Fahamu namna timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali mashindano ya klabu bingwa Afrika zinavyopatikana

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,286
3,018
Kuna kundi kubwa la watu wamekuwa wamekariri tu kuwa msimu fulsni timu nane hazitoanzia hatua ya awali lakini hajui hata ni vipi inapatikana na pia hajui kama idadi aliyotaja inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.

Sasa uzi huu faida kwa member anayeongoza kwa nyuzi za udaku, uongo na fitna na pia na wachambuzi na wana michezo mbalimbali wasiojua ni kwanini kuna timu zinatokea hazianzii hatua ya awali.

Shirikisho la soka barani Africa (CAF) ina jumla ya wanachama 54, na katika hao kuna wanachama 12 ambao wanapaswa kuingiza timu mbili mbili katika mashindano ya klabu bingwa, na wanachama 42 waliobaki wao wanaingiza timu moja moja tu klabu bingwa.

Katika mashindano ya klabu bingwa timu zinapaswa kutoana ili zibakie timu 32 ambazo zitacheza mtoano ili zipatikane timu 16 za kucheza hatua ya makundi.

Kutoanza kwa baadhi ya timu katika hatua ya awali ni kutokana na wanachama wengine kutoshiriki michuano ya klabu bingwa kutokana na sababu zao mbalimbali ikiwemo uchumi, na miindo mbinu yao hivyo kutokuwasilisha timu zao kucheza michuano hiyo.
Laiti kama ikitokea kuwa wanachama 52 wameamua kushiriki michuano ya ngazi ya vilabu, itafanya kuwe na idadi ya timu zifuatazo;
Association 12 timu mbili mbili = timu 24
Association 40 timu moja moja = timu 40
Hivyo jumla itakuwa ni timu 64 zitakazoshiriki klabu bingwa
Kwa mazingira ya namna hiyo ikitokea, hakutakuwa na timu yoyote amvayo haitoanzia hatua ya awali. Timu zote zitapaswa kucheza kwanzia hatua ya awali, kisha zitatoana na kubakia timu 32 ambazo zitacheza hatua inayofuata.

Naomba nije kumjibu GENTAMYCIME hoja yake ya kwamba Simba na timu zingine saba hazitaanzia hatua ya awali.

Cha kwanza ieleweke kuwa kuelekea msimu wa 2023/2024 zitachukuliwa performance ya misimu mitano ambayo itaanzia msimu wa 2018/2019 mpaka msimu wa 2022/2023 ambapo Simba inashika nafasi ya 9, je ili Simba isianzie hatua ya awali msimu ujao ni mazingira yapi yatokee?

Ni endapo itatokea timu 57 pekee zinazoshiriki michuano ya klabu bingwa msimu wa 2023/2024 badala ya timu 64, kwa maana ya wanachama 45 pekee ndio walioshiriki michuano ya CAF ngazi ya vilabu kati ya wanachama 54.

Kutokana na mazingira ya hapo juu, endapo wanachama ataongezeka kutoka kwenye hiyo idadi ya 45 ndivyo na idadi ya timu ambazo hazitoanzia hatua ya awali zitapungua. Na endapo idadi ya wanachama kutoka 45 watazidi kupungua, itasababisha idadi ya timu zisizoanzia hatua ya awali kuongezeka.

Mwisho nahitimisha kuwa hakuna msimamo au guarantee ya kuanzia hatua ipi katika michuano ya klabu bingwa mpaka ijulikane wanachama wangapi watashiriki michuano ya klabu bingwa msimu husika.
 
358132229_18226265845226150_1278681305450744382_n.jpg
 
Kuna kundi kubwa la watu wamekuwa wamekariri tu kuwa msimu fulsni timu nane hazitoanzia hatua ya awali lakini hajui hata ni vipi inapatikana na pia hajui kama idadi aliyotaja inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.

Sasa uzi huu faida kwa member anayeongoza kwa nyuzi za udaku, uongo na fitna na pia na wachambuzi na wana michezo mbalimbali wasiojua ni kwanini kuna timu zinatokea hazianzii hatua ya awali.
uarantee ya kuanzia hatua ipi katika michuano ya klabu bingwa mpaka ijulikane wanachama wangapi watashiriki michuano ya klabu bingwa msimu husika.
Ni watu wachache sana wataelewa hiki ulichoandika. Binafsi nimekuelewa.
 
Kuna kundi kubwa la watu wamekuwa wamekariri tu kuwa msimu fulsni timu nane hazitoanzia hatua ya awali lakini hajui hata ni vipi inapatikana na pia hajui kama idadi aliyotaja inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.

Sasa uzi huu faida kwa member anayeongoza kwa nyuzi za udaku, uongo na fitna na pia na wachambuzi na wana
Upuuzi mtupu
 
kifupi ushiriki wa simba kwa kuto kuanzia hatua ya mtoano itatokana na idadi ya timu zitakazothibitisha kishiriki mashindano, timu zikiwa nyingi na idadi ya timu zinazotakiwa kuingia direct kwene makundi zinapungua.
sio ubora wa timu ndio una determine kuingia direct makundi, bali idadi ya timu shiriki ndio inapelekea timu kucheza playoff
 
Simba ni nafasi ya 7. Kama hujui takwimu acha kuandika magazeti uchwara
Njoo na link inayoonesha msimu huu Simba inashika nafasi ya saba, mnaishi kwa kusikiliza watu pasipo kufatilia mambo. Hiyo nafasi ya saba ni assumption tu ya msimu wa 2024/2025 ambapo matokeo ya msimu wa 2023/2024 bado haijulikani timu zitavuna kipi. Angalia msimo wa msimu huu VS msimamo wa assumption ya msimu kwaajili ya mashindano ya msimu miwili mbele ( 2024/2025) kwenye attachment.
IMG_20230713_065711.jpg
IMG_20230713_065607.jpg
 
kifupi ushiriki wa simba kwa kuto kuanzia hatua ya mtoano itatokana na idadi ya timu zitakazothibitisha kishiriki mashindano, timu zikiwa nyingi na idadi ya timu zinazotakiwa kuingia direct kwene makundi zinapungua.
sio ubora wa timu ndio una determine kuingia direct makundi, bali idadi ya timu shiriki ndio inapelekea timu kucheza playoff
Wewe ni mmoja ya watu wenye kuelewa
 
Gazeti loote unahangaika tu kusikia Simba hawatoanzia hatua ya awali na ni nambari 7 kwa ubora Africa.
Ushauri wangu ni utulie tu sindano ikuingie unavyohangaika inaweza vunjikia ndani..
Natoa somo kwa wajinga na wapumbavu wasiojua kitu. Vipi nawewe ni miongoni mwa hao waliopo kwenye kundi la wasiojua rank na namna inavyotokea hadi timu isianzie hatua ya awali? Mipira mnajifunzia kwa wachambuzi badala ya kuufatilia mpira.
 
Malalamiko Fc naiona inarudi Kwa Kasi sana..!

Mzungu pori alishauri kuhusu kulalama lalama,Lakini hamsikiiii..! Kila siku lawama.
 
Back
Top Bottom