MrPhilosopher Kanju
Member
- Aug 26, 2017
- 63
- 66
JE UKOMAVU WA KIAKILI NI NINI? SABABU ZINAZO PELEKEA MTU KUKOMAA KIAKILI, SABABU ZINAZO PELEKEA MTU KUSHINDWA KUKOMAA KIAKILI, JE UNAWEZAJE KUMTAMBUA MTU ALIYEKOMAA KIAKILI.
NA, Mr PHILOSOPHER KANJU
Je ukomavu wa kiakili ni nini?
Ukomavu wa kiakili ni hali ya akili kufikia kipimo cha kujua kwa kina, kupembua, kuchuja mambo kiyakinifu na kwa usahihi, umahiri, umahiri kuzingatia context /muktadha husika na kila kitu azungumzacho kuwa na logic/mantiki ndani yake. Ukomavu kiakili hupelekea mtu kuweza kuwe za kuchagua maneno ya kusema na kuyachuja kabla ya kutumia kinywa kuyatoa nje na kusikika kwa watu. Ukomavu wa kiakili humfanya mtu kujisikiliza mwenyewe kwanza (kujisemea kimoyo moyo) na kukichujakitu unacho taka kukisema ili ukichanganue kwamba kina mantiki ndani yake au la.
Hii itapelekea kila unapozungumza kuzungumza vitu vyenye mantiki ndani yake na kuondosha uwezekano wa kuzungumza mambo ambayo yatakuwa na makosa ya kimantiki (fallacy in argumentation). Hivyo kutokana na ukomavu wa kiakili utakuwa na uwezo wa kutambua wakati sahihi wa kuongea na mtu sahihi wa kuongea naye na kupitia ukomavu ulio nao utakusaidia kuwajua watu kutokana na uzungumzaji wao.
Na pia ukomavu wa kiakili ni hatua maridhawa kwa mtu kuwa na uwezo wa kuitumia akili kwa ufanisi wa hali ya juu na mtu mwenye ukomavu wa kiakili kuwa na uwezo wa kutumua angalau asilimia 80 ya akili katika kila kitu afanyacho.
Na hapa mtu huyu anakuwa na uwezo wa ku reasoning, ku boubt, kutoa judgmenet na kasha kutoa justification kwa kila kitu awazacho. Na kufikia level hii ya kufikiri hupelekea mtu kuwa na uwezo wa kuzuia emetions, feelings katika kufanya maamuzi hivyo utakuwa unaongozwa na akili kwa kila jambo ufanyalo hivyo ukishafikia katika hatua hii unaitwa critical thinker. Hivyo ukomavu wa kiakili hupelekea na kuleta matokeo chanya kwa mtu kwa sababu mtu huyu anakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
Sababu zinazo pelekea mtu kukomaa kiakili?
Zipo sababu nyingi sana za kukomaa kiakili. Baadhi ya sababu hizo ni kama vile.
Kusoma vitabu vingi vyenye kuongeza maarifa. Ubongo hauhitaji chakula cha kula kwa mdomo ili unawili, kujipanua na kukua bali huhitaji kupata na kuingiza maarifa mapya kila siku kwa kusoma vitabu mbalimbali. Hivyo kutokana na kawaida ya kusoma huufanya ubongo kukomaa na kuingiza maarifa mapya na nadharia mbalimbali kupitia nyanzo mbalimbali vya kupata maarifa kama vile vitabu, makala na hata majarida mbalimbali.
Kutokana na mwingizo wa maarifa mapya huufanya ubongo kuwa active muda wote na kuweza kufanya upembuzi yakinifu juu ya nadharia mbalimbali. Ubongo unapopata chakula chake kupitia maingizo mapya ya vitu mbalimbali ulivyo soma huufanya ubongo kuwa kutambua kwa haraka kilichoandikwa sehemu husika na hapa kuifanya akili kuwa makini sana kwa kile kitu kipya kilicho ingia kwenye ubongo hivyo kazi ya akili ni kupima, kuchuja, na kukipitisha kile kilichochujwa na akili ambavyo vyote vilikuwa kwenye ubongo na kuweza kukihifadhi katika memory ya kuhifadhi mambo katika mfumo wa ubongo. Hivyo kupitia kusoma nadharia, majarida, makaka na vibatu mbalimbali hupelekea ukomavu wa kiakili.
Kusoma vitabu mbalimbali vyenye kuifikirisha akili. Pia kusoma vitabu mbalimbali vyenye kuifikirisha akili humfanya mtu kupataa wasaa wa kutulia na kufikiria kwa kina yale yaliyo andikwa sehemu husika hivyo hupelekea kutafuta majibu kwa kujiuliza mwenye na kwa kutafuta majibu juu ya vitu vyote zilivyomtatiza. Kawaida haipendi kusumbuliwa ndio maana watu wengine ambao hawajakomaa kiakili hawapati muda wa kuifikirisha akili na watu hawa ndio wale watu ambao kila kitu akisikiacho hukiamini papo hapo bila kukipima kwamba hicho kitu kina ukweli wa aina gani ndani yake na hii hupelekea watu wengi kuamini vitu vya uongo kwa sababu hawana uwezo wa kufanya upembuzi juu ya walivyo visikia. Hivyo ukiwa na uwezo wa kuifikirisha akili utaifanya akili kuwa bize kutafuta majibu na kawaida ya akili ukiwa na kawaida wa kuisumbua hukuletea majibu kwa haraka zaidi. Na kupitia hii wewe utakuwa mtu wa kuelewa vitu mapema kwa sababu huilazi akili bali huiamsha kwa kuifikirisha hivyo kupitia dhana hii akili hukomaa kwa sababu utakuwa na uwezo wa kutatua maswali magumu.
Utayari wa kuikomaza akili. Pia hii ni sababau moja wapo ya mtu kukomaa kiakili, utayari huu humfanya mtu awe neutral kwa kila kitu mtu huyu anatakiwa kuwa huru katika akili yake, anatakiwa asiwe na kizingiti chochote kinacho izingiti akili yake. Kwa ujumla naweza kusema mtu huyu anatakiwa kufikiria nje ya box na si ndani ya box. Unatakiwa kutokuwa mfungwa wa kitu chochote maana yake unatakiwa unapokuwa mfungwa kitu fulani basi utakuwa huna uwezo wa kukipinga kitu ambacho unakiona sio sahihi hivyo ukishidwa kukijaji kitu ambacho unakiona hakija kaa sawa basi wewe teali utakuwa mfungwa wa kitu na kwa maana hiyo utakuwa unafikiri ndani ya box na sio ndani ya box.
Maana yake ukisha kuwa teari kuifanya akili yako ikomae basi maana yake unatakiwa usiwe mfungwa wa imani yeyote bali wewe utumie akili katika reasoning na si kutoa maamuzi ambayo yatakuwa na madhaifu ndani yake. Ndio maana kupitia hili mwanafalsafa Rene Descartes ”usiamini kitu bila ya kuthibitisha kwamba kweli kipo na unatakiwa ku doubt kwa kila kitu na ku reasoning kila kitu then ndio uje na justification juu ya kitu na inatakiwa kudoubt hata uwepo wako wewe kama kweli upo” haya ameyatoa katika nadharia yake ya maarifa itwayo Rene Descartes’s MEDITATION ON THE FIRST PHILOSOPHY. Hivyo ukisha kuwa na uteyari wa kuikomaza akili yako basi utakuwa na uwezo wa kupokea kila aina ya maarifa hata kama yanakinzana na imani yako lakini wewe utakuwa na uwezo wa kuyapokea kwa kuiangalia mantiki iliyopo ndani ya maarifa hayo.
Uwezo wa kufikiri kwa kina au kufanya Meditation. Mwanafalsafa Rene Descartes na Emmanuel Kant wote huamini kwamba meditation/ Taamuli humfanya mtu wa kawaida kukomaa kiakili kwa sababu meditation ni hatua kubwa ambayo mtu hufanya (Transcendental abstraction) ambapo mtu kuwa na uwezo wa kwenda hadi katika mind yake na kuweza kutambua yale yaliyopo katika mind yake na hii meditation husaidia kupata majibu ya maswali magumu ambayo umeshindwa kuyapata kwa akili ya kawaida na pia husaidia kutoa Illusions/ makando kando yaliyopo kwenye ubongo na kuufanya ubongo kuwa clear na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi njia hii pia aliitumia Rene Descartes na mwanasayansi wa Fizikia ya kisasa (modern Physics) Albert Einstein ambaye ilimsaidia hadi kutoa nadharia mbalimbali kama THEORY OF GENERAL RELATIVITY. Hivyo kufikiri kwa kina na kufanya meditation huifanya akili kukomaa.
Sababu zinazo pelekea mtu kushindwa kukomaa kiakili.
Zipo sababu vyingi sana zinazo pelekea mtu kushindwa kukomaa kiakili. Sababu za jumla zinazo pelekea mtu kushindwa kukomaa kiakili kwanza
Mazingira yanaweza kumfanya mtu kushindwa kukomaa kiakili. Mazingiza amabayo hayana changamoto zozote ni ngumu sana mtu kukomaa kiakili kwa sababu hayo yatakuwa mazingira ambayo watu wake wamebweteka na wameridhika na hali walizo nazo hivyo watu hawa wakiwa na hali kama hii wanakuwa na ukomo wa kufikiri hivyo mtu akishakuwa tu na ukomo wa kufikiri basi hatakuwa na uwezo wa kufikiri zaidi hivyo hata kukitokea changamoto zozote hawatokuwa na njia ya kuzikabili bali watazipokea na kuamua kuishi nazo hivyo kila tatizo linalo zuka litakuwa ni ngumu kutatulika kwa sababu walengwa wanakuwa wameshindwa kupata njia ya kuzikabili changamoto kwa sababu ukomavu wao wa akili ni mdogo na upo limit.
Pia aina ya watu unaochangamana nao. Watu unaochangamana nao ndio watakufanya wewe uwe mtu wa aina gani ukichangamana na watu ambao hawawazi ya maana kamwe huwezi komaa kiakili kwa sababu watu unaochangamana nao hawawezi kusaidia akili yako iwe fikirifu hivyo unapokosa ufikirifu wa akili basi kamwe huwezi pata ukomavu wa akili kwa sababu ukomavu wa akili unatokana na akili kufanya kazi yake kwa ufanisi wa hali ya juu hivyo akili ikifanya kazi yake yake ya kufikiri kawaida kamwe haiwezi komaa kwa sababu haipati changamoto ya kiufikirifu.
Je unawezaje kumtambua mtu aliyekomaa kiakili.
Mtu aliyekomaa kiakili utamtambua kwa mambo afanyayo hufanya mambo ambayo hayana makosa ya kimantiki. Na mtu aliyekomaa kiakili utamtambua kwanza jinsi anavyo ongoa ni mtu ambaye kwanza amejawa na hekima nyingi na busara hivyo ni mtu ambaye huchagua maneno ya kuongea kutokana na muktadha husika na kutambua mtu na wakati sahihi wa kuongea. Pia mkomavu wa akili utamtambua katika kutoa maamuzi hutoa maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi. Na mkomavu wa akili utamtambua kwa kugundua changamoto na kuzitatua. Hivyo yapo mambo mengi sana ambayo yatapelekea kumtambua mtu aliyekomaa kiakili.