Fahamu kuhusu Bermuda triangle

Fahamu kuhusu Bermuda triangle

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,479
Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamsha meli, ndege pamoja na binadamu.

4. Viumbe vigeni viishivyo sayari nyingine (aliens).
Inasemekana kuwa viumbe viishivyo angani, huwa vinakaa aktika eneo hilo la Bermuda triangle na hilo ni kama Mecca yao. Viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu yat Duniani,

kwahiyo basi ndege, meli pamoja na binadamu wanapopita pale huvutwa na kani ya uvutano ambayo ni kubwa sana toka kwa wale viumbe waishio katika ilo eneo hilo la bermuda.

5. Kituo cha majaribio ya silaha.
Inasemekana serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo, pia inasemekana kwamba serikali ikishirikiana na viumbe watokao sayari (Aliens) zingine huhusika katika majaribio hayo.

Na hiyo teknolojia ni kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege pia.

6. Mji uliopotea
Inasemekana katika eneo hilo kulikuwa na mjia wa kale chini ya maji katika bahari ya Atlantic, ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati.
Na huo mji ulisahaulika milele kwahiyo basi Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege.

7. Kituo cha Maharamia
Inasemekana Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao, maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bend-era nyeusi zenye picha ya fuvu. Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwanini ndege na meli huwa zunapotea katika eneo hilo kwani

wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.

8. Volkano.
Inasemekana Volkano pamoja na gesi ya methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama. Eneo hilo mlimekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita.

FB_IMG_1676581963662.jpg
FB_IMG_1676581977894.jpg
FB_IMG_1676581981579.jpg
FB_IMG_1676581969523.jpg
 
Attachments

  • FB_IMG_1676581963662.jpg
    FB_IMG_1676581963662.jpg
    54.3 KB · Views: 85
Hapo ni sehemu ambayo upepo toka pande nne za dunia hukutana na kufanya msuguano kuelekea chini kwenye bahari na kutengeneza jicho kwenye maji ambalo huzunguruka kuelekea chini, hivyi huvimeza vitu vyote vipitavyo eneo hilo.
 
Binafsi me napenda documentaries na taarifa mbalimbali kuhusu nature na yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Kwa kuzingatia hili niliwahi kufatilia makala kadhaa zenye kuzungumzia maeneo hatarishi zaidi duniani. Na moja ya maeneo haya ni pale wanapopaita Nyumba ya shetani ama "Bermuda Triangle".

BERMUDA TRIANGLE
Bermuda Triangle ni eneo la Bahari ya Antlantiki mbele ya pwani ya Amerika Kaskazini, baina ya Florida, Puerto Rico na visiwa vya Bermuda.

Tangu miaka 1960s jina la "pembetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili

Bermuda Triangle,ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle ni eneo la magharibi mwa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kubwa ya ndege na vyombo vya baharini vinadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama, hitilafu ya vifaa, maafa ya asili.

Tamaduni maarufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili

Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi.

Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa muda wa miaka 500.

Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda.

Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Hata hivyo wanasayansi wameshindwa kutoa uthibitisho dhahiri wa mgongano huo.

Wanasayansi wengi wameshindwa kutoa majibu sahihi juu ya kupotea kwa ndege na vyombo mbalimbali vya usafiri eneo hilo wakiishia kupaita "NYUMBA YA SHETANI" wakinasibu na uwepo wa makazi ya shetani eneo hilo.

Mdau wa JF tupe knowledge uliyonayo kuhusu eneo hili.

1677682395737.jpg
View attachment 2533908
 
Na hata wakifika hapo mawasiliano yanakata na dira haisomi tena kisha wapotelea kusiko julikana.
 
Maria Celestine , yatch ilipotea Katika eneo la Bermuda triangle na ikapatikana maili kadhaa nje ya eneo hilo lakini abiria na capteni hawakuwemo, na kila kitu ndani ya chombo hicho kilkuwa intact, Kama vile glass na chupa za pombe zilizokuwa mezani zikiwa bado mezani. Ni Kama vile watu wameondoka na kuiacha meli.
Hiyo ndio Bermudas triangle ( Wormhole to the unknown underworld)
 
Hii ni stori ni kweli?
 
Utafiti na uchunguzi wa Bermuda Triangle haujawahi kukamilika na kutoa majibu. Mpaka atakaposhuka Mtu huko chini na kurudi.
 
Hili eneo nimepita hapo naelekea orlando Florida kwanza mkifika hapo ndege inayumba kama basi linaloendeshwa kwenye makorongo ndege inasumbuka sana ni zaidi ya dk 45 za hiyo shida mkifika hapo service zote za ugawaji wa vyakula vinywaji hustop mpaka mvuke eneo hilo kama uja funga mkada wa sit utajikuta umerushwa kutoka sehemu ulipo mpaka sehemu ingine hapa kila mtu humuanvalia mwenzake akihofia ndio ndege inaenda kuanguka soon hapa ule usemi mavi yanagonga chupi yana rudi hapo ndio mahara pake kiukweli panatisha sana mkiwa anga hilo
 
Binafsi me napenda documentaries na taarifa mbalimbali kuhusu nature na yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Kwa kuzingatia hili niliwahi kufatilia makala kadhaa zenye kuzungumzia maeneo hatarishi zaidi duniani. Na moja ya maeneo haya ni pale wanapopaita Nyumba ya shetani ama "Bermuda Triangle".

BERMUDA TRIANGLE
Bermuda Triangle ni eneo la Bahari ya Antlantiki mbele ya pwani ya Amerika Kaskazini, baina ya Florida, Puerto Rico na visiwa vya Bermuda.

Tangu miaka 1960s jina la "pembetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili

Bermuda Triangle,ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle ni eneo la magharibi mwa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kubwa ya ndege na vyombo vya baharini vinadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama, hitilafu ya vifaa, maafa ya asili.

Tamaduni maarufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili

Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi.

Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa muda wa miaka 500.

Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda.

Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Hata hivyo wanasayansi wameshindwa kutoa uthibitisho dhahiri wa mgongano huo.

Wanasayansi wengi wameshindwa kutoa majibu sahihi juu ya kupotea kwa ndege na vyombo mbalimbali vya usafiri eneo hilo wakiishia kupaita "NYUMBA YA SHETANI" wakinasibu na uwepo wa makazi ya shetani eneo hilo.

Mdau wa JF tupe knowledge uliyonayo kuhusu eneo hili.

View attachment 2533909View attachment 2533908
"kitabu cha mnyazi mungu kimeeleza haya yote"
 
Hamna ukweli wa hizo picha wala maandishi hayo.
Movie ndio zinadanganya.
kama huna elimu ya kutosha utaamini.
ni eneo linasemekana kupoteza vitu vingi ila haijawahi kuwa prved, ajali hata victoria zinatokea.
Hiyo idea imekuja juzi juzi mwanzo wa karne ya 20.
Msiogope hamna hiyo stry wala sehemu ya bermuda haina maji yanazunguka hivo😂😂😂.
 
Hamna ukweli wa hizo picha wala maandishi hayo.
Movie ndio zinadanganya.
kama huna elimu ya kutosha utaamini.
ni eneo linasemekana kupoteza vitu vingi ila haijawahi kuwa prved, ajali hata victoria zinatokea.
Hiyo idea imekuja juzi juzi mwanzo wa karne ya 20.
Msiogope hamna hiyo stry wala sehemu ya bermuda haina maji yanazunguka hivo.
 
Ngoja tumuombe ndugu Kiranga aje atie neno ili tuongeze ufahamu wale tulio na taarifa finyu juu ya eneo hilo
 
Maria Celestine , yatch ilipotea Katika eneo la Bermuda triangle na ikapatikana maili kadhaa nje ya eneo hilo lakini abiria na capteni hawakuwemo, na kila kitu ndani ya chombo hicho kilkuwa intact, Kama vile glass na chupa za pombe zilizokuwa mezani zikiwa bado mezani. Ni Kama vile watu wameondoka na kuiacha meli.
Hiyo ndio Bermudas triangle ( Wormhole to the unknown underworld)
dunia pmj na teknlojia yte wamesgndw kjua nn knajik hapo mpak leo?
 
Back
Top Bottom