IJUE SHERIA
Member
- Dec 11, 2017
- 11
- 146
FAHAMU NAMNA YA KUFUNGUA MIRATHI.
Na Mwanasheria Wetu.
1.MIRATHI NI NINI.
Mirathi ni mali ya marehemu aliyoiacha kwa ajili ya kurithisha warithi wake halali. Hakuna mirathi kabla ya kifo cha mtu.
Ni lazima mtu afe ndipo ipatikane mirathi. Na mirathi kwa ujumla wake huhusisha mali alizoacha marehemu.
2. NINI LENGO LA UTARATIBU WA MIRATHI.
Lengo kuu la kuwepo utaratibu maalum wa mirathi ni kukusanya, kuangalia, kusimamia, na kugawa mali alizoacha marehemu. Kulipa madeni aliyoacha marehemu na kujua madeni hayo yalipo nalo ni lengo la kuanzishwa utaratibu huu wa mirathi.
Lakini jingine katika hili ni kusimamia shughuli za mazishi ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo ya marehemu kuhusu namna na wapi azikwe. Hizi zote ni shughuli zilizopelekea kuanzishwa utaratibu wa mirathi.
Kama utaratibu huu usingewekwa na sheria basi ingekuwa rahisi mali za marehemu kupotea hovyo,kuharibiwa, kutumiwa vibaya na kuhujumiwa.
Lakini ingekuwa rahisi kwa wale wote wanaomdai marehemu kupoteza haki zao za madai baada ya kufa. Lakini kwa utaratibu maalum wa mirathi hawa nao hawawezi kupoteza haki zao.
3. NI SHERIA ZIPI HUTUMIKA KATIKA MIRATHI.
Hapa Tanzania zipo sheria tofauti tatu zinazotumika katika mirathi. Ipo sheria ya serikali"The Indian Succession Act 1865", zipo sheria za kimila"The Customary Law Declaration Order 1963" na zipo sheria za dini ya kiislamu"The Qur an & Sunnah". Makala ya leo hayataingia ndani zaidi kueleza sheria hizi. Kwa leo itoshe kujua tu kuwa sheria zinazotumika kwa hapa kwetu ni hizo tatu.
4. NAMNA YA KUFUNGUA MIRATHI.
( a ) Hatua ya kwanza kabisa pale tu mtu anapokufa hakikisha hazipiti siku thelathini kabla ya kupata cheti cha kifo.
Makao makuu ya wilaya ndipo vinapopatikana hivi vyeti. Na wilaya inayotumika ni ile wiaya alikofia marehemu. Cheti hiki ni lazima katika shughuli za mirathi.
( b ) Hatua ya pili ni kufanya kikao cha familia na kumteua msimamizi wa mirathi. Wanafamilia watakaa watajadili na kwa pamoja watampata msimamizi wa mirathi.
Mnapokaa kikao cha familia hakikisha zile ajenda zote mlizojadili zinawekwa katika maandishi. Na ni katika kikao hicho ambapo utatakiwa kuandaliwa mukhtasari.
Mukhtasari utaeleza ajenda za kikao, waliohudhuria, aliyeteuliwa kusimamia mirathi, hutaja warithi na mengine mengi. Mukhtasari hutakiwa kuandikwa kwa mkono na sio kuchapwa. Na kila aliyehudhuria atasaini.
( c ) Hatua ya tatu ni kupata barua kutoka serikali za mitaa. Ukisema nataka barua ya kufungua mirathi basi serikali za mitaa wanajua ni barua ya aina gani upewe.
( d ) Hatua ya nne ni kwenda mahakamani ili kuthibitishwa kuwa msimamizi wa mirathi. Hapa utatakiwa kwenda na cheti cha kifo, barua ya serikali za mitaa, mukhtasari wa kikao cha familia, na picha mbili za pasipoti.
Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa ikiwa marehemu aliacha wosia na katika wosia huo msimamizi wa mirathi ametajwa basi hakutakuwa na haja ya kukaaa kikao cha familia kumteua msimamizi wa mirathi.
Hii ina maana hata mtakapokwenda mahakamani ili kumthibitisha huyo msimamizi wa mirathi basi badala ya kuambatanisha mukhtasari mtaambatanisha wosia.
Mahakamani ndiyo hatua ya mwisho. Kwahiyo baada ya taratibu za kimahakama ikiwamo ile ya kutoa tangazo kwa mwenye kupinga kumalizika, basi msimamizi atapitishwa na atapewa fomu maalum ya usimamizi mirathi.
TOA MAONI, NA PENDEKEZA MADA AMBAYO UNGEPENDA IJADILIWE HAPA 0784482959.