SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,901
Duh...sasa wenye majina mengi kazi tunayo!
Jina la kuzaliwa (la kilugha) naitwa Samulakai. Wakati naanza shule miaka hiyo walimu walioniandikisha wakaniita Samu Makai. Hiyo Makai sio jina la ukoo, ni la baba. Nimeenda kanisani wakanipa jina la kizungu....Salutaris. Nilivyoomba passport wakataka majina matatu....nikaandika Samu Makai Magori. Magori ni jina la ukoo lakini halimo kwenye vyeti vyangu vya shule. Nimefunga ndoa ya kikristo, cheti kikaandikwa Salutaris Samu Magori.
Mtaani hapa wananiita Baba Silke. Silke ni jina la mwanangu. Kazini wananiita Makai. Nikienda kijijini wananiita Samulakai. Kanisani wananiita Salu au Salutaris. Nikienda kwa mzee wangu hupenda kuniita Samu. Na hapa JF mnaniita SMU.
Sasa hapo 'namechisha" vipi majina?