Fahamu Kuhusu Kubadili Private Company Kuwa Public Company

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,497
5,533
Habari za mwaka huu wa 2023, ni amtumani yangu kwamba katika safari yako ya upambanaji unaendelea kujipa moyo na kupambana kwa nguvu.Usikate tamaa.

Leo nataka nichongoze mada ndogo yenye ukubwa. Naichokoze hii mada ili niweze kuamsha hamasa kwa wale ambao wana maono makubwa basi waweze kuendelea kuwa na maono makubwa zaidi. Leo hii nitazungumzia jinsi ya kubadili kampuni ambayo ni Private LIMITED Company kuwa Public Limited Company.

Lakini kabla ya kuzama ndani nieleze kwa ufupi tofauti zake

Tofauti ya Public Limited na Public Limited Company ipo zaidi katika eneo la idadi ya wanahisa na uwezo wa kuwaalika watu wengine ili wanunue hisa katika kampuni husika. Kwa kawaida Public limited company zinakuwa na uwezeo wa hisa zake kuuzwa katika soko la hisa kama vile DSE.

Kwa hivyo basi ili kampuni iweze kushiriki katika soko la hisa ni lazima ibadilishwe kutoka Private na Public.Hata hivyo ni muhimu tufahamu kwamba Kampuni kuwa Public hakumaanishi kwamba ni lazima iwe listed ndio maana unaweza kukutana na kampuni ambayo ni public lakini huwezi kukuta katika soko la hisa.

Hata hivyo uzuri wa kampuni ambayo ni Public ni kwamba mmiliki anakuwa na uwezo wa kuhamisha hisa zake kwenda kwa mwingine bila kuzuiwa na bodi.Kwenye kampuni binafsi mwanahisa hana uwezo/ruhusa ya kufanya hivo bila idhini ya bodi.

Nimekutana na wajasiriamali wengi ambao wanataka kuanzisha kampuni huku lengo lao likiwa ni kupata mtaji na mara nyingi nawauliza kuhusu maono yao na utayari wao wa kuweka taarifa za kampuni wazi ili ziwe scrutinized na watu wote kwani huo ndio msingi wa kampuni public.

Wengi huofia na huamua kuanza na Privte Company ambapo baada ya biashara kukua basi huweza kubadilisha kampuni kuwa Public.

Hata hivyo lazima nikiri kwamba bado kwa Tanzania kuna changamoto ya watu kuwa na utayari wa kubadlli kampuni zao za Private kuwa Public hali ambayo hupelekea watu kushindwa kutumia fursa za kujenga ukwasi.

Wengi hawafahamu kwamba kila biashara ina hatua ya kuzaliwa,kukua,kufika kilele,kuporomoka na kufa/kufilisika.

Hivyo basi kitendo cha kuifanya kampuni Private kuwa public inapofika katika kilele cha mafnikio huipa kampuni uhai mpya na kumwezesha mmiliki kuvuna faida na kwenda kuwekeza katika biashara nyingine changa huku akiacha sasa kampuni ikue zaidi chini ya mikono ya wengine.

Sasa leo nataka nieleze kwa ufupi tu jinsi ya kubadilisha kampuni Private kuwa Public.

Hatua ya kwanza ya kubadilisha Private Company kuwa Public Company inaanzia kwenye Memorandum and Articles of Association ambazo ni lazima zifanyiwe marekebisho ili ziendane na matakwa ya sheria kwa Public Company.

Baada ya hatua hii nyaraka huwasilishwa kwa mrajisi wa Makampuni kwa ajili ya usajili na mchankato huu ukikamilika basi kampuni inakuwa ni PUBLIC LIMITED COMPANY.

Baada ya hatua kama unahitaji kampuni yako iwe listed kwenye soko la hisa itakupasa uwasilishe nyaraka na taarifa katika mamlaka ya soko la mitaji na dhamana kwa Tanzania wanaitwa CMSA ili wakague na kujiridhisha juu ya ukweli wa taarifa uulizotoa kuhusu hali halisiya kampuni yako/yenu.

Moja ya nyaraka ambayo mtapaswa kuwasilisha inaitwa Prospectus ambayo hii inakuwa ni kama Business Plan inayoonyesha hali halisi ya kampuni pamoja na matarajio ili kuwaonesha wawekezaja tarajali kwamba mmejizatiti kama kampuni kwa ajili ya kufanya biashara.

Ni muhimu sana unapoanzisha kampuni uwe na maono juu ya uelekeo wa kampuni yako hasa iwapo una mpango wa kuifanya iwe ni PUBLIC company kwani utakapoweza kuifanya kampuni yako kuwa PUBLIC utakuwa umefikia kiwango cha kuweza kujipima kwamba umejenga kampuni yenye hadhi.

Uzuri ni kwamba Unaweza kuifanya kampuni kuwa limited bila kupoteza mamlaka yako ya usimamizi wa kampuni. Unaweza kufanya hivi kwa kuhakikisha kwamba wewe unakuwa ni majority shareholder au unaweza kuwapawanahisa hisa ambazo hazina nguvu ya kupiga kura (Non voting shares).

Ukiongea na mwanasheria anayefhamu sheria za makampuni anaweza kukuengenezea waraka ambao unakupa nguvu ili usije ukawaalika watu na wakaja kukuvurugia maono yako.

Karibu tujadili zaidi kuhusu kampuni za Private na Public na juu ya faida zake katika uchumi wa taifa letu.
 
Aksante
Screenshot_20230112-083904.jpg
Screenshot_20230112-102146.jpg
Screenshot_20230112-102156.jpg
 
Back
Top Bottom