Fahamu kuhusu usimamizi wa miradi (Project Management)

Jul 3, 2016
19
45
Habari,

Ni matumaini yetu kwamba nyote mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na majukumu ya kitaifa.
Leo tungependa ku-share nanyi juu ya miradi (Projects) na usimamizi wake kiujumla (Projects Management)

USIMAMIZI WA MIRADI (PROJECT MANAGEMENT) ni utumiaji wa taaluma, ujuzi na zana za kitaalamu katika utekelezaji wa mradi (project implementation) ili kuhakikisha malengo mahususi ya mradi (project objectives) na malengo makubwa (project goals) yanafikiwa.

Mafanikio katika mradi yanaangaliwa katika utimilifu wa vipengele vitatu:
  1. Gharama (costs)
  2. Ratiba (Schedule)
  3. Uainisho (specification))
Hivyo basi kwa muktadha huu, USIMAMIZI WA MIRADI huweza pia kutafsiriwa kama kitendo kifanywacho na mameneja wa mirad katika utumiaji wa kila mbinu kuhakikisha mradi unatekelezeka ndani ya vipengele hivi vitatu (yaani gharama, ratiba na uainisho).

MRADI NI NINI ?
Kabla ya kutoa tafsiri ya neno hili ni vyema kwanza tukafahamu maana ya neno shirika (organization) na pia operesheni (operation)

Shirika ni kikundi cha watu waliojikusanya pamoja kwa ajili ya kufikia au kutimiza lengo fulani ima la kibiashara, kimichezo n.k
Operesheni ni shughuli yoyote ifanywayo na shirika yenye sifa ya kujirudia rudia,na pia yenye sifa ya kuwa endelevu.

Hivyo basi kwa mukatadha huu neno MRADI huweza kutafsirika kama ni shughuli yoyote ifanywayo na shirika isiyo ya kudumu yenye lengo la kutengeneza/kuleta bidhaa au huduma mpya ndani ya kipindi cha muda maalum na kwa kutumia kiasi maalum cha rasilimali (resources). Siku zote lengo kubwa la shughuli hii (yaani mradi) ni kuliwezesha shirika kufikia malengo yake ya kimkakati (strategic goals)

Sifa za mradi
Mradi siku zote huwa na sifa zifuatazo:

  1. Mradi una sifa ya upekee, hii ina maana ya kwamba mradi unapokamilika au kufikia malengo yake, huja na bidhaa au huduma ambayo haikupata kuwapo mwanzo katika eneo husika.
  2. Mradi huwa na muda maalum, utekelezaji wa mradi huanza kwa kipindi mahsusi na hupaswa kumalizika kwa kipindi mahsusi. Japo wakati mwingine mabadiliko katika mipango hutokea na kuathiri umaalum wa muda katika utekelezaji.
  3. Mradi huisha na huwa wenye mafanikio pale malengo yake mahsusi yanapofikiwa (project objectives), ambapo kufikiwa kwa haya malengo mahsusi hupelekea pia kufikia japo kwa asilimia kadhaa lengo kubwa la mradi (project goal)
Ni imani yetu kwamba kwa siku ya leo tumeweza ku-share nanyi juu ya hichi tulichonacho

Tunatoa huduma ya ushauri wa kitaalamu katika maeneo yafuatayo: PROJECT PLANNING AND MANAGEMENT, BUSINESS DEVELOPMENT AND MANAGEMENT, OPERATIONS MANAGEMENT, LEADERSHIP SKILLS DEVELOPMENT & TAX MANAGEMENT

Pia tunatoa huduma za:
-Uandishi wa michanganuo ya miradi (Project Proposals)
-Uandishi wa mipango ya biashara (Business Plans)
-Uandishi wa mipango mikakati ya mashirika (Strategic Plans)
-Utoaji wa semina katika maeneo tuyatoleayo ushauri wa kitaalamu.


Kwa mawasiliano tutafute kwa namba 0719 518367, 0657935110, 0783 695639
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com
 

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,522
2,000
Je mna uwezo wa kuandaa proposal za kutafuta donors ili kufadhiri miradi?
 
Jul 3, 2016
19
45
Gharama zenu zikoje hususani katika uandishi wa project proposals na pia mnapatikana wapi?
Na pia project proposal document endapo mtaniandalia itakuwa na vitu gani hasa?

Tunashukuru kwa swali lako mdau
Viambatanisho katika proposal inategemea na matakwa ya mteja, ila kiujumla hujumuisha
-Project description (hapa inajumuisha Problem justification, project goal, project objectives, project methodologie/strategies, stakeholders analysis n.k)
-Project budget (Bajeti)
-Logical frame work (Bao la mantiki)
-Monitoring and evaluation plan (Mpango wa ufuatiliaji na tathmini)
-Implementation plan (Mpango wa utekelezaji) n.k

Gharama ni kwamba, tunacharge 5% ya jumla kuu ya mradi (Grand total). Na kwa taasisi ambazo zinaomba pesa kutoka mashirika kama Foundation for Civil Society tunawasaidia mpaka kujaza fomu za maombi ya fedha.

Kwa upatikanaji wetu, tunapatikan mkoani Dar es Salaam,.

Tunatumai tumekidhi kiu yako.

Karibu sana.
 

Dhwahiri

Member
Jun 20, 2016
17
45
Je munafundisha Namba ya kuandika Project Proposal,Business Plan Na Strategic Plan.Naomba ufafanuzi tafazali
 
Jul 3, 2016
19
45
Je munafundisha Namba ya kuandika Project Proposal,Business Plan Na Strategic Plan.Naomba ufafanuzi tafazali

Ahsante kwa swali lako mdau.
Kwa sasa bado hatujaanza hiyo huduma, ila kama mpo organized tunaweza kuwafuata na kukufundisheni (Ikiwa mpo ndani ya Dar es Salaam)

Karibu sana mdau
 

Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,652
2,000
Projects triple constraints - scope, time and cost. Kwenye schedule ulimaanisha time? Kwenye specifications ulimaanisha scope. Ni muhimu utumie misamiati inakayoeleweka au kutumika duniani (pia kutegema na aina ya mradi). Usijefanya mwanafunzi wako akiwa kazini au kwenye conference au mkusanyiko wa wataalam wa usimamizi miradi akaanza kuulizwa we umesomea wapi, kama watajali; vinginevyo hawatamwelewa.
 
Jul 3, 2016
19
45
Projects triple constraints - scope, time and cost. Kwenye schedule ulimaanisha time? Kwenye specifications ulimaanisha scope. Ni muhimu utumie misamiati inakayoeleweka au kutumika duniani (pia kutegema na aina ya mradi). Usijefanya mwanafunzi wako akiwa kazini au kwenye conference au mkusanyiko wa wataalam wa usimamizi miradi akaanza kuulizwa we umesomea wapi, kama watajali; vinginevyo hawatamwelewa.

Habari mdau,
Ni kweli kwenye Schedule, tunamaanisha TIME, katika specification, hapa tunamaanisha "description of project objectives" (ambazo siku zote hupaswa kuwa SMART), japo Project Scope pia yaweza maanishwa as among project specifications.

Tumepokea ushauri wako juu ya matumizi ya misamiati, na tunaahidi kuufanyia kazi.

Ahsante sana, na Karibu.
 
Jul 3, 2016
19
45
Ni kwanini nyinyi msiandae hayo maandiko ya mradi mkapata fedha wenyewe badalaa ya kuwaandikia watu?

Habari mdau,
Ahsante kwa swali lako.
Kuna njia nyingi za kufanya kile kinachoitwa "knowledge and skills utilization" inaweza ikawa utilized kwa maslahi binafsi au kwa maslahi ya jamii.
Sisi tumeamua ku-utilize ujuzi na taaluma yetu hii kwa jamii, na ndio maana tunatoa huduma ya kuwaandikia michanganuo wale wenye kuhitaji. Japo hii haituzuii nasi kuandaa michanganuo ya maombi ya ruzuku kwa ajili yetu pindi tunapokidhi vigezo vinavyowekwa na wafadhili (Donars)

Karibu sana.
 

dangadunguri

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
1,279
2,000
Je mna uwezo wa kuandaa proposal za kutafuta donors ili kufadhiri miradi?

donors sio kwamba wanatoa pesa kwa uandishi mzuri, je umelenda their interests and areas??? na donors wanabadilisha maeneo yakutolea fund kila baada ya muda. Kwa bongo bila 10% andika mradi unaotaka hupati kitu
 

Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,652
2,000
Habari mdau,
Ni kweli kwenye Schedule, tunamaanisha TIME, katika specification, hapa tunamaanisha "description of project objectives" (ambazo siku zote hupaswa kuwa SMART), japo Project Scope pia yaweza maanishwa as among project specifications.

Tumepokea ushauri wako juu ya matumizi ya misamiati, na tunaahidi kuufanyia kazi.

Ahsante sana, na Karibu.

Scope sio description ya objective bali ni high level documentation ya project objectives, deliverables, tasks, budget and time (schedule). Project scope ndio mama wa project planning and integration.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom