Fahamu namna ya kuingia deep web & dark web

Ndio, Virus inaweza kusababisha physical damage. Umewahi kusikia habari ya kirusi kinachoitwa Stuxnet?. Stuxnet iliharibu mitambo ya nyuklia ya Iran mwaka 2010. Inasemekana pia ilikwamisha urukaji wa roketi moja ya India. Juzi juzi ikasemekana virus ndo ilikuwa sababu ya kushindwa kwa jaribio la roketi la Korea Kaskazini.

Ndo maana zinaitwa ÇYBER WEAPONS. Zinaweza hata 'kuua' kwa namna tofauti tofauti. Kwa mfano; Virus kama Stuxnet inachohitaji ni kujua target, kujua hardware na software za target, na kisha shambulizi linatokea kupitia PLCs (Programmable Logic Controllers). Binafsi naamini pia Virus inaweza kuwa AI (Artificial Intelligence), inayoweza kuji-adapt na kuweza kupenya yenyewe kwenye mifumo tofauti tofauti, ku-access na ku-overwrite PLCs - hatimae..... booooom!!: aina hii ya Virus mara nyingi inatumia kile kinachoitwa 'Zero Day Exploits'

Kwahiyo, ndio virus inaweza kuunguza PC ikiwa imeagizwa kufanya hivyo. Ingawa kwa zama hizi, hackers hawapendi kutumia aina hii ya virus. Hapa chini ni baadhi ya vitu ambavyo virus inaweza kufanya kwenye PC yako na hivyo kupelekea physical damage;
  • Hard drive trashing - Inai-peleka spidi HDD - mfululizo mpaka inakufa.
  • Over voltage - Kwa teknolojia ya 'software based Overclocking', ni rahisi kuongeza voltage kwa kiwango ambacho kinaharibu RAM au CPU. Motherboards huwa zinapunguza voltage ili RAM na CPU ziweze kufanya kazi vizuri. Boards za kisasa zinatengenezwa kwa namna ambayo 'overclocking' inaweza kuwa manipulated kupitia OS. Umeme wa kiwango cha 2.3 volts unatosha kuunguza RAM za DDR2 na umeme wa kiwango cha 2 volts unatosha kuunguza DDR3. Vivyo hivyo, CPU zinaweza kuungua kwa njia hiyo hiyo. Naamini hata Video cards zinaweza kukaangwa pia.
  • Fan speed manipulation - Virus inaweza kuisimamisha au kuipunguza kasi feni ya PC yako mpaka ina-overheat. Ili kuikaanga PC yako vizuri, virus pia ina-disable program zilizowekwa kwenye PC yako kwaajili ya kuzuia 'temperature failure'. Sijasikia kama inawezekana kuiongeza kazi feni. Lakini virus inaweza kuruhusu voltage kubwa zaidi ya uwezo PSU (Power Supply Unit) iingie kwenye PC yako... na hivyo kuilazimisha feni kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kupooza matukio. Japo ni nadra kutokea.
  • Overloading PSU - PSU ikizidishiwa mzigo, inachemka sana... kinachotokea? vifaa ndani vinaungua au vinafeli, hasa hasa capacitors.
  • Motherboard BIOS: Unaweza ku-flash PC si ndio? Sasa virus inaweza kukusaidia ku-flash PC yako. Shida ni kwamba, virus inaweza kuflash BIOS na kulazimisha feni isimame/ isifanye kazi. Feni ikizima, process ya ku-flash inakwamia katikati, bios inabaki kuwa half flashed au inakuwa kuwa katika corrupted state, wenyewe tunasema inakufa mpaka umpate fundi wa kuifufua.
Kwa kifupi, kuna namna kadhaa za kukaanga vifaa vya kielektroniki. Unaweza kuvipika kwa kutumia joto kali, kuunguza kwa umeme, kuvichakaza haraka kwa kuvifanyisha kazi kuzidi uwezo wake au kuvigonga gonga mpaka vife.

View attachment 1515293
Duuh nayajua leo haya asee. Ubarikiwe kiongozi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom