Fahamu mambo 11 ambayo huyajui kuhusu samaki

1) Samaki hupata huzuni/msongo wa mawazo (depression) kama apatavyo binadamu

2) Kuna Samaki wanaishi zaidi ya miaka 70 ila yupo aliyeishi miaka 112 anaitwa Bigmouth buffalo

3) Kibaolojia kuna makundi (species) 30,000 ya samaki yanayotambulika

4) Kihistoria Samaki ameanza kuwepo duniani miaka milioni 500 iliyopita

5) Samaki halii (crying) kwahiyo ule msemo wa machozi ya samaki kwenda na maji ni fasihi tu ndio imetumika

6) Samaki huwa analala... Japo sio kama binadamu lakini samaki pia huwa analala... Ulalaji wa samaki huwa ni kupunguza mizunguko yake, hupunguza uwezo wa kuhisi jambo, hupunguza metabolism... Na kwa wakati huu ndio rahisi kuwavua kwa nyavu kwan huwa Hawana ujanja ujanja

7) Unajua kuwa kuna Samaki wanabadilisha jinsia kutoka kuwa wa kiume kwenda kuwa wa kike au kike kwenda kuwa wakiume kwa kitaalumu huitwa Sequential hermaphroditism.... Mara nyingi sababu ya kubadilisha huko kwa jinsia hutokana na mazingira

8) Je unajua kuwa baadhi ya lipstick na rangi za kucha zinatokana na magamba ya samaki NA PIA shahawa/manii ya samaki aina ya nyangumi pia hutumika kutengenezea shampoo, lipstick na baadhi ya vipodozi

9) Bunju/ fugu ni miongoni mwa samaki watamu sana ila ni samaki wenye sumu kali sana inayoweza Kukuua muda mchache...Nchini Japan ili upewe idhini ya kumpika samaki huyu unatakiwa uwe na cheti maalum cha kusomea.... Lakin kwa Tanzania anapikwa tu japo sio na kila mtu ila supu yake ina balaa

10) Binadamu anaweza kujua ladha 7,000 lakini kambare anauwezo wa kujua ladha 27,000

11) Horse fish ni kama kinyonga tu kwa sababu wanafanana kwa baadhi ya mambo mfano... Mwendo wao kinyonga na horse fish wote hutembea taratibu, kinyonga na horse fish wote wanauwezo wa kujibadilisha rangi kuendana na mazingira, kinyonga na horse fish wote wanauwezo wa kuona mbele na nyuma wakati wa kutembea...... Mkunga nae ni kama nyoka kwa ufanano wao mfano umbo lao, maisha yao, na pia sumu zao

View attachment 1886696
haha
 
Kwenye huu uzi nimeona watu wengi wapo misinformed. Kusema kambale sio samaki ni chura nimeshangaa sana.

Tusipende kusikiliza myths na kuzisambaza kama vile ni fact. Yani unapigiwa story kijiweni na wewe bila kufuatilia unachukua kuwa ndio ukweli.
 
Samaki gani ana mustachi?
 
Samaki gani ana mustachi?
Chura ana mustachi? Je unajua hizo barbels/whiskers ni za kazi gani? Na je unajua kuna species nyingi tu kuacha kambale ambazo zina barbels/whiskers mfano catfish n.k

Je unajua kuwa species mbalimbali za mimea na wanyama hu adapt na ku evolve tofauti kutokana na mazingira wanayoishi?

Kama nyangumi ni samaki mbona anazaa na kunyonyesha tofauti na samaki wengine?

Je unajua kuwa hata papa wako tofauti mfano kwenye mfumo wa reproduction kuna wanaotaga mayai nje (oviparity) kuna wanaozaa (vivipariry) na kuna wanaorutubisha mayai yao na kutotolesha yakiwa ndani ya tumbo/oviduct (ovoviviparty).

Mkuu mjue tu kuwa kuna factors nyingi zinazotumika ku classify hivyo viumbe mpaka vikawekwa kundi moja la samaki hata kama kuna baadhi ya tabia na features vinatofautiana.

Sio kwasababu kambale ana barbels na sato hana basi una conclude kuwa kambale sio samaki.
 
Najua kila ulichouliza kama najua.

Kambale anapatikana kwenye hiyo familia ya catfish.

Haujawahi kuona chura ana mustachi?

Yaani kwa kifupi kambale na beberu tofauti yao ni kambale anaishi mpaka miaka 60 na anaweza kukua kumfikia Hashim Thabit.
 
Kambalae siyo samaki ni chura.

Katika wale ndubwi atakayeota miguu anakua chura atakayekosa miguu anaevolve na kua kambale.

Samaki huhitaji maji kuishi ila kambale waweza mtoa kwenye maji ukamuacha kwenye beseni kwa saa mbili na ukamkuta yupo hai.

Akijifukia kwenye tope ndiyo utamsahau ila siku ukifukua tope unamkuta.

Si ndo tuanze kula vyura sasa
Kwahiyo sisi tunaokula kambale tunakula chura
 
Back
Top Bottom