Fahamu tofauti ya Virusi na Bakteria

Fahamu tofauti ya Virusi na Bakteria

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
581
Reaction score
1,739
Hivi naweza kuviita vijidudu viwili vimekua vikileta shida na matatizo sana katika mwili wa binadamu toka enzi na enzi.

Virus (Kirusi) ni mdudu ambae hawezi kuzaa ama kua na athari bila ya kuwapo ndani ya seli hai za mwili wa mwanadamu (seli nyeupe)

Bacteria ni mdudu ambae anaweza kuishi sehemu nyingi ndani na nje ya mwili wa binadamu ambapo baadhi yao huleta magonjwa na wengine hutumika katika kusaidia hatua mbali mbali ndani ya mwili wa binadamu.

Virus ni vidogo zaidi ya Bacteria na vyote huitaji kua na Microscope ili uweze kuwaona.

Virusi
Virusi toka karne na karne wamekua wakileta athari kubwa sana na tiba yake ni ngumu kupatikana kwa urahisi kutokana na uwezo wake wa kuishi ndani ya Cell ya binadamu. Kwa kifupi ni kwamba ili uweze kuua kirusi inabidi uuwe cell za mwili kwavile virusi huweza kuzaliana na kufanya kazi vikiwa ndani ya seli za kiumbe hai.

Mfano wa Virus ni kama HIV virus, Corona Virus, Ebola, Small pox, Hepatitis na wengine wengi ambao huitaji kinga ili uweze kuwadhibiti.

Kama hapo mwanzo nilivoandika virus huweza kuishi ndani ya Cell za mwili zilizo hai hivo kupelekea kupata tiba yake kua ngumu.

Virusi vya ukimwi vimekua vikishambulia seli nyeupe zinazotumika kama kinga ya mwili, huweza kuingia ndani ya hii seli kuidhohofisha kisha kuia na kuhamia katika seli nyingine hivo ili uweze kutibu ukimwi unapaswa kutafta dawa ya kuua hiki kirusi kikiwa ndani ya celi nyeupe muhimu za mwili bila ya kuathiri hizi seli nyeupe.

Baada ya kua na changamoto kubwa ya kupata dawa za hizi Virus ndio ikaweza kutaftwa njia mbadala ya kuwekewa Kinga ili usipate baadhi ya magonjwa yanayoenezwa na Virus.

Corona pia imekua ngumu kupata tiba yake moja kwa moja hivo wanasayansi hutibu zile dalali za mwanzo kama mafua, kikohozi, ukosefu wa pumzi mpaka kupelekea mtu kupona.

Virus wengi asili yao ni wanyama na ndege kama vile kirusi cha Corona kinashabihana na Popo kwa 90%, kirusi cha ukimwi kinashabihana na sokwe hivo hivo virusi vya mafua ya ndege na nguruwe na hii hutokana na kuishi ama kua karibu na wanyama sana kwa muda mrefu.

Bacteria
Bacteria wameko katika makundi mengi lakini katika mwili wa binadamu kuna ambao huitajika kusaidia baadhi ya shughuli za kimwili na kundi jingine ni ambao husababisha magonjwa.

Bacteria wenyewe huweza kuishi ndani na nje ya miili yetu, pia mwili wa binadamu hauwezi kuishi bila ya bacteria na kuna kiwango huitajika mwilini.

Kuna bacteria walioko tumboni ambao husaidia kusaga chakula na wengine wengi hupatikani katika ngozi.

Bacteria kwenye mwili wa binadamu wako wengi zaidi ya seli hai za miili zetu

Baadhi ya Bacteria huweza kusababisha madhara kama ‘food poison’.
 
Yaani hawa wachina! Kula kula kwao hadi popo, na wanyama wengine kumetugharimu. Asante kwa andiko la virusi na bakteria
 
Walipigwa na Njaa sana miaka ya 70 wakawa wanakula kitu chochote chenye uhai, mambo yakarudi sawa lakini wakashindwa kuacha kula visivoliwa
 
Hivi kwa nini watu wengi tunashindwa kuelewa? Hivi unaanzaje virus au bacteria kumuita mdudu? Hivi unataka kusema viruses are under insecta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda wewe ungetuambia Virus na Bacteria ni nini?
Virusi ni chembe ndogo sana iliyoundwa na maada jenetiki, kama DNA au RNA, katika koti la protein

Bakteria ni viumbehai vidogo sana vyenye seli moja ambavyo hustawi katika mazingira tofauti na huonekana kwa hadubini pekee.

Ukitumia neno mdudu unafail mkuu. Wadudu ni insects hivyo ni never ever bacteria or virus be insects. Hii ni lugha ya layman.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hv corona anapewa "shikamoo", halafu hao wengine wanapewa "mambo zenu.?"
 
Hivi kwa mfano kirusi na bacteria wakidundana nani anamtoa mwenzake knock out?
 
Virusi ni chembe ndogo sana iliyoundwa na maada jenetiki, kama DNA au RNA, katika koti la protein

Bakteria ni viumbehai vidogo sana vyenye seli moja ambavyo hustawi katika mazingira tofauti na huonekana kwa hadubini pekee.

Ukitumia neno mdudu unafail mkuu. Wadudu ni insects hivyo ni never ever bacteria or virus be insects. Hii ni lugha ya layman.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtoa somo angetumia hiyo lugha uliyoitumia sisi ma layman wenzake tusingemuelewa kwa wepesi
 
Safi sana ila apo kwenye Connection ya Sokwe na HIV dah!!!
Hivi naweza kuviita vijidudu viwili vimekua vikileta shida na matatizo sana katika mwili wa binadamu toka enzi na enzi.

Virus (Kirusi) ni mdudu ambae hawezi kuzaa ama kua na athari bila ya kuwapo ndani ya seli hai za mwili wa mwanadamu (seli nyeupe)

Bacteria ni mdudu ambae anaweza kuishi sehemu nyingi ndani na nje ya mwili wa binadamu ambapo baadhi yao huleta magonjwa na wengine hutumika katika kusaidia hatua mbali mbali ndani ya mwili wa binadamu.

Virus ni vidogo zaidi ya Bacteria na vyote huitaji kua na Microscope ili uweze kuwaona.

Virusi
Virusi toka karne na karne wamekua wakileta athari kubwa sana na tiba yake ni ngumu kupatikana kwa urahisi kutokana na uwezo wake wa kuishi ndani ya Cell ya binadamu. Kwa kifupi ni kwamba ili uweze kuua kirusi inabidi uuwe cell za mwili kwavile virusi huweza kuzaliana na kufanya kazi vikiwa ndani ya seli za kiumbe hai.

Mfano wa Virus ni kama HIV virus, Corona Virus, Ebola, Small pox, Hepatitis na wengine wengi ambao huitaji kinga ili uweze kuwadhibiti.

Kama hapo mwanzo nilivoandika virus huweza kuishi ndani ya Cell za mwili zilizo hai hivo kupelekea kupata tiba yake kua ngumu.

Virusi vya ukimwi vimekua vikishambulia seli nyeupe zinazotumika kama kinga ya mwili, huweza kuingia ndani ya hii seli kuidhohofisha kisha kuia na kuhamia katika seli nyingine hivo ili uweze kutibu ukimwi unapaswa kutafta dawa ya kuua hiki kirusi kikiwa ndani ya celi nyeupe muhimu za mwili bila ya kuathiri hizi seli nyeupe.

Baada ya kua na changamoto kubwa ya kupata dawa za hizi Virus ndio ikaweza kutaftwa njia mbadala ya kuwekewa Kinga ili usipate baadhi ya magonjwa yanayoenezwa na Virus.

Corona pia imekua ngumu kupata tiba yake moja kwa moja hivo wanasayansi hutibu zile dalali za mwanzo kama mafua, kikohozi, ukosefu wa pumzi mpaka kupelekea mtu kupona.

Virus wengi asili yao ni wanyama na ndege kama vile kirusi cha Corona kinashabihana na Popo kwa 90%, kirusi cha ukimwi kinashabihana na sokwe hivo hivo virusi vya mafua ya ndege na nguruwe na hii hutokana na kuishi ama kua karibu na wanyama sana kwa muda mrefu.

Bacteria
Bacteria wameko katika makundi mengi lakini katika mwili wa binadamu kuna ambao huitajika kusaidia baadhi ya shughuli za kimwili na kundi jingine ni ambao husababisha magonjwa.

Bacteria wenyewe huweza kuishi ndani na nje ya miili yetu, pia mwili wa binadamu hauwezi kuishi bila ya bacteria na kuna kiwango huitajika mwilini.

Kuna bacteria walioko tumboni ambao husaidia kusaga chakula na wengine wengi hupatikani katika ngozi.

Bacteria kwenye mwili wa binadamu wako wengi zaidi ya seli hai za miili zetu

Baadhi ya Bacteria huweza kusababisha madhara kama ‘food poison’.
Nyama ale Mchina Kunawa tunawe Dunia nzima tena kwa Sanitizer
 
Back
Top Bottom