Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,954
- 8,093
CT Scan (Computerized Tomography Scan) ni aina ya kipimo cha kuchunguza tishu na ogani za mwili kwa kutumia mionzi ya X-ray. CT scan huweza kupima sehemu zote za mwili, kuanzia kichwani mpaka miguuni. Pia hujulikana kama Computed Axial Tomography (CAT scan) auX-ray Computed Tomography (X-ray CT Scan). Hiki ni kipimo kisichosababisha maumivu yoyote wakati kinafanyika
Namna Inavyofanya Kazi
Mashine ya CT Scan ina sehemu ya kulala na mtambo wa X-ray wenye umbo kama donati. Wakati wa kupimwa utalala kwenye kitanda kisha mtambo wa X-ray utapelekwa sehemu inayotaka kuchunguzwa.
Kwa kutumia mionzi ya X-ray, picha nyingi hupigwa kutoka pande mbalimbali za sehemu ya mwili inayochunguzwa. Kisha kompyuta huunganishwa picha hizi kutoa picha ambazo huonesha ndani mpaka nje ya mwili. Picha hizi hutoka kwa slices (vipande vipande) vya sehemu za mwili. Pia huweza kutoa picha za 3D za sehemu inayochunguzwa. Kwa kurahisisha uelewa, fikiria kama mtu anakata mkate; Hivyo basi, CT scan huchukua picha za sehemu za mwili kwa vipande vipande visivyozidi milimita moja katika upana (kama vipande vya mkate); Hivyo kuwezesha kuona viungo na ogani za ndani ya mwili. CT scan za kisasa zina uwezo wa kupiga slices hadi 640.
Picha za CT Scan hutoa picha zenye taarifa nyingi zaidi kuliko picha za X-ray za kawaida. CT Scan ina uwezo wa kuonesha tishu za kawaida na zisizo kawaida.
CT Scan haina maumivu yoyote wakati inapofanyika na haihitaji maandalizi maalumu.
Contrast media, dawa yenye madini ya joto (Iodine) hutumika kusaidia tishu za mwili kuonekana vizuri kwenye picha za CT Scan.
Kuna aina mbalimbali za CT Scan ambazo hutegemea na sehemu ya mwili inayochunguzwa.
Kuna aina zifuatazo;
- CT Scan ya Kichwa (CT Scan of the Brain)
- CT Scan ya kifua (Chest CT Scan)
Cardiac CT inaweza kufanyika kuchunguza moyo.
- CT Scan ya Tumbo na Kiuno (Abdominal and Pelvic CT)
- CT Scan Ya Miguu na Mikono (CT Scan Of The Extrimities)
CT Angiography
CT Angiography ni aina ya CT Scan ambayo hutumika kuchunguza mishipa ya damu ya sehemu maalum ya mwili. Hutumia contrast ambayo huweza kwenye mishipa ya damu inayoenda kwenye sehemu inayotaka kuchunguzwa na kisha picha za CT kuchukuliwa kama kawaida. Husaidia kugundua matatizo yanayotokana na mishipa ya damu au damu kuganda.
Matumizi Ya CT Scan
Kipimo cha CT Scan hufanyika ili;
- Kugundua uvimbe kwenye misuli, mifupa au viungo vya mwili, ukubwa wake na mahali ulipo.
- Kugundua sehemu mifupa ulipovunjika
- Kuongoza vipimo vingine kama kutoa kinyama sehemu fulani ya mwili kwa ajili ya histopatholojia au utoaji wa mionzi kwa ajili ya matibabu.
- Kufuatilia matibabu ya magonjwa mbalimbali kama ya moyo, saratani, uvimbe kwenye mapafu, tumbo au ini.
- Kugundua viungo vilivyoumia kwa ndani au kuvuja damu (internal injuries and internal bleeding)
Kipimo cha CT Scan hakina maamdalizi maalum kabla ya kufanya.
Madhara
Mionzi inayotumika kwenye CT Scan inaweza kuleta madhara kwenye seli za mwili na kuharibu vinasaba hivyo kuleta hatari ya saratani miaka mingi baadae. Kiasi cha mionzi kwenye kufanya CT Scan moja ni karibu mara 100 ya mionzi ya picha ya X-ray moja. Hata hivyo, uwezekano huu wa kupatan saratani hapo baadae ni mdogo, na unazidi faida inayopatikana kwa kufanya CT scan.
Contrast media, inayotumika kuonesha tishu vizuri kwenye CT Scan huweza kuleta allergy (mzio) kwa mgonjwa.
Usalama Wa CT Scan Wakati Wa Ujauzito
CT Scan ambazo zinafanyika maeneo ambayo sio tumbo na kiuno hazina madhara yoyote kwa mtoto tumboni.
CT Scan ya maeneo ya tumbo na kiuno hufanya mtoto apate mionzi ya X-ray ambayo inaongeza uwezekano wa mtoto kupata saratani ukubwani kwake. Kwa hiyo haishauriwi kufanya CT Scan tumboni na kiunoni isipokuwa pale ni muhimu kuokoa maisha ya mjamzito.