Fahamu mambo 10 kuhusu 'El Chapo' the drug lord

Fahamu mambo 10 kuhusu 'El Chapo' the drug lord

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,624
Reaction score
931
1437036260183.jpg

Joaquin Guzman Loera a.k.a El Chapo mzaliwa wa mexico na mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya anayetafutwa na Marekani na Mexico kwa udi na uvumba, leo nimeamua kushare na nyinyi wana JamiiForums kuhusu mafia huyu wakimeki Mexico.

1.Forbes walishawahi kumuweka kwenye listi ya watu wenye pesa nyingi Duniani mwaka 2009.

2.Ni miongoni mwa watu wenye nguvu na ushawishi Duniani akikamata nafasi ya 67.

3.Alipewa jina la Osama bin Laden wa Biashara ya Madawa ya Kulevya.

4.Ametoka kwenye familia masikini na amesoma mpaka darasa la 3, akaanza kuuza bangi na baba yake mzazi akiwa na umri wa miaka 15 akamjenga nyumba mama yake.

5.Amekaa gerezani kuanzia mwaka 1983 mpaka 2001 chini ya ulinzi mkali wa wanajeshi na usalama, lakini alitoroka baada ya kuonga dola 2.5m, alipitia kwenye toroli la kukusanyia nguo chafu gerezani.

6.Selo yake ilikuwa tofauti na zingine alipata kila kitu alichokuwa anataka zikiwemo cocaine na malaya na alibadili selo kuwa kama hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

7.Alipewa jina la "public enemy No 1"nchini Marekani na harususiwi kukanyaga nchini humo.

8.Ana wake wa 4 na watoto 10 lakini wote wanafanya biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

9.Alikuwa akiingia kwenye migahawa au kasino, bar hakuna mtu ataruhusiwa kutoka mpaka yeye amalize kilichompeleka pale na bili zote watu walizo tumia analipa yeye.

10.Ana ulinzi wa zaidi ya Rais wa Marekani na kwenye mizunguko yake ya kawaida anatembea na walinzi 15 makomandoo.

NB: Donge nono litatolewa kwa atakaye fanikisha kukamatwa kwake dola milioni 5 kwa Marekani na 3.8 kwa mexico, jumla dola milioni 8.8.

Nawasilisha
 

Attachments

  • 1437036260183.jpg
    1437036260183.jpg
    11.2 KB · Views: 1,638
Huu jamaa kiboko mbona ana asili kama mhindi
 
Duniani Kuna watu huzaliwa kwa staili ya aina yake
 
Hapo namba 5 rekebisha iwe kuanzia mwaka 1991 baada ya kukamatwa nchini Guatemala. Alipotoroka mwaka 2001 alikua katumikia miaka 7 ya kifungo chake cha miaka 20.

Namba 9, sio tu hawakuruhusiwa kutoka ,simu zao zilikusanywa ili mtu asije kutoa siri alipo na baada ya kutaa kuondoka alilipia bili na kuwataka watu radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Huyo alikua kipenzi cha wananchi kama alivyo lowassa au sio
 
ulinzi wake huwezi fananisha na wa obama. ana ulinzi wa hali yajuu lakini si kama ilivyo kwa obama
 
jamaa hatareee,hiyo hela waliyotoa kama zawadi ya kufanikisha kumkamata anaweza kuitoka hata yeye mwenyewe.wanajisumbua tu.na atakayetoa taarifa na kufanikiwa kukamatwa kwake akijulikana lazima wamdedishe
 
Mexico ina matajiri wa madawa wengi na soko lao kubwa ni wamarekani wenyewe
 
Back
Top Bottom