi ama barafu. Macho ya bundi yanachukua asilimia 75% ya eneo lote la fuvu la kichwa chake ukilinganisha na ukubwa wa macho ya binadamu yanayochukua asilimia 5% ya sehemu yote ya fuvu la kichwa. Ni ajabu kwa kiumbe huyu pia kuwa na uwezo wa kugeuza kichwa chake pande zote kwa nyuzi 270° pasipo kuhusisha mwili mzima.

Hali hiyo inamlazimu kwa sababu ya jicho lake kutokuwa katika umbo la mduara kuruhusu kuzunguka kama ilivyo kwa viumbe wengine.Pia anauwezo mkubwa wa kuona wakati wa usiku zaidi kuliko mchana kutokana na ukubwa wa macho yake yenye nerves zenye kumuwezesha kuona zaidi usiku ambapo uwezo wake wa kuona usiku ni 2½ zaidi ya binadamu.

Pamoja na uoni hafifu wakati wa mchana bundi hulazimika kufanya mawindo yake mchana hasa wakati wa hali mbaya ya hewa kama baridi kwa sababu manyoya yake yasiyoweza kumlinda zaidi katika vipindi hivyo vya baridi au wakati wa mvua.

Nini kinamsaidia kujua windo lilipo? Bundi anauwezo mkubwa wa kusikia pamoja na sensi zilizo katika manyoya ya kichwani inayoweza kufahamu wapi windo linapatikana.

Pia, bundi anauwezo mkubwa wa kumfikia windo lake pasipo kutoa sauti yoyote ya mapigo ya mabawa wakati wa kupaa tofauti na ndege wote. Hiyo hutokana na ukubwa wa mabawa yake yanayozidi mwili na manyoya mepesi yanayomfanya awe na mapigo ya mabawa yasiyo na sauti na mwezo wa wastani ukilinganisha na ndege wengine wawindao kama falcon na eagle.

=====
MJUE VIZURI BUNDI..

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana. Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo. Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu. Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili. Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana. Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi. Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji. Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu. Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu. Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU!!!

Nawaambia ukweli bundi anahusika na uchawi nimeishi vijijini kwa akili ya kawaida haiwezekani bundi analia nyumbani kwa ko tena wanne halafu mtu anapata ajali anakufa mnazika hapo utasema bundi ananusa hapana mura
 
Anaweza tu kuwa anatumiwa na washirikina kama wanavyotumiwa wanyama na ndege wengine kama njiwa, fisi, paka na pengine hata kunguru. Ila kiuasilia ni ndege mmoja mpole tu. Pamoja na hayo; bundi mara nyingi amelia karibu na nyumba nayokaa wala hatukusikia lolote baya kwetu wala kwa jirani.
 
Habarini wanaJF,

Nafikiri kila mtu (ukiacha watoto wa kishua) anamfahamu ndege wa ajabu aitwaje Bundi.

Huyu ni ndege wa ajabu kutokana na mambo makuu yafuatayo:-

1. Akilia hutoa machozi ya damu

2. Ana uwezo mkubwa wa kusense mifupa au nyama zinazooza na zilizooza.

Ukiona mahali kila mara Bundi analia usiku, jua kwamba hapo kuna marehemu mtarajiwa. Hasa kama mnamuuguza mgonjwa kwa muda mrefu ambaye baadae siku zake zinakuwa zimefika.

In most cases, binadamu wa kifo cha namna hiyo hutanguliwa na baadhi ya viungo vyake mwilini kuanza kuoza huko ndani.

Bundi anao uwezo mkubwa wa kunusa / ku-sense hivyo vitu vinavyoanza kuoza ndo maana anakuwa kila wakati anasubiri huo 'mzoga tarajiwa'.

Ukiona bundi analialia sana usiku maeneo fulani, hesabu siku tu, utasikia kuna mtu kafariki.

download-2.jpeg
download-1.jpeg
download.jpeg
 
Yale siyo machozi ya damu. Ni rangi tu ya vilainishi vya macho. Pia kila kitu ni Imani tu. Bundi Ni ndege wa kawaida Kama walivyo ndege wengine. Kuhusu mlio, kila species ya kiumbe ana mlio wake unique hivyo huwezi leo kulazimisha mlio wa bundi ufanane na wa kuku. Nakushauri achana na hizo Imani za watu wa Zamani. Siku hizi Kila kitu ni research.
 
Back
Top Bottom