Fahamu namna ya kuingia deep web & dark web

NAINGIAJE DEEP WEB?
Kuingia deep web ni rahisi kuliko unavyofikiri. In fact, inawezekana tayari umewahi kuingia deep web ila hujui kama uliingia. Sema tu watu wengi wanashindwa kutofautisha baina ya DEEP WEB na DARK WEB - majina mawili yanayofanana lakini yenye maana mbili tofauti. Bila shaka ungependa kufahamu utofauti, si ndio? Twendzetu...

DEEP WEB NI NINI?
Watu wengi wanachanganya baina ya deep web na dark web/ dark net. Kwa lugha nyepesi, deep web ni taarifa zote ambazo zimehifadhiwa mtandaoni ambazo hazijawa indexed na search engines. Huhitaji kutumia special tools zozote au dark net browser kuingia kwenye deep web; unahitaji tu kujua ni wapi kwa kutafuta. Specialized search engines, directories, na wikis zinaweza kuwasaidia watumiaji kupata data wanazozitafuta.

Taarifa nyingi zimefichika kwasababu watu wengi wanaotumia mtandao wanaona hazina maana. Nyingi kati ya hizo huwa 'zinajificha' kwenye databases ambazo Google aidha hawako interested nazo au zimepigwa pini zisionekane. Taarifa nyingi ni za zamani sana na zimepitwa na wakati. Maudhui ya iPhone apps, mafaili ya kwenye Dropbox account yako, academic journals, rekodi za mahakama na kurasa binafsi za mitandao ya kijamii - vyote ni mifano ya data ambazo mara nyingi haziwi indexed na Google lakini zipo mtandaoni.

Search engines nyingi za deep web zimesitishwa au zimenunuliwa, kwa mfano Alltheweb, DeeperWeb, na CompletePlanet. Zipo chache zilizobaki ambazo zinaweza kukupa matokeo zaidi ya Google, Bing, au Yahoo ambazo ni : Dogpile, na The WWW Virtual Library

Lakini hizi ni general haziko specialized, na mara nyingi specialized search engines huwa ni bora zaidi ya general search engines katika kutafuta taarifa kwenye the deep web. Kama unatafuta nyaraka za mahakama, kwa mfano, tumia website ya nchi yako inayotunza taarifa za mahakama za nchi husika. Kama unatafuta academic journals, vivyo hivyo. The more specific you can be, the better, vinginevyo utajikuta unapata matokeo yale yale ambayo ungepata Google. Kama unahitaji faili fulani mahsusi, mfano Excel file au PDF, jifunze jinsi ya ku-specify unapotafuta mtandaoni.

KWA HIYO, VITU GANI HASA VINAPATIKANA DEEP WEB?
Deep web ina vitu ambavyo havionekani kwa search engines. Hapa chini ni mifano ya vitu ambavyo vimo kwenye deep web:
  • Taarifa zote kuhusu email yako.
  • Taarifa zote kuhusu akaunti zako za mitandao ya kijamii.
  • Taarifa zako za online banking accounts ulizonazo.
  • Data ambazo makampuni yanahifadhi kwenye private databases zao.
  • Data zilizomo kwenye databases za kisayansi na kitaaluma.
  • 'Medical records'
  • Nyaraka za kisheria.
Taarifa nyingi zilizomo deep web ni zile ambazo usingependa mtu aki-search mtandaoni azione - kwa mfano taarifa zako za benki - na ni kwasababu ni taarifa za siri na zikiingia mikononi mwa wakulungwa zinaweza kuleta kizaazaa. Wahuni 1:1 imeandikwa; Kama unaingia kwenye akaunti yako mojawapo kwa kuandika 'user name', 'password', au aina fulani ya 'authentication', basi taarifa unazozipata kwenye akaunti hiyo zinapatikana kwenye deep web. Majanga si eti? Hapana, usiogope. Deep web inaweza kulinda taarifa zako na kulinda faragha yako pia.

LAKINI JE, DEEP WEB NI SALAMA?
Well, unaweza kusema deep web ni salama hususani kama ukiilinganisha na dark web. Dark web ni sehemu ya deep web. Websites za Dark web mara nyingi zinahusiana na shughuli za kihalifu - lakini sio zote. Nitalielezea hilo baadae.

Kupata vitu vilivyomo kwenye deep web ni salama kwa kiwango fulani. Hebu fikiria. Ni mara ngapi unaingia kwenye email yako na kuangalia statements zako za benki online bila wasiwasi wowote. Lakini hiyo haimaanishi kuangalia aina hii ya taarifa binafsi mtandaoni sio hatari. Kwa mfano, akaunti zako zilizomo kwenye deep web zina taarifa nyingi binafsi ambazo wahalifu wanaweza kuwa wanazitaka. Na hiyo ndo sababu ni muhimu sana kutumia 'strong' na 'unique passwords' kwa akaunti zako zote. Kwa mfano kutumia combination ya herufi, tarakimu na alama ili iwe ngumu kwa mtu 'kukisia'.

Hatari nyingine ni hii hapa; Unaweza kufanya ujinga wa kuingia kwenye akaunti zako binafsi kwa kutumia 'Public Wi-Fi network' ambayo haiko protected. Kwa mfano, unaweza kulipa bili fulani online wakati unasubiri kupanda ndege kwa kutumia Wi-Fi ya Airport. Aisee, usirudie tena huo ujinga. Badala yake tumia 'Virtual Private Network' maarufu kama VPN — ambayo inaweza ku-encrypt data zako na kulinda usiri wako mtandaoni.

Hatari nyingine; Unaweza kupokea email ambayo inaonekana imetoka kwa yule ambaye unadhani ndiye kumbe sio, inaonekana salama lakini si salama. Kwa mfano, inaweza kuonekana imetoka benki, ambao wanatunza taarifa za akaunti zako deep web. Email hiyo inaweza kukuelekeza uandike namba yako ya kadi ya benki, au ubonyeze link fulani waliyokutumia na ufuate maelekezo. Braza, kuwa makini. Kama benki yako hawana utaratibu wa kuwatumia watu email na kuomba taarifa zao - kausha, usiwe na pupa. Kuna watu aina ya Hushpuppi wapo busy mtandaoni kwa tricks kama hizo. Hii inaitwa "phishing."

DARK WEB NDO WAPI?
Dark web ni stori nyingine - na pengine ndo ile uliyokuwa unaichukulia kama ndo deep web kutokana na jinsi ulivyosoma kwenye magazeti au kuangalia kwenye TV. Lakini kumbuka, DEEP WEB na DARK WEB ni vitu viwili tofauti. Ingawa watu huwa wanatumia majina haya mawili interchangeably, lakini moja — ambayo ni Deep web — ina data ambazo kwa sehemu kubwa ni 'harmless data' na 'digitized records'. Hii nyingine sasa — Dark web — ndo shida, imejizolea umaarufu duniani kwa shughuli za kihalifu.

Browsers za kawaida haziwezi kuingia kwenye dark web websites. Badala yake, Dark web inatumia kile kinachoitwa 'The Onion Router hidden service protocol'. Wengi wanaifahamu kama TOR - ni kifupi cha 'The Onion Router'. Servers za “Tor” zimefichwa na kwahiyo hazionekani kupitia search engines na zinamwezesha mtumiaji kuficha utambulisho wake wakati akiwa anaperuzi mtandao. Wakati huo huo, waandishi/wachapishaji (publishers) wa websites zilizopo dark web nao ni 'anonymous' vile vile - kwasababu 'Tor' ina 'special encryptions'.

Ukiingia dark web, unakua umeingia kwenye ulimwengu mwingine wa mtandao. Kila unachokutana nacho humo ni cha humo humo - hakitoki nje ya mtandao wa 'Tor network', ambayo inatoa ulinzi na usiri kwa kila mtumiaji kwa kiwango sawa.

Zingatia: Website za Dark web zinaishia na .onion badala ya vile ulivyozoea, yaani kwa mfano .com, .org, au .gov.

HUKO DARK WEB KUNA VITU GANI?
Dark web inafanya kazi kwa kiwango cha juu sana cha usiri (A high degree of anonymity). Inabeba shughuli na maudhui ya aina zote: yale yasiyo na madhara, na pia inabeba shughuli, huduma, bidhaa na maudhui ya kihalifu.

Kwa mfano, website moja ya dark web inaweza kuwa ina majibu ya vitendawili vyote vigumu duniani. Website nyingine ya dark web inaweza kuwa inasaidia kuboresha eBooks ziwe na mwonekano 'professional'. Pia website nyingine ya dark web inaweza kuwa ni 'forum' tu ya watu ambao wanaamini kuwa uhuru wa kujieleza (free speech) upo hatarini - kwahiyo wanazama gizani ili wawe huru kujadili mambo yao huko pasipo kuingia mikononi mwa vyombo vya usalama na udhibiti.

Lakini dark web inafahamika zaidi kwa maudhui machafu (dark content) - yaani, maudhui ya kihalifu na pengine yanayotisha. Hii hapa ni baadhi ya mifano ya content nyeusi unazoweza kuzikuta kwenye dark web:
  • Taarifa zilizoibiwa. Ukisikia kuna mahali watu wamefanya udukuzi, au kumetokea kile kinachoitwa 'data breach', kuna uwezekano mkubwa taarifa hizo zilizoibiwa - kuanzia 'Social Security numbers' mpaka 'bank card numbers' — zinaenda kuuzwa sokoni - kwenye dark web. Unaweza pia kununua vitu kama 'log-in credentials', 'hacked Netflix accounts', n.k.
  • Bidhaa haramu. Madawa haramu yote yanatembea dark web. Pia unaweza kupata sumu na kemikali za kila aina ambazo hutumiwa katika shughuli za mauaji/ uharibifu.
  • Vitu, huduma na maudhui ya kutisha. Things get ugly fast ukiwa dak web. Vitu kama umwagaji damu, wauaji wa kukodi, usafirishaji haramu wa binadamu, ngono za watoto, viungo vya binadamu, bidhaa feki, na silaha za aina zote - zote zinaweza kupatikana dark web.
Kwa kifupi, unaweza kununua CHOCHOTE ambacho akili yako inaweza kufikiria - hata vile ambavyo ni bora hata usifikirie.

JE, DARK WEB NI SALAMA?
Haha... ni swali la kijinga, right? Lakini hapana - dark web inaweza kuwa salama in some cases — fikiria kwa mfano, unapotafuta vitu halali vinavyopatikana huko kupitia dark web websites unazoziamini - na si vinginevyo.

SAFETY ISSUES ZA KUZINGATIA UNAPOINGIA GIZANI.
  • Shughuli za kihalifu. Ukiingia dark web upo uwezekano mkubwa utakutana na websites zinazoendeshwa na magenge ya kihalifu duniani. Sasa, licha ya kuwa wanauza bidhaa na huduma haramu, wanaweza pia kukutumia, kukudukua na kukuibia. Jiangalie bro!
  • Kuvunja sheria. Unaweza kukamatwa, kushtakiwa na kuhukumiwa kwa vitu unavyofanya dark web. Ni muhimu kuhakikisha huvunji sheria - serikali zina mikono mirefu, usijisahaulishe bro.
  • 'Links za kimagumashi'. Uki-click kwenye link yoyote, narudia tena... uki-click link yoyote kwenye dark web - upo uwezekano mkubwa kuwa umeshachukua vitu ambavyo huvihitaji. Uwezekano ni mkubwa pia kuwa, uki-click link yoyote iliyopo dark web au uki-download chochote unakuwa umefanikiwa kujizolea virusi vya kila rangi; so usishangae computer yako ikizima papo kwa papo na isiwake tena!!!
  • Wana usalama. Wazee wa usalama wamo pia dark web kwaajili ya kuwanasa wajuba wanaojihusisha na shughuli za kimagumashi. Na wao, kama walivyo wajuba wengine walioko dark web, ni watu wasiojulikana - wanafanya kazi pasipo wewe kuwatambua kuwa ni wana usalama. Ninachoweza kukwambia ni kwamba, utakaposhtuka utajikuta tayari upo jela na hujui umefikaje.
Vipi, bado unataka kuendelea na safari ya kuelekea gizani? Sawa, basi jitahidi uwe 'selective' ukifika huko, uwe mwangalifu wa aina ya website unazoingia. Mimi nakutakia kila la heri, urudi salama.

NAINGIAJE DARK WEB?
Kuingia dark web ni rahisi pia kuliko ulivyofikiri. Unachotakiwa kufanya ni ku-download dark web browser, mfano 'Tor browser'. Ukisha-download dark web browser yoyote, install. Ukisha-install, anza kutumia - inafanya kazi kama browser ya kawaida tu; andika URL unayoitaka - bofya enter na karibu dark web! Hata hivyo, ugumu upo kwenye kupata hicho unachokitafuta. Sio rahisi kama inavyokuwa unapotumia search engine za kawaida kama Google. Dark web haina 'index' au 'ranking system' ya kukusaidia kupata unachotaka.

Zipo dark web search engines. Moja inaitwa 'Uncensored Hidden Wiki' inatoa mwongozo unaoelekeza namna ya kupata vitu mbalimbali kwenye dark web. (Ikiwemo na miongozo ya namna ya kuingia kwenye websites haramu pia.)

NAJILINDAJE NINAPOTUMIA DEEP WEB NA DARK WEB?
Ukiingia deep web — hata kama unataka kuangalia kama pesa yako uliyotumiwa imeingia benki kwa njia ya mtandao - ni vizuri ukajidhatiti kwa software za ulinzi na uhakikishe zipo Up to date. Tumeshaongelea matumizi ya VPN kwenye public networks. Nakupa dondoo chache za kukusaidia uwe salama unapotumia Tor na dark web browsers zingine. Kuna mengi ya kuzingatia lakini hizi zikupe mwanga wa mema na mabaya.

Tor inafahamika kuwa inamfanya mtumiaje awe anonymous, kwa hiyo ni browser sahihi kwaajili ya ku-share taarifa nyeti/ za siri na watu wako wa karibu au kutoa taarifa fulani za uhalifu kwa serikali au vyombo vya ulinzi pasipo wewe mtoa taarifa kujulikana. Cha msingi hakikisha Tor na applications zake zote zipo updated. Pia hakikisha Operating system ya vifaa unavyotumia kuingia deep/ dark web ipo up to date pia.

Kamwe usitumie email ya kawaida kwenye websites unapotumia Tor. Ingawa Tor imeundwa kumficha mtumiaji, lakini kuweka email yako sio wazo zuri - kunaweza kuwafanya watu kukujua (It may expose your identity). Ile tu kwamba kuna wahalifu mtandaoni, itoshe kuwa ni kengele ya tahadhari kwako kuwa taarifa zako za siri zinaweza kuangukia mikononi mwao muda wowote. Kuingia dark web kunawaingiza watu wengi matatizoni. Tofauti na deep web, ambayo ina taarifa muhimu na zenye manufaa, dark web imejaa uhalifu wa kila namna.

Kwakuwa Tor servers zinamficha mtumiaji wa dark web, hakuna namna mamlaka zinaweza kuratibu/ kudhibiti shughuli, maudhui, bidhaa au huduma zilizomo dark web. Pia mamlaka haziwezi ku-trace mawasiliano au kufuatilia miamala ya malipo yanayofanyika dark web kwasababu malipo yanafanyika kwa Bitcoin, digital currency ambayo inafanya kazi independently pasipo kuratibiwa na benki kuu yoyote duniani.

Kwa upande mwingine, yapo machapisho na maudhui huko dark web ambayo yanawekwa na watu ambao wao wanaamini ndio namna pekee ya kupata na kuendeleza uhuru wa kweli wa habari (A truly free press). Kabla hujapotelea gizani, jifunze na uzifahamu hatari za dark web. Hakikisha una-install na kutumia strong security software kwenye computer yako na vifaa vyote ili kulinda privacy na usalama wa data zako.

Kutumia dark web ni hatari. Kuna vitu na watu ambao ni vizuri ukawaepuka ukiingia huko gizani.

Kwanza ni Viruses. Kuna websites zinaweza kuingiza viruses kwenye vifaa vyako, na kuna aina nyingi za viruses huko. Kamwe usi-download chochote ambacho huna uhakika nacho toka kwenye website ambayo huiamini.

Pili ni Hackers. Unaweza kuzikuta hacker forums kwenye dark web. Ukiingia humo unaweza kuwaajiri/ kuwa-kodi computer hackers kwaajili ya shughuli za kihalifu. Haishangazi, hizi njemba ulizoziajiri/ ulizo-zikodi zinaweza kabisa kukugeuka na kuku-hack wewe mwenyewe!!!

Tatu ni Webcam hijacking. Wadukuzi wanaweza kujaribu kupata 'remote administration tool' — maarufu kama “RAT” — kwenye vifaa vyako. Hii inawawezesha ku-hijack webcam yako — ikimaanisha kuwa, wanaweza kukuona au kuona kinachoendelea upande wako kwa kutumia camera za vifaa vyako. Kwahiyo, ni vizuri kama hutumii webcam yako basi ifunike na tape/ kipande cha karatasi.

Maudhui ya Dark web yanaweza kuwa haramu. Muda wowote ukiwa umeambatana na madawa haramu, maudhui haramu na uchafu mwingine wa namna hiyo, unaweza kujikuta mikononi mwa pilato. Kisingizio kuwa ulibonyeza kwa bahati mbaya au ulitaka tu kujua kuna nini - haitakusaidia sana mbele ya pilato. Kwa mfano, uki-share picha na video za Child pornography au ukinunua bidhaa/ huduma haramu, unaweza kujikuta mikononi mwa FBI/ CIA/ TISS/ Interpol n.k. Hapa chini ni baadhi ya mifano ya namna vyombo vya usalama vilivyofanikiwa kuingia na kufumua mitandao ya kihalifu dark web.

Silk Road. Hii ilikuwa ni 'online black market' iliyokuwa inauza illegal drugs. Ilianzishwa mwaka 2011. Mauzo yanakadiriwa kufika US$1.2 billion. Mmiliki wake anaeitwa Ross Ulbricht alishtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

AlphaBay. Hii nayo ilikuwa online black market nyingine, ilianzishwa mwaka 2014. Ilikua kubwa mara 10 ya size ya Silk Road baada ya Silk Road kufa. Bidhaa zilizokuwa zinauzwa humo zilikuwa ni za aina tofauti tofauti - kuanzia madawa mpaka data zilizoibiwa. Mwanzilishi wake Alexandre Cazes alikamatwa. Baadae alikutwa amekufa selo huko Thailand, inasemekana alijinyonga.

Hansa. Hii nayo ni online black market ambayo ilikua kwa haraka baada ya kufungwa kwa AlphaBay kwakuwa wauzaji waliokuwa wanatumia AlphaBay walihamia Hansa. Lakini polisi wa Netherlands (Dutch police) walikuwa tayari wamepenya na kuingia humo na wakapata taarifa zote za kiintelijensia walizohitaji kufanya kazi yao. Hansa ilifungwa mwaka 2017.

KWANINI DEEP WEB NA DARK WEB ZIPO?
Kwasababu zote zinamhakikishia mtumiaji vitu vikubwa viwili; high degree of privacy and anonymity.

Deep web inasaidia kulinda taarifa zako binafsi ambazo ungependa zibaki siri. Lakini kama ukiingia kwenye akaunti yako ya benki mtandaoni, taarifa za akaunti hizo sio siri tena. Unajua ni kwanini? Kwasababu benki itajua kuwa umeingia. Ndiposa, wahenga walisema - hakuna siri ya watu wawili - kama benki imejua, yoyote anaweza kujua. Dark web yenyewe inafanya kazi kwa kanuni kuu ya 'total anonymity'. Unachofanya dark web kinabaki kuwa siri yako wewe tu. Ukichukua tahadhari zote zinazotakiwa ukiwa dark web, hakuna namna ambayo unaweza kuwa tracked au ulichofanya kuwa traced mpaka kufika kwako.

Kwa baadhi ya watu, usiri/ faragha/ privacy ni muhimu sana mtandaoni. Wanaweza kuwa wanahitaji ku-control taarifa zao binafsi mtandaoni ambazo internet service providers na websites zinakusanya kuwahusu. Uhuru wa kujieleza pia ni issue, na baadhi ya watu ndicho wanachokifuata huko dark web au wanapotumia dark web browsers kama Tor. Anonymity inamwezesha mtu kutoa maoni yake, kwa mfano, ambayo wengi hawayapendi lakini sio haramu. Dark web inawasaidia sana watu wa namna hiyo.

**************
UPDATE:

MUONGOZO WA KUINGIA DARK WEB - HATUA KWA HATUA

Google inakupa sehemu tu ya yaliyomo kwenye mtandao. Inakadiriwa kuwa, web ina maudhui kiasi cha mara 500 zaidi ya yale unayoyaona kupitia Google. Yale unayoyaona uki-google yanafahamika kama “surface web,” kwa hiyo mengine yote, yasiyoonekana kupitia search engine za kawaida huitwa “deep web” au “invisible web”.

Dark net, au dark web, ni sehemu ndogo sana ya deep web. Kuna mtu hajasoma vizuri hapo, narudia tena - Dark web ni sehemu ndogo sana ya deep web. Dark web inajumuisha websites na huduma ambazo zimefichwa kwa makusudi na wamiliki wake. Wote, wamiliki na watumiaji wa dark net huwa hawafahamiki. Ingawa si kila kitu katika dark net ni haramu, lakini ndiko zinakopatikana 'black markets' nyingi sana, 'hacker forums(Forums za wadukuzi)', 'malware vendors'(Wauzaji wa virusi), na shughuli haramu nyinginezo.

DARK WEB NI KITU GANI HASA?

Dark web, au dark net, ni sehemu ndogo ya deep web ambayo imefichwa kwa makusudi. Websites na data zinazopatikana kwenye dark net zinahitaji 'tool' maalum kuweza kuzifikia.

Websites nyingi zilizoko dark web ni masoko ambako bidhaa na huduma haramu kama vile madawa ya kulevya, silaha za moto na taarifa za kadi za benki za watu zilizoibiwa huuzwa humo. Zipo sehemu za ndani zaidi katika dark net (darkest corners) ambazo huko ndiko watu huenda kuajiri/ kukodi wauaji, kujihusisha na usafirishaji wa binadamu na kubadilishana picha na video za ngono zinazohusisha watoto.

Zaidi ya hayo, dark net ina maudhui na data ambazo zinaweza kupatikana kwa faragha. Inaweza kuwa ni blog, forum, chat room au private gaming server. Uzuri wa dark net ni 'anonymity'. Hakuna anaemtambua mwenzake humo ndani, endapo kila mmoja amechukua tahadhari zinazotakiwa. Taarifa za watumiaji wa dark web haziwezi kuingia mikononi mwa serikali wala makampuni yanayokusanya taarifa za watu.

Mara nyingi dark web na Tor hutumiwa na waandishi wa habari na 'whistleblowers' kubadilishana nyaraka/taarifa nyeti (sensitive information), akiwemo mzee Edward Snowden mwenyewe.

JINSI YA KUINGIA DARK NET.

Kuingia katika sehemu kubwa ya dark net unahitaji Tor. Nimeshaelezea huko nyuma Tor ni kitu gani. Njia rahisi ya kuipata Tor ni kwa kutumia Tor Browser. Angalia usichanganye madesa - Tor na Tor Browser ni vitu viwili tofauti. Tor Browser inapatikana bure kabisa, itafute kupitia Google.

Kama unajali sana usiri na usalama wako ni vizuri ukaanza kutumia VPN tangu hatua ya kwanza na pia unapotafuta vitu kupitia Google ni vizuri ukatumia private/incognito mode iliyomo kwenye browser yako. Imetengenezwa juu ya msingi wa Firefox, Tor Browser inakuwezesha kuingia mtandaoni kawaida na kwenye dark web. Hakikisha una-download Tor Browser kutoka kwenye website official ya Tor ili uwe salama.

Ulinzi wa ziada: Tumia VPN

Internet providers na websites zinaweza ku-detect pale ambapo Tor inatumika kwasababu 'Tor node IPs' ziko public. Ingawa websites haziwezi kuku-identify na wala ISPs hawawezi ku-decrypt internet traffic yako, wote wanaweza kuona kuwa Tor ipo inatumika. Hii inaweza ikazua maswali na kusababisha waanze kuchunguza. Kama unataka kutumia Tor kisiri, unaweza ukatumia aidha VPN au Tor Bridges (Tor nodes ambazo haziko publicly indexed). Unapotumia VPN, ISP wako hawezi kuona kama upo connected kwenye Tor node, ataona tu ile encrypted tunnel ya kwenye VPN server.

MISELE NDANI YA DARK NET

Sasa kwa kuwa tayari una Tor, unaweza kuingia dark web. Dark net websites zinaitwa “Tor hidden services”, na unaweza kuzitofautisha na wensites za kawaida kwa kutumia URLs zake. Badala ya ".com" au ".org", websites za dark net zinatumia the top-level domain, “.onion“.

Bila shaka, kuzipata hizi websites za .onion ni mtihani wa kwanza, kwasababu hazionekani kwenye Google search results. Huko nyuma nimeelezea kuhusu Silk Road, sasa huwezi kuandika tu "Silk Road" halafu ukategemea itakupeleka dark web... no no no. Unahitaji search engines zenye uwezo wa kufanya kazi kwenye Dark web

Nakupa majina ya search engines chache ambazo zinaweza ku-index websites za .onion: Kuna NotEvil, Ahmia, Candle, na Torch. Pia kuna directories kama dark.fail. Usisahau - kuwa makini sana unapotumia onion URLs ambazo ziko public. Jiridhishe kutoka vyanzo mbalimbali upate uhakika wa URL unayoingia kabla hujaamua kuingia.

Dark web haikosi matapeli, phishing sites, na malware zilizokuwa designed kuwa-trick newbies. Links zinazokuwa posted kwenye clear web mara nyingi huwa ni mtego. Na kwasababu kuna matumizi kidogo sana ya HTTPS kwenye dark net, kuthibitisha kama website ni genuine au la kwa kutumia SSL certificate haina maana.

Reddit ni resource muhimu pia kwaajili ya kuitafuta website ya dark net au deep web unayoitaka. Jaribu kuingia /r/deepweb, /r/onions, na /r/Tor subreddits.

Anonymity iko mikononi mwako.

Sasa unaweza ku-browse dark web sites na hidden wikis, lakini kama umepanga kufanya chochote zaidi ya hapa, utahitaji kuchukua tahadhari zaidi. Kama umepanga kufanya manunuzi kwenye masoko yaliyomo dark net kama vile Silk Road ili kupata dawa ambazo mamaako mzazi anazihitaji ili aendelee kuwa hai, kwa mfano, utahitaji kutengeneza fake identity. Utatakiwa kufungua encrypted email yenye email address mpya, utatakiwa ku-encrypt meseji zako kwa PGP, utatakiwa kutumia jina bandia (A pseudonym), utatakiwa kuwa na anonymous bitcoin wallet, utatakiwa ku-disable Javascript kwenye Tor Browser, utatakiwa kufanya utafiti wa wauzaji wa hiyo dawa, na kadhalika.

Narudia tena, ni vigumu kuelezea vya kutosha juu ya namna usalama na usiri ilivyo muhimu kwenye dark net. ISP wako na serikali wanaweza wasione unachofanya kwenye Tor Network, lakini wanaweza kujua kuwa upo kwenye Tor Network, na hiyo peke yake inatosha kuwafanya wakutolee mimacho. Hivi kwani, ukiona mtu ameenda kununua rizla dukani - wazo gani la kwanza linakujia kichwani? Basi ndivyo serikali itakavyokufikiria ikigundua upo kwenye Tor. Mahakama moja mjini Marekani ilitoa hukumu inayoonesha kuwa kutumia Tor ni kigezo tosha cha kuwawezesha wana usalama kufanya msako na kukamata computer yoyote iliyotumika kwenye Tor - popote duniani.

Tahadhari nyingine muhimu ni kuhakikisha kwamba URLs zako za .onion ziko sahihi. Usikosee hata herufi moja - kwasababu URLs za Onion zina maandishi na namba ambazo ziko shaghala baghala. Ukipata URL ambayo una uhakika nayo, ihifadhi katika encrypted note - kwasababu Tor browser haitakutunzia kumbukumbu kwaajili ya baadae. Vinginevyo ni rahisi kujikuta umeingia choo cha jeshi.

Zingatia: Unapoingia dark web utahitaji kutumia Tor na VPN - vyote vinachangia sana kupunguza spidi ya mtandao. Kwahiyo tafadhali, kuwa mvumilivu.

Ni matumaini yangu umepata kitu katika uzi huu. Mic drop... paah!
#Virus
Faida na hasara zote zangu mwaka huu wa 22
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom