Mama Sophia Simba: Kwanza nikiri kwamba si jambo zuri kwamba katibu mkuu wangu imebidi Baraza Kuu limwondoe. Mimi binafsi siyo kitu ambacho nilitarajia, kwa sababu mimi ndiye niliyemtafuta yeye na jina lake kulipeleka kwenye vikao vya chama ili lipitishwe. Kwa hiyo, hiyo imeonyesha kwamba ni udhaifu kwa upande wangu. Nikiri kwamba sikulifanyia kazi vizuri lile jina. Pengine nilikuwa sikujiandaa vizuri.
Binadamu kufanya makosa ni kawaida, na pale nilikosea. Hata hivyo, nilijitahidi sana kufanya naye kazi vizuri. Nimekaa naye kipindi cha mwaka mmoja. Unapopewa madaraka inabidi kwanza ujifunze, kwa hiyo nilijitahidi sana kuhakikisha kwamba katibu mkuu huyu, ambaye mimi mwenyewe nilimtafuta, aweze ku-cope na ile ofisi. Lakini kukawa kuna matatizo ya Kwanza huwezi kumfananisha huyo na akina Thecla Mchauru, Kate Kamba, Dk Msimu ambao kiwango cha elimu yao kidogo ilikuwa zaidi. Hata Halima Mamuya elimu yake iko juu zaidi ya huyu. Huyu alibebeshwa mzigo ambao hakustahili, tulifanya makosa. Tulimbebesha mzito mkubwa wa kiutendaji. Pengine kisiasa kazi nyingine angeweza kuzifanya, lakini kiutendaji Kuna kazi za utendaji zina miiko yake ambayo kiwango cha elimu yake ilikuwa kidogo kina matatizo.
Raia Mwema: Sawa kulikuwa na makosa, lakini wewe ulimpataje pataje hadi akaukwaa ukatibu mkuu wa UWT? Mama Sophia Simba: Huyu alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, ndicho kitu kimoja ambacho kilinifanya nimteue. Nimekuwa naye kwenye baraza tokea mwaka 2003. Mimi nimemjua Husna wakati nikigombea ujumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo, nilipokwenda Arusha yeye ndiye aliyenisaidia kutafuta kura, siyo campaigner, lakini ndiyo nilianza kumfahamu.
Lakini nikamfahamu pia ndani ya vikao. Kwa hiyo nilimjua kwa hivyo. Na kwa bahati mbaya sana, sikujaribu kuomba ushauri kwa mtu yeyote kutaka kujua habari zake zaidi. Ndiyo maana nasema nakiri makosa. Hakuna mtu aliyenishawishi kuhusu yeye.
Hii habari imenishangaza sana...yaani Ms Simba anakiri kuwa Husna Mwilima alikuwa na udhaifu kwa kiasi hicho...yet Rais Kikwete amemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba? What does that say about President Judgement?
Correction...laizre-faire
Thanks for the thread. Mimi kama mwanamke mtanzania naomba kujua UWT inamwakilisha nani? Ilianza kama chama cha wanawake wa Tanzania, na ikawa imeimarika sana wakati wa chama kimoja. Lakini baada ya kuja multiparties, UWT imekuwa umoja wa wanawake wa CCM. Hilo limeiondolea credibility machoni mwa wanawake. As long as haikubali kuwa independent of party politics na kusimamia maslahi ya wanawake wote wa Tanzania bila kujali kama ni wana CCM au la, sioni kama kuna mtu yeyote atakayeweza kurudisha hadhi ya UWT ya zamani. Mimi binafsi siko tayari kuwa mwanachama wa UWT kabla sijajua hicho chama kinasimamia vipi maslahi yangu kama mwanamke wa kitanzania.
swali kwa Sophia Mathew Simba: Unakiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kitwana Kondo kama boyfriend.Unakiri kuwa Kitwana Kondo hakukuoa.Unakiri kuwa wakati wa mahusiano yenu,Kitwana Kondo alikua na mke wake na wewe ulilifahamu hilo.Uone kuwa ulikiuka maadili kuwa na mahusiano na mume wa mtu?huoni kuwa unapaswa kumwomba radhi mke wake kwa kuingilia ndoa yake?
{ The Son Of Africa}