Binafsi me napenda documentaries na taarifa mbalimbali kuhusu nature na yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Kwa kuzingatia hili niliwahi kufatilia makala kadhaa zenye kuzungumzia maeneo hatarishi zaidi duniani. Na moja ya maeneo haya ni pale wanapopaita Nyumba ya shetani ama "Bermuda Triangle".
BERMUDA TRIANGLE[emoji848]
Bermuda Triangle ni eneo la Bahari ya Antlantiki mbele ya pwani ya Amerika Kaskazini, baina ya Florida, Puerto Rico na visiwa vya Bermuda.
Tangu miaka 1960s jina la "pembetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili
Bermuda Triangle,ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle ni eneo la magharibi mwa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kubwa ya ndege na vyombo vya baharini vinadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama, hitilafu ya vifaa, maafa ya asili.
Tamaduni maarufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili
Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi.
Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa muda wa miaka 500.
Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda.
Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Hata hivyo wanasayansi wameshindwa kutoa uthibitisho dhahiri wa mgongano huo.
Wanasayansi wengi wameshindwa kutoa majibu sahihi juu ya kupotea kwa ndege na vyombo mbalimbali vya usafiri eneo hilo wakiishia kupaita "NYUMBA YA SHETANI" wakinasibu na uwepo wa makazi ya shetani eneo hilo.
Mdau wa JF tupe knowledge uliyonayo kuhusu eneo hili.
View attachment 2533909View attachment 2533908