Fahamu vipimo mbalimbali vya picha vinavyotumika hospitalini kuchuguza magonjwa

Dr Norman

Member
Oct 6, 2019
11
40
Katika tiba vipimo vya radiolojia ni muhimu sana kwenye uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, vipimo vingine hutumika kama tiba. Hivi ni baadhi ya vipimo ambavyo hutumika hospitalini.

NB : Vipimo hutofautiana ufanisi wa kuangalia viungo vya ndani.

QQhmItr.jpg


1. KIPIMO CHA ULTRASOUND

Ultrasound ni kipimo ambacho hutumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha ya viungo vya ndani ya mwili. Hutumika kufanya uchunguzi wa magoonjwa mbalimbali, kugundua visababishi vya maumivu, kuvimba au maambukizi kama majipu ya ndani. Pia hutumika kuchukua sample za tishu kwa ajili ya kupima maabara.

Hutumika zaidi kwa wakina mama wajawazito kufutatilia ukuaji wa mtoto tumboni. Kipimo cha ultrasound hakitumii mionzi, ni kipimo salama zaidi hakina madhara yoyote

e1390375-f5b0-4893-9edf-3d36671ec508.jpg


2. KIPIMO CHA X RAY

Hiki ni kipimo cha haraka, kisicho na maumivu ambacho hutumia mionzi kuangalia viungo vya ndani mwili hasa mifupa.

Mionzi ya X-ray inapopita mwilini hunyonywa na kuakisiwa tofauti tofauti kadiri inavyopita ogani moja kwenda nyingine. Ogani ngumu kama mifupa huakisi mionzi hii na kutengeneza picha nyeupe, mapafu kwa sababu ya hewa hupitisha miozi hii hivyo hutoa picha nyeusi.

X-ray hutumika zaidi katika wodi za mifupa kuangalia mivunjiko ya mifupa. Hutumika kuangalia magonjwa mengi kwenye mapafu, tumbo , utumbo nk.

NB: X-ray si salama kwa mama mjamzito iwapo huhitajika lazima mtoto alindwe

xrayimages.jpg


3. KIPIMO CHA CT SCAN

CT Scan ni kipimo kikubwa na kisasa ambacho hutumia muunganiko na mlolongo wa picha nyingi za X-ray zilizochukuliwa katika pembe (angle) tofauti tofauti na kuhaririwa na compyuta kutoa picha kamili ya viungo vya mwili. CT Scan hutoa picha ya viungo vya ndani katika vipande (slices) vidogo vidogo.

CT Scan hutoa taarifa nyingi zaidi ya picha X-ray. Hutumika kuchunguza magonjwa mbalimbali hasa saratani/uvimbe na kusaidia madaktari kupanga matibabu stahiki. Hutumika katika dharura kwa watu waliopata ajari ili kuangalia kama ubongo umepata majeraha au damu imevilia kichwani na kwa waliopata kiharusi kuangalia kama damu imevilia kichwani

Kwa kawaida mtu anapopiga CT Scan hupata dozi kubwa ya mionzi kuliko X-ray; dozi hii ni wastani wa mara 1000 zaidi ya X-ray. Lakini dozi mara moja huwa haileti madhara.

Kipimo cha CT scan kinapatikana nchini.

ct-computed-tomography.jpg


4. KIPIMO CHA MRI

MRI ni kifupi cha Magnetic Resonance Imaging; kipimo hiki hutumia nguvu kubwa ya usumaku picha za viungo vya ndani ya mwili.

MRI hutumika kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya mwili hasa kuchunguza uvimbe kwenye ogani kama ubongo, tumbo, utumbo, uti wa mgongo nk.

MRI ni kipimo salama kabisa lakini kwa sababu ya kutumia sumaku kubwa hakitumiki kwa watu wenye betri ya moyo, watu waliowekewa magoti bandia.

Kipimo cha MRI kinapatikana hospitali kubwa kama Muhimbili

MRI.jpg


download (2).jpg
 
NHIF inacover huduma zote ila kwa MRI utahitaji kibali Chao kabla ya kufanya.

Package za bima nyingine sizifahamu.
Shukran Dr.

Ninapoenda kufanya checkup ya mwili mzima nizingatie vipimo gani hasa ambavyo vitaniwezesha kuijua afya ya mwili mzima na matatizo yake?
 
Dr. Ebu kacheck reference zako vizuri, X-Ray haijagundiliwa na Marie Curie. Hiyo imegunduliwa na Roentgen ni German scientist. Maria Curie alifanya ugunduzi kwenye issue za Radioactivity, radioactive material.
Ugunduzi wa msingi kutumia mionzi katika tiba ulifanywa na mwanamama mwanasayansi Marie CURIE kutoka Poland, aligundua X Ray na alitumia katika vita ya dunia kutibia wanajeshi walioumia vitani. View attachment 1262892
 
Sawasawa ndugu niliteleza nilimaanisha matumizi ya x ray katika tiba yalihasisiwa na Marie Curie, alitengeneza mashine zinazotembea aliziita Little Curie ili kupiga wanajeshi walioumia
Dr. Ebu kacheck reference zako vzr, X-ray haijagundiliwa na Marie Curie. Hiyo imegunduliwa na Roentgen ni German scientist. Maria Curie alifanya ugunduzi kwenye issue za Radioactivity, radioactive material.
 
Back
Top Bottom