Fahamu kisa cha huyu binti kujinyonga

Fahamu kisa cha huyu binti kujinyonga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,158
Reaction score
831,829
Nadhani mnakumbuka kisa cha huyu binti ambaye kwa sasa ni marehemu RIP aliyejinyonga akiwa chuoni Iringa?
Huyu binti ni mmojawapo wa wahanga wa mimba za bahati mbaya? Mimba kabla ya ndoa... Lakini aliweza kuhimili kwa kupitia magumu yote mpaka kujifungua na hatimaye baada ya muda kuweza kuendelea na masomo yake ngazi ya chuo...
Kwa jinsi inavyosemwa mahusiano yaliyozaa mimba na hatimaye mtoto hayakuwa endelevu... Lakini binti akawa ana faraja kwa kuwa na mtoto mzuri wa kiume asiye na tatizo lolote....
Matendo ya Mungu si ya mwanadamu.... Mtoto yule mzuri akatwaliwa na Bwana mwezi March mwaka huu akiwa na miaka 3... Jiweke kwenye nafasi ya huyu binti... Uyaone maumivu yake... Lakini mbaya zaidi, baba mtoto kwa sababu zisizojulikana hakufika msibani wala hakuhudhuria mazishi ya mwanae... Ikawa ni maumivu juu ya maumivu kwa mama wa mtoto.... Ila akafarijiwa na kufarijika kuwa hili nalo litapita!

Ikiwa ni chini ya siku 40 tangu msiba... Likatokea lingine kubwa zaidi na lililomuongezea maumivu mama mtoto marehemu..... Mzazi mwenzie yule aliyeshindwa hata kufika kaburini kwa mwanae akaoa / akafunga ndoa na mwanamke mwingine tena kwa sherehe!
Kumbuka mtoto alifariki March kwahiyo kwa vyovyote baba alioa mwezi April..... Compressed inner pains were too heavy to bear.... Mama mtoto marehemu akaamua kuchukua uamuzi aliochukua
Wote hawa sasa ni marehemu.... My apology kama picha zinakwaza ama kwa namna yoyote zitaleta maumivu kwa wengine
IMG-20180510-WA0008.jpg
IMG-20180510-WA0016.jpg
 
Attachments

  • IMG-20180510-WA0008.jpg
    IMG-20180510-WA0008.jpg
    23.4 KB · Views: 130
Asante kwa ujumbu mzito. Pamoja na hayo mimi ni Baba wa mabinti sina mtoto wa kiume. Hii dhana ya mimba za bahati mbaya naona inaanza kutumika vibaya.
Mapenzi ya ujanani hayana tafakuri ya matokeo na yajayo.... Na wengine hudanganywa ama kudanganyika... Dhana ya bahati mbaya ni matokeo ya kufanya kitu bila kupanga
 
Mapenzi ya ujanani hayana tafakuri ya matokeo na yajayo.... Na wengine hudanganywa ama kudanganyika... Dhana ya bahati mbaya ni matokeo ya kufanya kitu bila kupanga

Kubwa ni mvuto ulioko wa mambo ya nature linapokuja mambo ya Kujamiiana. Leo hii ukapime DNA watoto majumbani mwetu watabaki wangapi niwakwako kibaolojia?
 
Inanikumbusha dada mmoja alikuwa anatoroka usiku kwa baba yake Engineer alikuwa anakaa jirani na kanisa la Kakobe, binti alikuwa anatoroka usiku anaenda kujamiana na mlinzi wa nyumba ya jirani ambaye ni mtu mzima kuliko baba yake. Alipopata mimba babayake hakuwa na tatizo akasema kwa kuwa wanaoendana basi waoane. Yule mlinzi alikubali binti akawa hataki. Walifungishwa harusi wanaishi wote ikawa mwisho wa elimu na mwanzo wa maisha ya taabu. Hiyo ni mmoja wapo ya aina ya mimba ya bahati mbaya
 
X
Nadhani mnakumbuka kisa cha huyu binti ambaye kwa sasa ni marehemu RIP aliyejinyonga akiwa chuoni Iringa?
Huyu binti ni mmojawapo wa wahanga wa mimba za bahati mbaya? Mimba kabla ya ndoa... Lakini aliweza kuhimili kwa kupitia magumu yote mpaka kujifungua na hatimaye baada ya muda kuweza kuendelea na masomo yake ngazi ya chuo...
Kwa jinsi inavyosemwa mahusiano yaliyozaa mimba na hatimaye mtoto hayakuwa endelevu... Lakini binti akawa ana faraja kwa kuwa na mtoto mzuri wa kiume asiye na tatizo lolote....
Matendo ya Mungu si ya mwanadamu.... Mtoto yule mzuri akatwaliwa na Bwana mwezi March mwaka huu akiwa na miaka 3... Jiweke kwenye nafasi ya huyu binti... Uyaone maumivu yake... Lakini mbaya zaidi, baba mtoto kwa sababu zisizojulikana hakufika msibani wala hakuhudhuria mazishi ya mwanae... Ikawa ni maumivu juu ya maumivu kwa mama wa mtoto.... Ila akafarijiwa na kufarijika kuwa hili nalo litapita!

Ikiwa ni chini ya siku 40 tangu msiba... Likatokea lingine kubwa zaidi na lililomuongezea maumivu mama mtoto marehemu..... Mzazi mwenzie yule aliyeshindwa hata kufika kaburini kwa mwanae akaoa / akafunga ndoa na mwanamke mwingine tena kwa sherehe!
Kumbuka mtoto alifariki March kwahiyo kwa vyovyote baba alioa mwezi April..... Compressed inner pains were too heavy to bear.... Mama mtoto marehemu akaamua kuchukua uamuzi aliochukua
Wote hawa sasa ni marehemu.... My apology kama picha zinakwaza ama kwa namna yoyote zitaleta maumivu kwa wengine View attachment 772106View attachment 772117
Mapenzi ni ugonjwa!
Masikini binti hakuwa na mshauri wa kimaisha.
Ila huyo bwana kajipalia makaa ya moto.
Karma itamuwinda.
 
chanzo wanaume

ndio maana skuizi mnaanza kupokonywa madaraka ya ukuu wa nyumba (kichwa cha nyumba)
kwa ufuska wa hivi.
 
Biblia inasema moyo una mawazo. Mawazo ya moyo kama hayajapata chakula chanya ambacho ni "neno" (Neno linaweza kuwa neno la Mungu au la binadamu) hali huwa sio nzuri.

Hakuna kitu kibaya duniani kama kukata tamaa. Kukata tamaa humfanya mtu asifikiri vyema na anaweza kufanya jambo mpaka ukastaajabu.
 
Kujiua ni ujinga
We sema tu hayajakufika...pamoja na kwamba binadamu tumepewa akili kuna baadhi ya vitu huwa tunavifanya si kwa akili yetu na ndio maana kuna wataalamu wa saikolijia vile vile kuna wazee ambao kwa maeneo mengi huwa tunawatumia kama sehemu ya kutuweka sawa hasa tunavyofikwa na magumu. Ukimwona mtu kajinyonga kuna mambo mengi kichwani yamemzongonga lakini pia hajapata watu wa karibu wa kumtia moyo.

Wachache kutokana na pilikapilika za maisha huwa ndio tunaona kujinyonga sio deal (kama wewe ulivyoita ni ujinga) kutokana na ukweli kisaikolojia tulishajiandaa kubeba tatizo lolote mbele yetu

Kimsingi "anaejinyonga" na "anaeuua mtu" kisa mapenzi ama tukio lolote kimsingi wote wana sifa moja ila mmoja ni ya ujasili uliopitiliza na kufanya tukio kubwa la kufanya mauaji ila mwingine ni dhaifu kiasi kwamba ameona ana thamani ya kuishi na ndio maana anajinyonga
 
Biblia inasema moyo una mawazo. Mawazo ya moyo kama hayajapata chakula chanya ambalo ni "neno" (Neno linaweza kuwa neno la Mungu au la binadamu) hali huwa sio nzuri.

Hakuna kitu kibaya duniani kama kukata tamaa. Kukata tamaa humfanya mtu asifikiri vyema na anaweza kufanya jambo mpaka ukastaajabu.
Ni kweli mkuu
 
Back
Top Bottom