Fahamu tafsiri sahihi ya "computer" kwa kiswahili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu tafsiri sahihi ya "computer" kwa kiswahili.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Remote, Jul 15, 2011.

 1. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Waswahili wengi hufikiri kwamba hakuna maana halisi ya computer na badala yake wanatohoa neno hilohilo nakuandika "Kompyuta". Hivyo ni makosa maana halisi ya Computer ni neno "NGAMIZI" na kwa laptop computer huitwa "NGAMIZI PAKATWA" Source: Ulimwengu wa kiswahili TBC1, Nawasilisha.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  tarakilishi ni nini?
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,725
  Likes Received: 8,288
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilidhani vivyohivyo!
   
 4. M

  Mtata Mbosa Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni jibu sahihi """TANAKILISHI"""
   
 5. r

  rununu Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mh! nakumbuka kuna mtu alishawahi kusema, je TARAKILISHI na NGAMIZI ni sawa? maana mimi naifahamu kuwa ni Tarakilishi
   
 6. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Nawalaumu sana hao wanatoa tafsiri za maneno na vitu mbalimbali. Tukiangalia kwa uzuri lugha ni muingiliano wa lugha mbalimbali. Ndio maana tuna maneno bora kama shati, meza, chai, pesa, hela, gari n.k. Hivi kwa nini fan iitwe pangaboi badala ya feni tulivyozoea? Computer ingekuwa komputa, television ingekuwa televisheni, fax mashine ingekuwa faksi n.k. Hakuna ubaya kuiga. Lugha zote zinaiga.
   
 7. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Congo nakubaliana na wewe ila nafikiri computer ingeitwa kompyuta badala ya komputa!
   
 8. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  La muhimu hapa kwa mawazo yangu ni kuwa kitu tumekitumia kwa miaka nenda rudi kwa jina fulani. Wataalamu wanakuja na majina ya ajabuajabu. Ah nimekumbuka, calcultor inaitwa kikokotozi, ovyo kabisa. Tungesema kalikuleta. Asante.
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Eti kiwembe cha kuchongea pencils kinaitwa KIFIRIO. Duh kazi kweli kweli.
   
 10. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ninajaribu kukuelewa: unaona kama ni kupoteza wakati na rasilimali kutafuta tafsiri ya 'Kiswahili' ya maneno hasa yanayohusiana na sayansi na teknolojia. Unadhani hakuna haja ya kuwa na istilahi mpya, unataka tuendelee na 'utohozi'.

  Sioni shida sana ingawa sikubaliani na wewe kwenye baadhi ya maeneo.

  Lakini, huu u--'hovyo' unaouona umeutoa wapi?
   
 11. r

  rununu Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Nakubaliana na wewe kabisa lugha hukua hasa ukizingatia kuwa tupo katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na kuwa kuongeza istilahi si lazima utohoe au uangalie mazoea ya matumizi ya neno husika, tutatohoa hadi lini wakati uwezekano wa kutafuta istilahi mpya upo? kiswahili si maskini kiasi cha kutohoa kila neno, mimi naona ni vema kutumia haya maneno mapya kuliko yale tuliyoyazoea, na tuache kutumia lugha ya kiswahili kwa mazoea.
   
 12. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swahili kina wenyewe.
  Ndio muwatafute majibu mtayapokea ya kutosha . Watu wa bara swahili wapi na wapi?
   
 13. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ni sawa kabisa
   
 14. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2014
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kiswahili raha
   
 15. aka2030

  aka2030 JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2016
  Joined: Jan 5, 2013
  Messages: 1,165
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  point tupu
   
 16. C

  COMFORT JAFFER JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2016
  Joined: Dec 30, 2015
  Messages: 213
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ni jina la sifa la Kompyuta {NGAMIZI}. NGAMIZI ina kazi kubwa 3. kazi moja kati ya hizo ni kuwa inatumika kama kitarakilishi. Isipokuwa haifai kuiita hivyo kwa kuwa hiyo ni sifa miongoni mwa sifa zake. Kwa maana nyingine tutakuwa na majina mengi tukifuata kila sifa ya NGAMIZI kuwa ni jina lake. Ukiita kwa jina la Kitarakilishi mimi naweza kuiita kwa jina la Kikumbukishi {data storage} na bado nitakuwa sahihi ila si jina lake. Mimi nae maneno meengi kama niko Mjengoni
   
 17. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2016
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,135
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna mgongano wa kiswahili cha kenya na tanzania. Kenya computer kiswahili chao ni tarakilishi, na Tanzania ni ngamizi.
  Kumbuka kenya wanapenda kupita kwenye njia yao ya kiswahili kwa sababu wameshautangazia ulimwengu kwamba chimbuko la kiswahili ni kenya.Na ulimwengu umeamini hivyo kiasi kwamba akihitajika mtaalamu wa kiswahili simu hupigwa Nairobi.
   
 18. k

  klf Member

  #18
  Apr 16, 2016
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Napenda kujulisha wanaoshirki sehemu ya Lugha kwamba mimi peke yangu nimetunga Kamusi Fupi ya Istilahi ya Ngamizi/Tarakirishi. Kwa wakati huu sokoni hakuna kitabu cha namna hii kinachopatikana.
  Mtu awe yeyote mwenye hamu ya kuwa na toleo la kitabu hicho (bure bilashi) kwa njia ya mtandao aombwe kuwasilisha nami klfmzungu@gmail.com. Nia yangu ndio kujaribu kuboresha hali kimsamiati ya Kiswahili. Tukishirikiana kwenye mradi huu hakika hadhi ya lugha hiyo itapata nafuu kubwa. Mimi mwalimu mstaafu MwIrish ambaye nimefundisha KiIngereza nchini TZ na Kenya kwa miaka ishirini hivi. Kwa muda mrefu sasa mvuto wa KiSwahili kwangu haupunguka hata kidogo.
   
Loading...