Fahamu mambo ya kuzingatia unapotaka kununua boti ndogo kwa ajili ya utalii/uvuvi/matumizi binafsi

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,952
12,526
1578980562690.png

Mambo ya kuzingatia pale unapotaka ununue boti ndogo kwa ajili ya utalii, uvuvi au matumizi binafsi.

1. Material yaliyotumika kutengenezea boti
- Mbao
Mbao imekuwa ikitumika kuunda boti tangu miaka ya nyuma. Faida zake ni kuwa na gharama nafuu na hasara ina wahi kuharibika ukilinganisha na chuma au aluminium.

- Fiberglass
Boti nyingi za kisasa zimetengenezwa kwa material ya fiberglass ili kuzifanya kuwa nyepesi na kupata speed nzuri na utumiaji mzuri wa mafuta. Hasara yake ni gharama na ni ngumu kufanya repair.

- Aluminum
Hii imetumika kutengeneza boti ndogo na kufanya boti kuwa nyepesi pia haipati kutu. Hasara zake ni bei kubwa sana na marekebisho yake ni gharama.

- Chuma
Chuma kinaaminika kwa ubora na kukaa muda mrefu zaidi kwa matumizi. Hasara ni kuingiliwa na kutu na gharama kufanya marekebisho.

2. Engine
Kwenye boti ndogo tunaweka engine kutokana na mahala ilipokaa na mapigo ya engine.

- Mahala engine itapokaa
Kuna boti zenye engine ndani(inboard engine) na boti zenye engine nje (outboard engine).

- Mapigo ya engine au mfumo
Hapa kuna 2 stroke engine na 4 stroke engine.

Angalizo. Tanzania asilimia kubwa ya engine za boti ndogo ni 2 stroke sababu ni urahisi wa ufundi wake.

3. Urefu au Saizi ya Boti
Boti zipo za saizi mbalimbali, urefu wa boti unatumika katika usajili wa boti. Kadiri boti inapokuwa ndefu na gharama za usajili kwa mita huongezeka. Saizi ya boti kubeba abiria kadiri ya hitaji yako ni kitu muhimu kujua ni idadi gani unataka watu wabebwe kwenye boti.

Angalizo: Shirika la uwakala wa meli wana shughulika na usajili wa boti kuanzia mita 4 na kuendelea, kwa kutoa leseni na cheti cha ubora wa chombo (Sea worthness certificate)

4. Visaidizi vya uongozaji wa boti
Hapa utachagua boti yako iwe na kisaidizi kipi katika kukuongoza safarini. Kuna Gps, Boat tracker, Compass

5. Mfumo wa kuwasha engine ya boti
Boti utachagua iwe ya kuwasha kwa kuvuta kick (manually start), kutumia fungua (Key ignition) au Remote.

6. Aina ya nishati utayotumia
Hapa utachagua engine yenye kutumia nishati uitakayo na ya bei nafuu kwako.
Mafuta kuna engine za diesel na petrol.
Kuna engine za umeme hizi nyingi huwa chini ya 10Horsepower.
Sasa kuna mpaka engine za nishati ya gesi.

7. Mfumo wa kusukuma boti (Propulsion System)
Unaweza ukachagua boti ya kutumia propeller za kawaida au pangaboi ambao ni rahisi na wa muda mrefu.

Jet system au mfumo wa kuvuta na kutupa maji nje kwa pampu. Jet system hii ina faida ya kuwa na speed kubwa na ni mfumo wa kisasa ambao unastarehesha chombo kwa kuondoa mitikiso. Hasara yake ni gharama, unataka matunzo na unaendeshwa na chombo kikiwa kwenye mzunguko mkubwa.

8. Mfumo wa usukani (Steering System)
Utachagua boti yako uendeshe kwa usukani kama wa gari (Wheelie) ambao huwekwa katikati ya boti.

Mfumo wa Joystick (kijifimbo kidogo kama batani) Hii utumika kukata kona kulia au kushoto kwa kupeleka uelekeo unaotaka.

Mfumo wa kawaida wa kushika ekseleta na usukani ulio unganishwa kwenye engine ya boti.

Vitu vingine ni kuangalia mwaka wa boti kutengenezwa, Mtengenezaji, Matoleo na Muundo.
Kama kuna vingine wadau wataongezea zaidi.

"SEA NEVER DRY"
 
Ungetupatia na bei zake kama zipo hapa bongo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unataka boti mpya ni bora umfate Songoro Marine and Boat Yard au Eristic Tanzania uwape vigezo unavyotaka wakutengenezee fiber boat ambayo itakuwa na engine yake. Kwa fiber boat ndogo bei inaweza kuanzia million 9.


Pia unaweza ukanunua nje na kuiagiza hapa nchini, kwa South Africa huwa naona kuna bei nafuu kwenye Gumtree. Tatizo kwenye makadirio ya kodi sijajua TRA wanakadiria vipi sije wakaweka boti kama kitu cha anasa, maana kuingiza kifaa cha uvuvi kuna msamaha wa kodi kama kwenye trekta.
 
Back
Top Bottom