Fahamu degere wanavyoweza kukutoa haraka kimaisha

Jebel

JF-Expert Member
Jul 10, 2021
306
2,041
Leo nimeona nitoe idea ambayo naamini vema kwa namna moja ama nyingine inaweza kuwasaidia waTanzania kadhaa.

WAZO: BIASHARA YA SAMAKI AINA YA DEGERE

1. Ufafanuzi

Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisheria kusafirishwa na kuuzwa. Samaki hawa huwa kwa kiasi kikubwa wananuliwa na watu ambao wanaenda kupika majumbani na kwenye migahawa.

2. Sehemu ya kufanyia biashara hii
Kwa uzoefu wangu sehemu sahihi ambayo biashara hii itaweza kukutoa haraka sana kama ukiifanyia katika jiji la Mwanza. Kuna sababu juu mbili za kupendekeza jijini Mwanza
a) Upatikanaji wa bidhaa samaki kwa urahisi na wingi
b) Soko la uhakika yaani wateja wengi kutokana na idadi ya wakazi kuwa wengi katika jiji hili.
c) Gharama ya maisha katika jiji la Mwanza ni ndogo sana kuanzia chumba cha kupanga hadi chakula.

3. Chimbo la bidhaa samaki degere
Samaki hawa unaweza kuwa unawanunua katika mialo ya pale pale Mwanza mjini, mwalo maarufu sana ni Mkuyuni kwa Mswahili, hapa ni karibu sana na njia panda ya kwenda Butimba. Changamoto ya mwalo huu au ununuzi wa samaki katika mialo hii ya mjini ni competition kubwa ya wanunuaji hasa wanawake, kama wewe siyo mzoefu lazima utakimbia na kuachana kabisa na biashara hii.
Ushauri: sehemu sahihi ya kununua samaki hawa kwa bei ya chini, bila mashindano na faida kupata kubwa sana ni kwenda kisiwani.
-Hapa napendekeza zaidi kisiwa cha Bwiro. Huku utapata samaki wengi, wazuri, bei nzuri, na utapiga faida kubwa sana ukiwafikisha Mwanza mjini.

4. Namna ya kufika na sehemu ya kulala
Kutokea Mwanza mjini hadi Bwiro nauli ni 4000-5000 tu, boat au meli. Kuna boat 3; Nyachijanja, Umia Ujae kubwa na Umia Ujae ndogo. Zinatoka Kirumba saa 4/5 asubuhi kila siku. Ni mda wa masaa3 na nusu hadi 5 kulingana na hali ya hewa ya siku hiyo. Ukifika kule guest ni kuanzia shilling 2000-4000. Kule ningeshauri ufikie guest ya Kasemele bei ya 4000 kwa mgeni ila ukishakuwa mwenyeji ni 3000. Ni guest nzuri, safi, vitanda safi 5/6 chuma, mashuka safi, maji masaa24/7. Ni pazuri sana.

5. Mtaji

Biashara hii mtu yeyote anaweza kuifanya kwani mtaji wa elfu hamsini 50,000/= unatosha kabisa kwa kuanzia na baada ya kuuza utashangaa faida utakayoipata. Samaki hawa bei yake kwa kule kisiwani ni kuanzia 1000 au pengine kama wamepatikana kwa wingi unanunu samaki 3 kwa 2000. Ukiwa na 50elfu unapata mzigo mzuri sana wa kutosha na ukishaaminika hata kama huna hela utapewa samaki na ukirudi unalipa.

6. Sehemu ya kuuzia
Kwa Mwanza mjini sehemu yoyote utakayopanga samaki hawa hasa pembezoni mwa barabara lazima samaki watanunuliwa na wataisha bila shida yoyote. Ningeshauri kwa mtu atajayekuwa interested afanye kwanza mzunguko kwa pale mjini na viunga vyake kama Nyegezi, Nyashishi, Buhongwa na maeneo mengine aone population na namna wengine wanavyouza; bei na utokaji.
Hata kama huna mtaji wa kulipia meza katika masoko ya samaki unaweza kuanza na hii ya kupanga pembezoni mwa barabara na baadaye unaweza kuanza kulipia meza kwa kuungana na wengine.

7. Faida yake

Faida mama ya samaki hawa siyo mnofu utakaouza bali ndani yake kuna “kidude” kinaitwa “bondo “. Kinakuwa kama sehemu ya utumbo lakini ni very valuable kwani hiki kidude ndicho kinachotumika kutengeneza hizi nyuzi za kushona binadamu ambazo hazitolewi bali zinayeyeka zenyewe, hasa operation ya sehemu ambazo ni sensitive.

Kumbe utagundua kwamba samaki ambaye umemununua shilling 3000 kule kisiwani unaweza kumuuza 5000 mjini Mwanza na bondo utakalotoa ukaliuza shilling 2000 au 1500 au 1000 au zaidi kutegemeana na size yake. Kwa hiyo utagundua kuwa utapiga faida sehemu mbili, kwanza kwa kumuuza samaki mwenyewe na pili kwa kuuza bondo lake. Kwa ufupi kama samaki umewanunua kisiwani ni lazima upate faida nzuri tu ukiwafikisha mjini.

JE, UMESHAWAHI KUJIULIZA NI KWANINI KILA KUKICHA WATU WANAJENGA MAJUMBA PAMOJA NA HALI KUWA NGUMU? BASI HAYA NDO MADINI YA KUSOMA ILI NAWE UFANIKIWE

8. Changamoto zake
Biashara hii kama zilivyobiashara zote nayo inachangamoto zake japo siyo kubwa sana. Changamoto ambazo nitazigusia na kutoa ushauri ni mbili;

a) Usafiri wa majini. Binafsi kilichonifanya niache kufanya biashara hii pamoja na faida yake kuwa nzuri ni baada ya familia yangu kutopenda niendelee kufanya biashara ya kusafiri majini. Binafsi natokea mkoa ambao hakuna ziwa karibu kwa hiyo wazazi na ndugu zangu walikuwa na hofu sana wanaposikia najishughulisha na biashara ya kwenda kusafiri majini mara kwa mara. Hata aliyekuwa mchumba wangu(kwa sasa mke wangu, nampenda sana) alikuwa hapendi sana mimi kwenda majini japo hakuwahi kunikataza. Ushauri, usafiri wa majini naweza kusema is more safe kuliko aina nyingine yoyote ya usafiri kuwahi kutokea. Kwa sasa kwa sababu ya maendeleo ya sayansi ya mawasiliano hata ikitokea shida yoyote msaada unafika mapema tofauti na siku za nyuma. Majini kwa sasa mtandao unasoma 3G, lakini pia kila boat kuwa kuna maboya kwa kila abiria.

b) Changamoto ya pili ni usumbufu wa maliasili kwani samaki hawa kama nilivyosema mwanzoni hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa. Hawa huwa wakiwakamata samaki na wewe usiongee vizuri, yaani ukaanza ubishi na ugalalizi basi wanaweza kuchukua na kukufirisi mzigo wote. Hakuna kifungo wala faini bali wanachukua samaki tu. Binafsi nimewahi kukamatwa sana nao lakini ni rahisi sana kuongea nao na bahati nzuri wanahitaji elfu 5 hadi elfu 10 na maisha yanaendelea. Ushauri, ukianza biashara hii, jitahidi kuwafahamu kwani mda mwingi wanakuwa kivukoni, jenga nao urafiki, wambie ukweli juu ya uchakarikaji wako, wape kidogo; biashara utafanya vizuri sana.
Changamoto hizi zote kwa mtu ambaye yupo serious kweli ameamua kuingia biasharani basi ataweza kupambana nazo vema.

Ushauri na hitimisho

Kisiwani maisha ni ya kipekee sana, kutokana na mzunguko mkubwa wa pesa hasa wakati wa giza shauri ya wanunuzi wa dagaa kutoka maeneo tofauti tofauti ya nchi kuingia kule kununua dagaa, basi mabinti nao wanatumia fursa hii vema. Kumbe inawezekana ukaenda na mtaji lakini usipokuwa makini nao unaweza kurudi kwa kuomba lift ya boat. Kuwa makini sana ukiwa kule.

Ukiwa serious sana na biashara hii, baada ya mda mfupi sana unaweza kukusanya pesa ya kutosha na ukaweza kupiga hatua kubwa sana kimaisha na baadaye UTAKUJA kunishukuru.
 
Ubarikiwe sana mkuu
Ila samahan kwani hauna mpango wa kurejea kabisa kujiendeleza na hiyo biashara mkuu licha ya changamoto zake?
 
Kwa sasa nimetoka kidogo nchini Tanzania, labda naweza kufanya nikirudi lakini katika scale kubwa kidogo.
 
Aaahh sawa kabisa mkuu

Nimevutiwa nayo nikadhan labla kwa muda huu umeiboresha kwanzia upatikanaji wake mpka kufikia wateja

Mungu akusimamie urudi tena kwenye huo mradi
 
Naomba kujua yafuatayo 1,samaki unakausha hukohuko kisiwani au unabeba wabichi hadi mwanza mjini? 2,mabondo unauzia wapi? 3,je kuna wanunuzi wa jumla ikiwa mtu anataka kununua kisiwani bwiro na kuuza jumla mwanza mjini?naomba majibu ahsante mkuu
 
Ndugu,

-Kwa wepesi wa usafirishaji na unafuu wa gharama za ukaushaji ni vema ukawakausha huko huko kisiwani kisha ukaleta wakavu Mwanza.

-Ukifika tu kivukoni wanunuzi wa jumla wapo wengi sana, samaki ni chakula tena chakula pendwa kwa hiyo soko lake ni la uhakika.

-Mabondo yanatafutwa kama dhahabu au almasi inavyotafutwa, soko lake ni la uhakika japo bei huwa inabadilikabadilika kutoka kipindi hadi kipindi.

Natumaini nimejibu maswali yako.
 
Leo nimeona nitoe idea ambayo naamini vema kwa namna moja ama nyingine inaweza kuwasaidia waTanzania kadhaa.

WAZO: BIASHARA YA SAMAKI AINA YA DEGERE.

1. Ufafanuzi.

Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisheria kusafirishwa na kuuzwa. Samaki hawa huwa kwa kiasi kikubwa wananuliwa na watu ambao wanaenda kupika majumbani na kwenye migahawa.

2. Sehemu ya kufanyia biashara hii.

Kwa uzoefu wangu sehemu sahihi ambayo biashara hii itaweza kukutoa haraka sana kama ukiifanyia katika jiji la Mwanza. Kuna sababu juu mbili za kupendekeza jijini Mwanza
a) Upatikanaji wa bidhaa samaki kwa urahisi na wingi
b) Soko la uhakika yaani wateja wengi kutokana na idadi ya wakazi kuwa wengi katika jiji hili.
c) Gharama ya maisha katika jiji la Mwanza ni ndogo sana kuanzia chumba cha kupanga hadi chakula.

3. Chimbo la bidhaa samaki degere.

Samaki hawa unaweza kuwa unawanunua katika mialo ya pale pale Mwanza mjini, mwalo maarufu sana ni Mkuyuni kwa Mswahili, hapa ni karibu sana na njia panda ya kwenda Butimba. Changamoto ya mwalo huu au ununuzi wa samaki katika mialo hii ya mjini ni competition kubwa ya wanunuaji hasa wanawake, kama wewe siyo mzoefu lazima utakimbia na kuachana kabisa na biashara hii.
Ushauri: sehemu sahihi ya kununua samaki hawa kwa bei ya chini, bila mashindano na faida kupata kubwa sana ni kwenda kisiwani.
-Hapa napendekeza zaidi kisiwa cha Bwiro. Huku utapata samaki wengi, wazuri, bei nzuri, na utapiga faida kubwa sana ukiwafikisha Mwanza mjini.

4. Namna ya kufika na sehemu ya kulala.

Kutokea Mwanza mjini hadi Bwiro nauli ni 4000-5000 tu, boat au meli. Kuna boat 3; Nyachijanja, Umia Ujae kubwa na Umia Ujae ndogo. Zinatoka Kirumba saa 4/5 asubuhi kila siku. Ni mda wa masaa3 na nusu hadi 5 kulingana na hali ya hewa ya siku hiyo. Ukifika kule guest ni kuanzia shilling 2000-4000. Kule ningeshauri ufikie guest ya Kasemele bei ya 4000 kwa mgeni ila ukishakuwa mwenyeji ni 3000. Ni guest nzuri, safi, vitanda safi 5/6 chuma, mashuka safi, maji masaa24/7. Ni pazuri sana.

5. Mtaji

Biashara hii mtu yeyote anaweza kuifanya kwani mtaji wa elfu hamsini 50,000/= unatosha kabisa kwa kuanzia na baada ya kuuza utashangaa faida utakayoipata. Samaki hawa bei yake kwa kule kisiwani ni kuanzia 1000 au pengine kama wamepatikana kwa wingi unanunu samaki 3 kwa 2000. Ukiwa na 50elfu unapata mzigo mzuri sana wa kutosha na ukishaaminika hata kama huna hela utapewa samaki na ukirudi unalipa.

6. Sehemu ya kuuzia

Kwa Mwanza mjini sehemu yoyote utakayopanga samaki hawa hasa pembezoni mwa barabara lazima samaki watanunuliwa na wataisha bila shida yoyote. Ningeshauri kwa mtu atajayekuwa interested afanye kwanza mzunguko kwa pale mjini na viunga vyake kama Nyegezi, Nyashishi, Buhongwa na maeneo mengine aone population na namna wengine wanavyouza; bei na utokaji.
Hata kama huna mtaji wa kulipia meza katika masoko ya samaki unaweza kuanza na hii ya kupanga pembezoni mwa barabara na baadaye unaweza kuanza kulipia meza kwa kuungana na wengine.

7. Faida yake.
Faida mama ya samaki hawa siyo mnofu utakaouza bali ndani yake kuna “kidude” kinaitwa “bondo “. Kinakuwa kama sehemu ya utumbo lakini ni very valuable kwani hiki kidude ndicho kinachotumika kutengeneza hizi nyuzi za kushona binadamu ambazo hazitolewi bali zinayeyeka zenyewe, hasa operation ya sehemu ambazo ni sensitive.
Kumbe utagundua kwamba samaki ambaye umemununua shilling 3000 kule kisiwani unaweza kumuuza 5000 mjini Mwanza na bondo utakalotoa ukaliuza shilling 2000 au 1500 au 1000 au zaidi kutegemeana na size yake. Kwa hiyo utagundua kuwa utapiga faida sehemu mbili, kwanza kwa kumuuza samaki mwenyewe na pili kwa kuuza bondo lake. Kwa ufupi kama samaki umewanunua kisiwani ni lazima upate faida nzuri tu ukiwafikisha mjini.

JE UMESHAWAHI KUJIULIZA NI KWANINI KILA KUKICHA WATU WANAJENGA MAJUMBA PAMOJA NA HALI KUWA NGUMU? BASI HAYA NDO MADINI YA KUSOMA ILI NAWE UFANIKIWE.

8. Changamoto zake
Biashara hii kama zilivyobiashara zote nayo inachangamoto zake japo siyo kubwa sana. Changamoto ambazo nitazigusia na kutoa ushauri ni mbili;

a) Usafiri wa majini. Binafsi kilichonifanya niache kufanya biashara hii pamoja na faida yake kuwa nzuri ni baada ya familia yangu kutopenda niendelee kufanya biashara ya kusafiri majini. Binafsi natokea mkoa ambao hakuna ziwa karibu kwa hiyo wazazi na ndugu zangu walikuwa na hofu sana wanaposikia najishughulisha na biashara ya kwenda kusafiri majini mara kwa mara. Hata aliyekuwa mchumba wangu(kwa sasa mke wangu…nampenda sana) alikuwa hapendi sana mimi kwenda majini japo hakuwahi kunikataza. Ushauri, usafiri wa majini naweza kusema is more safe kuliko aina nyingine yoyote ya usafiri kuwahi kutokea. Kwa sasa kwa sababu ya maendeleo ya sayansi ya mawasiliano hata ikitokea shida yoyote msaada unafika mapema tofauti na siku za nyuma. Majini kwa sasa mtandao unasoma 3G, lakini pia kila boat kuwa kuna maboya kwa kila abiria.

b) Changamoto ya pili ni usumbufu wa maliasili kwani samaki hawa kama nilivyosema mwanzoni hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa. Hawa huwa wakiwakamata samaki na wewe usiongee vizuri, yaani ukaanza ubishi na ugalalizi basi wanaweza kuchukua na kukufirisi mzigo wote. Hakuna kifungo wala faini bali wanachukua samaki tu. Binafsi nimewahi kukamatwa sana nao lakini ni rahisi sana kuongea nao na bahati nzuri wanahitaji elfu 5 hadi elfu 10 na maisha yanaendelea. Ushauri, ukianza biashara hii, jitahidi kuwafahamu kwani mda mwingi wanakuwa kivukoni, jenga nao urafiki, wambie ukweli juu ya uchakarikaji wako, wape kidogo; biashara utafanya vizuri sana.
Changamoto hizi zote kwa mtu ambaye yupo serious kweli ameamua kuingia biasharani basi ataweza kupambana nazo vema.

Ushauri na hitimisho.
Kisiwani maisha ni ya kipekee sana, kutokana na mzunguko mkubwa wa pesa hasa wakati wa giza shauri ya wanunuzi wa dagaa kutoka maeneo tofauti tofauti ya nchi kuingia kule kununua dagaa, basi mabinti nao wanatumia fursa hii vema. Kumbe inawezekana ukaenda na mtaji lakini usipokuwa makini nao unaweza kurudi kwa kuomba lift ya boat. Kuwa makini sana ukiwa kule.

Ukiwa serious sana na biashara hii, baada ya mda mfupi sana unaweza kukusanya pesa ya kutosha na ukaweza kupiga hatua kubwa sana kimaisha na baadaye UTAKUJA kunishukuru.
Kwahiyo mkuu, cha kuzingatia ni bei wakati wa kununua?, na vipi kuhusu wauzaji, unanunua direct Kwa Wavuvi au kuna utaratib mwingine??
 
Ndugu,

-Kwa wepesi wa usafirishaji na unafuu wa gharama za ukaushaji ni vema ukawakausha huko huko kisiwani kisha ukaleta wakavu Mwanza.

-Ukifika tu kivukoni wanunuzi wa jumla wapo wengi sana, samaki ni chakula tena chakula pendwa kwa hiyo soko lake ni la uhakika.

-Mabondo yanatafutwa kama dhahabu au almasi inavyotafutwa, soko lake ni la uhakika japo bei huwa inabadilikabadilika kutoka kipindi hadi kipindi.

Natumaini nimejibu maswali yako.
ahsante sana,nimekupata mkuu,ubarikiwe kwa kusambaza mbinu na maarifa bila ubinafsi.
 
Shukran Kwa mwongozo mkuu, na vipi kuhusu vipindi vya Hali ya hewa hasa kipindi cha mvua, je ni miezi gani huwa biashara inakua vizuri sana, au haijalishi msimu?
 
Back
Top Bottom