Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,825
- 6,429
Habari za wakati huu;
ni muda mrefu tangu niliposhiriki mijadala hapa jukwaani.Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo sababu za mbalimbali ikiwemo za binafsi na za ujumla.Hata hivyo leo nimewiwa kurejea na kuleta muendelezo wa mijadala yetu ya biashara na ujasiriamali nikiamini kwamba kuna ambao inawasaidia.
Wakati naanza kuandika mijadala hii hapa jukwaani AI ilikuwa bada haijawa maarufu sokoni hivyo basi nilijitahidi sana kuandika kwa kadiri ya uelewa wangu.Hivyo basi nisisitize kwamba ninayoandika hapo ni maoni yanayotokana na uelewa wangu na sio ushauri wa kitaalmu.Vile vile unaweza kutumia AI kujifunza zaidi kuhusu biashara na ujasiriamali.Tusisahau kutafuta ushauri wa kitaalmu pale tunapotaka kuchukua hatua kuhusu ushauri wowote tunaopata mtandaoni.
Leo ninaleta mada inayohusu Debt instruments au Dhamana za Madeni.Debt isntruments ziko za aina nyingi kama vile Bank Guarantees,Letters of Credit,Mortgages n,k, Hata hivyo leo nitazungumzia aina ya Debt Instrument ambayo kimsingi inaweza kubeba hizo aina nyingine za Debt instrument ambayo huwa inaitwa Debentures.Debenture kwa kiswahili zinaitwa Hati Fungani(Kama sijakosea).
Katika biashara kuna wale ambao huwa wanawapa wafanyabiashara wenzao(Makampuni) mali kwa mkopo(Mali kauli) na kuna wale ambao huwa wanachukua mkopo Benki na kuutumia kununua mzigo wa biashara au kufanya uwekezaji.Kwa wale ambao huwa wanaenda Benki huwa wanapewa nyaraka mbalimbali kama vile Debenture Agreement na Mortgage Charge Sheet pamoja na nyaraka nyingine.Kwa wale ambao huwa wanapewa mkopo wa bidhaa(Mali kauli) huwa kunakuwa na Makubaliano fulani ya maandishi kwa kutegemea mahusiano inagwa wengi huwa hawalipi hili swala uzito.
Katika biashara hasa unapoamua kuunda kampuni,ni muhimu sana ukafahamu kwamba faida ya kampuni moja wapo ni uwezo wa kupata mtaji kwa njia mbalimbali ikiwamo kwa kupitia hizi njia za financing VIA Debt yaani kupata mtajia kupitia Deni.Ingawa wengi hutamani kupata mkopo kupitia Benki lakini changamoto kubwa ya benki ni kwamba huwa wanahitaji kufahamu Historia yako kibiashara ili waweza kuamua iwapo unafikia vigezo vya kupewa mkopo.Hivyo katika hatua za mwanzo utahitaji kutafuta namna ya kuingia katika mikataba na makubaliano ya aina mbalimbali kwa faida za kibiashara.
Debentures ni aina ya njia hizo ambazo unaweza kuzitumia ambapo huwakiutaratibu zinapaswa kulipiwa Stamp Duty na Kusajiliwa ofisi ya Msajili wa Makampuni.Zinaposajiliwa zinatambulika kisheria na inapotokea kampuni inafilisiwa huwa Zinapewa kipaumbele cha kulipwa kwanza kwa kutegemea aina ya makubaliano.
Faida nyingine za kuwa na makubaliano ya kikampuni ni kwamba inakusaidia sana katika kuhakikishwa kwamba unakuwa na credibility kwani makubaliano huwa ni msingi wa kuonesha uwezo wa kufanya kazi au biashara fulani.
Karibuni tujadiliane zaidi kuhusu Debentures,Debt Instrument,Mikataba na Dhamana ya Deni.
Iwapo unapenda kufahamu zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia Email:masokotz@yahoo.com.
Unaweza pia kuwasiliana nasi kwa ajili ya ushauri na msaada katika usajili wa Biashara,Leseni na Usimamizi wa biashara.Karibuni.