Fahamu juu ya sifa na taratibu za kuwa rubani

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Leo nitapenda tuongelee mambo machache juu ya Urubani watu wengi tumekua hatuna uelewa juu ya urubani kuhofia gharama.
Watanzania wengi hatuna uelewa tosha juu ya fani ya Urubani hii ni kutokana na kuogopa gharama kubwaa za Urubani pia na kupotoshana kwamba hatuna vigezo

Urubani ni kazi zilivyo kama kazi nyingine na inaingiza kipato kikubwa mno ikiwa ipo miongoni mwa kazi zenye kulipa vizuri na hulipa kuanzia $20,000-$40,000 per year hii inaongezeka kulingana na shirika husika

Nifanye nini niwe Rubani.....Wengi nchini kwetu tunaambizana kusoma urubani ni lazima umalize PGM high school tukizani urubani ni kama degree wakati si kweli Hakuna ulazima wa kuwa PGM ndio uwe Rubani lakini itakusaidia kuwa vizuri maana Geography itakuasaidia katika location

Kwenye urubani husomi kama Degree yaani miaka mitatu unamaliza hapana hapa tunafanya mafunzo kwa grade....

Kuna mafunzo ya awali ambapo ukihitimu unakua umepata Private Pilot Licence (PPL)
Then unapata Commercial Pilot License (CPL) hii ndio tunaowaona wanaoendesha bombardier
Key requirements to Join Flight School
Uwe na miaka walau 16yrs

Uwe umemaliza Ordinary secondary education level na uwe na ufaulu mzuri walau C 4 kwenye somo la kiingereza na physics itakusaidia

English language lazima uijue fluent maana ndiyo lugha ya mawasiliano

Uwe umepass vigezo vya aviation health examination
Uwe unaweza kulipa Ada katika flight school...
Mengineyo kama urefu weight baadhi ya vyuo wanaconsider kama ethiopia
hivyo vigezo ni kulingana na Tanzania Piloting Center
1: Private Pilot Licence (PPL);

hii ni leseni ya chini katika urubani. Ili upate leseni hii lazima uwe na masaa ya kuwa angani 40 (flying hours). Leseni hii inakuruhusu kuongoza ndege ambayo si abiria. Yaani ni wewe na familia yako na jamaa zako ndani ya ndege.

Kwa hapa Tanzania, pale airport kuna mzungu anafundisha leseni hii kwa zaidi ya mli. 35 Tsh. Nilisikia NIT walitaka kuanzisha course ya urubani sijui waliishia wapi....Kwa pale JK Nyerere Tanzania Piloting Center nilijaribu kufanya application mwaka 2018 wakanitumia hizi gharama.

2:Commrcial Pilot Licence (CPL); Hii ni leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za kukodiwa lakini si abiri.Lakini pia ukiwa na leseni unaweza kuajiliwa kwenye kampuni ya ndege kama Co-pilot wakati ukifukuzia masaa.Chuo cha Soroti flying school kinatoa mafunzo ya leseni hii kwa $62k

Hii leseni ni lazima uwe na m careasaa ya angani 200. Kwa mfano yule mzungu pale airport JNIA anatoza saa moja 200 USD. Ukiipata leseni hii unaweza ajiriwa sasa kama rubani kamili.

Gharama kamilj za hii CPL pale Tanzania Piloting Center ni kama ifuatavyo

Ground school cpl fees 2995$
Simulator cpl fees. 850$ kwa masaa 10
Practical flying hour 259$ kwa saa
Masaa ya chini ya practical 89hrs

3: Airline Transport Pilot Licence (ATPL); Hii ndo leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za abiria. Na ili upate leseni lazima uwe na masaa yasiyopungua 1000.Lakini uzuri wa leseni utafikisha hayo masaa ukiwa ni Co-pilot ilimradi upate sehemu ya kujishikisha.

Baada ya kupata hizo lesseni unaweza kuwa rubani rasmi sasa kurusha ndege tofauti tofauti.

Kunakua na Instrumental rating sasa pale unapotaka kusoma kurusha ndege aina tofauti japo basics mnakua mmefanya huko mwanzoni.
Moja ya marubani wachanga katika tasnia hii ni David Matoya....Nenda istagram utampata kwa Pilot pears...Amemaliza mafunzo yake ya urubani yaani CPL nchini Africa kusini ukiwa na maswali waweza kwenda kumuulizaa.

View attachment 1553237View attachment 1553238View attachment 1553240View attachment 1553241View attachment 1553239
IMG_20200830_155958.jpg
View attachment 1553242
 
Tuwekee na mishahara ya hao marubani kwa mashirika ya ndege tofauti tofaut
 
Kumbe namvumi king ndio yule pilot aliye hojiwa times fm ? Embu tuweke sawa kuna yule dogo mwarabu pale atcl juzi kqti kaweka rekodi karuka na msure wake ...yule na ww nani ni youngest pilot hapo bongoland. ?
 
Kwamba form 4 unaruhusiwa kujifunza urubani.
RUBANI NI DEREVA ALIYECHANGAMKA
 
Daaa, ukoo wetu sasa. Hakuna rubani hata mmoja, ngoja nimuandae mwanangu vizuri labda atakuja kuwa rubani.
 
Duhh hua sichangii sana jf.ila kiongoz thank so much .hizi mada zenye akili na kufunguana mawazo ya kutafuta pesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom