Fahamu kuhusu mzunguko wa Maji duniani

complex31

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
379
1,208
Je, unafahamu ya kwamba maji yaliopo ulimwenguni ni yale yale yaliekuwepo toka Dunia kuumbwa, hayapungui wala kuongezeka.

Maji hutokea kwa kuchanganywa kwa hewa mbili ambazo ni Hydrogen na Oxygen ila Hydrogen zinakua mbili H2O.

Mvua ikinyesha haya maji hufata njia zake za asili (tributaries) na kwenda kwenye mifereji, mito, mengine huingia chini ya ardhi na kupita kwenye mito ilio chini ya ardhi na kufikia hitimisho ambayo ni maziwa, mabwawa na bahari.

Hivyo hivyo maji yatokayo majumbani na kuingia kwenye Choo au Chamber huenda kwenye mizunguko hiyo hiyo ya mito ilio chini ya ardhi.

Pia unapokuja maji hayapotei hujankutoka kwa njia ya mkojo au jasho yakiwa yamechanganyika na madini mengine yatokayo kwenye mwili.

Maji haya yaliotuama baharini kwenye maziwa, uliotumia kunyeshea mazao, garden na vinginevo kwenye ardhi huchomwa na jua na kugeuka (mvuke) na kwenda kutunga mawingu huko juu na kisha badae hurudi kama mvua.

Mengine huganda baharini na kutengeneza iceberg kwenye kanda zilizo na baridi kali north pole na South pole.

Hivyo circle ya maji inakua hiyo hiyo,

Hayaongezeki wala kupungua.
 
Kwahiyo zile story za visiwa kupotea ni utopolo

Maana maji ni yale yale tokea enzi na enzi.
 
Kwahiyo zile story za visiwa kupotea ni utopolo

Maana maji ni yale yale tokea enzi na enzi.

Iceberg zilizoko baharini pamoja na Barafu zilizoko Antartica au Greenland zikiyeyu ndio hupeleka baadhi ya visiwa kufunika au kina cha maji kuongezeka pempezoni mwa visiwa pamoja na Bara
 
Iceberg zilizoko baharini pamoja na Barafu zilizoko Antartica au Greenland zikiyeyu ndio hupeleka baadhi ya visiwa kufunika au kina cha maji kuongezeka pempezoni mwa visiwa pamoja na Bara
Lakini mkuu kama tulivyopata kuona.

System yenyewe iko automated kiasi cha kutotia shaka kiasi hicho,maana huko nchani kuna baridi sababu jua halifiki sawa sawa.
 
Lakini mkuu kama tulivyopata kuona.

System yenyewe iko automated kiasi cha kutotia shaka kiasi hicho,maana huko nchani kuna baridi sababu jua halifiki sawa sawa.

Global Warming inaleta maafa, vipindi virefu vya joto
Sehem kama Siberia Russia kumeanza kua na joto
 
Back
Top Bottom