Fahamu aina mbalimbali za magari

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
Kwa muda mrefu nimekuwa nikipitia katika jukwaa hili kama msomaji ila changamoto nilioiona wengi wamekuwa hawafahamu aina mbalimbali za model za mgari, mfano nimeona kuna uzi unauliza tofauti ya alphard V na G, ningependa kuchukua nafasi hii kunza na hii model ya alphard kutoka katika kampuni ya toyota.

Nitajaribu kugusia sehemu mbalimbali za hizi gari ingawa si katika mpagilio sana maana mimi si muandishi mzuri

Toyota alphard ni gari zilizoanza kutengenezwa mwaka 2002 kama MPV (Mini Passenger Vehicle) hasa kwa soko la ndani (Japan). Mpaka sasa kuna vizazi vitatu vya toyota alphard, kizazi cha kwanza kilianzia 2002-2007, cha pili 2008-2014 na cha tatu ni 2014 na kuendelea

al.jpeg
first generation

alph.jpeg
second G

alp.jpeg
3 generation

Tukianza na first generation
Kwa ufupi hapa palikuwa na model 3 ambazo ni ambazo ni alphard V, alphard G na alphard hybrid.

Jinsi ya kugundua Alphard imetengenezwa lini
Mara nyingi gari tunazonunua huwa zimekwisha tumika hivyo katika kujiridhisha ni vizuri ukajua hii gari ilitengenezwa lini, kwa upande wa toyota alphard utafanya kama ifuatavyo

1. Angalia chassis namba ya gari ili kujihakikishia mwaka ulioandikwa ndio huo muuzaji anausema? Kama alphard yako ni pre face lifted (PFL) fungua boneti na kopi chesesi namba za zilizopo upande wa kushoto baada ya kufungua boneti PreFaceliftNumber.jpg

Na kama alphard yako ni face lifted(FL) imeandikwa nyuma ya injini hivyo toa plastic lililoziba utazikuta
BulkheadChassisNoCover.jpg

Baada ya hapo ingiza hizo chesisi namba Check Manufacture Year - Japan Partner itakutajia hiyo alphard ilitengenezwa mwaka gani hii ni njia ya kwanza ya kugundua alphard yako imetengenezwa lini.

2. Njia ya pili angalia lebo iliopo kwenye siti belt ingawa wauzaji wengi hukata hii lebo.

SeatBeltLabel.jpg

3. Kama ukikuta alphard yako lebo wametoa nenda kwenye mfuniko wa tool box uliopo upande wa kushoto mwa buti hapo kuna plastic la mfuniko ligeuze nyuma utaona kuna tebo inavidoti doti mstari wa kushoto uliosimama unaonyesha mwaka wakati mstari wa juu uliolala unaonyesha miezi wakati kidoti katikati ya tebo kitakuonyesha wiki hivyo kwa kuunganisha hivyo vitu vitatu utaweza jua gari lako limetengenezwa mwaka gani mwezi gani na wiki ya ngapi mfano hapo kwenye picha gari imetengenezwa wiki ya kwanza july 2005 hizi siri za magari hata wauzaji wengi huwa hawazijui nilichogundua.

ToolboxCoverLocation.jpg

YearManufacture.jpg

Tofauti kati ya alphard Pre face lifted(PFL) and New Face lifted
kama nilivyosema alphard zilianza kutengenezwa 2002 lakini kufikia may 2005 kuna mabadiliko kidogo yalifanyika katika bodi kama ifuatavyo

Kwa nje kulikuwa na mabadiliko katika headlight cluster kwa taa za mbele na nyuma alphard zilizotengenezwa baada ya may 2005 katika taa za mbele kwa pembeni kuna vinundu viwili wakati za awali zilikuwa na kinundu kimoja pia mpya zikawa na taa nyeupe yote wakati za awali zilikuwa na kinundu cha orange kutokana na size ya taa kuwa tofauti hivyo hata front grill zilitofautiana ingawa kwa mocho huwezi gundua ila ukiwa makini utaona new face lift(NFL) grill ya juu ni kubwa kuliko ya PFL model kama katika hiyo picha ya upande wa kushoto utofauti mwingine upo katika taa za nyuma za indiketa alphard za awali zilikuwa na mstari mmoja wa indiketa wakati zilizofanyiwa maboresho zilikuwa na mistari miwili tofauti nyingine ni kwenye taa za kurudi nyuma PFL(left photo) ilikuwa na taa ndogo wakati NFL ikawekwa taa kubwa zenye distinct light elements

FrontLightClusterSBS.jpg FrontLightClusterSV.jpg FrontGrilleSBS.jpg RearLightClusterSBS.jpg ReverseLightSBS.jpg

NDANI
Kwa ndani kitu kikubwa kilichobadilishwa ni head uni, NFL iliwekewa head unit kubwa (picha ya kushoto) yenye 8-inch wakati za awali zilikuwa na head unit ndogo

HUSBS.jpg


Jinsi ya kujua kama alphard ni 2WD au 4WD
K
wakuangalia kwa nje huwezi kutambua kama ni 2WD au 4WD labda kama hutojali chungulia chini utaona shaft imeenda tairi za nyuma na diff, njia nyingine ni kwakuangaria odel code na hapa huwa tunaangaria the first 5 alphanumeric ya model code ndio itakayotueleza kama gari ni 2WD au 4WD nazani itakuwa rahisi kama nitaweka katebo kuonyesha utofauti.

model codeengine codegradetrasmission
MNH 10W1MZ-FE (3.0L gasoline)MZ/MS/MXFront Wheel

Drive
ANH 10W2AZ-FE (2.4L gasoline)AS/AX
Front Wheel

Drive
MNH 15W1MZ-FE (3.0L gasoline)MZ/MS/MXFour Wheel

Drive
ANH 15W2AZ-FE (2.4L gasolineAS/AX
Four Wheel
Drive

Kwa alphard hizi model code zipo kwenye chassis plate kwa toleo la kwanza kabla ya kuinuliwa juu (pre face lifted) huandikwa upande wa kushoto baada ya kufungua boneti na kwa (face lifted model) huandikwa kwenye mlango wa mbele wa abiria. kwakuangaria hiyo tebo kama model code ni 10 basi hoyo ni 2WD na kama ni 15 basi ni 4WD

Kamera katika toyota alphard
miongni mwa vitu muhimu katika toyota alphard ni kamera maana kuendesha gari kubwa kama alphard hasa linapokuja swala la parking lingesumbua sana lakini kwa alphard kilikuwa solved before maana kupitia camera zilizopo mbele na nyuma yagari dereva ataweza ona kilichopo mbele na nyuma ya gari moja kwa moja kupitia head unity.
kamera ya mbele imewekwa chini ya grill ya mbele

FrontCamera.jpg

Hapa pia itategemea na mwaka wa kutengenezwa kuna zenye kamera ya pande mbili hivyo dereva ataweza kuona kushoto na kulia mwa gari lake na kuna zenye kamera tatu hivyo dereva ataweza ona kushoto, kulia na mbele mwa gari lake kamera mbili view

FrontCamera2View.jpg

kamera 3 view

FrontCamera3View.jpg
kwa kawaida kamera ya mbele huwa inawaka pale unapowasha tu gari ila unaweza izima kwa kupitia kitufe kilichopo kwenye mskanio(stering)

FrontCameraButton.jpg

Pia katika alphard zilizotengenezwa baada ya may 2005 kuna button ya kuchagua camera ionyeshe pande mbili au tatu

FrontCameraSwitchView.jpg

Kamera ya nyuma imewekwa kwenye mlango wa buti juu ya plate namba, hii huwa outomatic pole unapoweka gia ya kurudi nyuma pia itakuchorea pembe nne ya rangi ya njano ambayo ni maximum ya gari kurudi nyuma na pembenne nyekundu ambayo ni extream position kama kwenye picha

RearCameraLineStraight.jpg

Pale utakapoanza kukata kona ile langi ya njano itaanza elekea kule stering inapo elekea wakati mstari wa kijani utabaki ukionyesha uelekeo halisi wa gari
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
nilipata changamoto ya kufanya attachment kwani jamii forum mwisho 20 attachiments hivyo tunaendeleaRearCameraLineTurn.jpg
kutokana na hiyo picha mstari wa njano wa katika ni kama 1m kutoka kwenye bampa la gari wakati mstari mwekundu ni 0.5m na huo mweupe ni bampa.
pia katika kumpa dereva uhuru wa kuendesha alphard iliongezewa na sonar sensor hivyo zitasensi kama kuna kitu kinalikaribia gari na itakuonyesha upende kilipo hicho kitu ila hii option haipo kwa alphard zote hivyo itabidi mnunuaji uwe makini SonarSensorView.jpg katika hicho kipicha cha kijani kina nucta nne hivyo kama kunakitu kinakaribia kugonga gari upande fulani kinucta cha upande huo kitaanza kuwa taa nyekundu na kubip huku picha kwenye head unit ikikuonyesha kinachokaribia gari na kama utaendelea kukisogerea zaidi hicho kinucta kinaongeza speed ya kuwaka.

Buttons ndani ya toyota alphard
Kwa upande wa kulia mwa stering kuna button tano kama ifuatavyo RightButtonsNum.jpg
1. AC 100V SWITCH-utakapo bonyeza hii switch utaweza kuwasha sehemu ya kuchomekea yenye uwezo wa kutoa 100v hivyo utaweza kuchomeka hivi vitu vinavyotumia huu umeme wa kawaida ndani ya gari mfano chaja ya simu ya kawaida na vingine
2. AFS OFF SWITCH- kwa alphard zenye AFS HID light kwa kubonyeza hii button utakuwa umezima
3. LEFT DOOR SWITCH-kwa kubonyeza hapa utaweza kufungua na kufunga mlango wa kushoto
4. RIGHT DOOR SWITCH- kwa kubonyeza hapa utaweza kufungua na kufunga mlango wa kulia
5. Rear fog lamp switch-kwa model zenye fog lamp hii button itawasha na kuzima
LeftButtonsNum.jpg
kwa upande wa kushoto chini ya stering kuna hizi buttons
1. POWER DOOR SWITCH- utakapobonyeza hii button milango ya nyuma haita funguka tena automatiki
2. Power boot switch- utakapobonyeza hii button itafungua na kufunga boot la nyuma kwa wenye alphard zenye hii options
3. H-TEMS Switch-hii button itakuwezesha kuswitch shock absobers katika moja ya model 3 sport model, comfort na nomal kutegemea na uendeshaji unaoutaka.
4. Lane monitoring switch- hii botton itakuwezesha kucontrol mistari ya barabara kati ya ule wa katikati na ule wa njano wa pembeni hivyo utakapotaka kutoka ama kwa kusinzia gari itakukumbusha kwa alarm kuwa unaenda either nje ya barabara au upande wa mwenzio
5. TRC switch off-utakapo bonyeza hii button utakuwa umeweka traction control off hii option sio kwa alphard zote

Button zilizopo katikati ya seat ya dereva na abiria
CenterConsole.PNG
1. Passenger seat heater switch-hii button itawasha heater zilizopo chini ya seat a abiria ila hii haijawekwa kwenye model zote za alphard hasa ipo kwenye model ya MZG
2.Driver eat heater switch-hii itawasha na kuzima heater iliopo chini ya siti ya dereva
3.back door curtain switch- hii itafungua na kufunga pazia za zilizopo kioo cha nyuma
4. side curtain switch- hii itafungua na kufunga pazia za pembeni
5. rear sun roof switch-hii button itafungua na kufunga dirisha la juu.

TOFAUTI KATI YA ALPHARD G NA ALPHARD V
Moja kati ya swali ambalo huu lizwa na wanunuaji wengi wa toyota alphard ni tofauti kati ya alphard G na alphard V
haya ni maneno yaliopo kwenye upande wa nyuma wa kuria wa gari
1.Utofauti kati ya hizi gari mbili unaanzia kwa supplier hawa ni TOYOPET na NETZ. Toyopet ambao ni bussiness unit ya toyota hawa walisapply alphard G wakati Netz hawa walisupply alphard V na hii ni kwa first generation only hawa ni madiller wakubwa huku japan ambao wao ununua mzigo mkubwa na kuuza kwa end user hivyo ndio maana muda mwingine gari unanunua unakuta kuna sticker imeandikwa yokohama toyopet inamaana huyu ni agent wa toyopet alieko yokohama na wapo wengi mfanoKamig.jpg
Tulipoingia kwenye second generation toyopet waliendelea na alphard wakati Netz waliamua kuachana na alphard na wakaja na model yao wakaiita toyota VERFIRE hivyo kuanzia second generation kukawa hakuna tena alphard G na V ila tukawa na alphard agaist verfire
2. Tofauti ya pili ni kwenye grill za mbeleGvsVGrillePFL.jpg alphard G ukiangaria grill za mbele zina full chrome hiyo ya kushoto kwenye picha na ina mistari miwili ya ulalo katikati na logo ya alphard ipo katikati ya mstari wa kwanza na utaona kwa ndani kuna mistari mingi iliosimama. kutokana na hiyo picha G ni kushoto naV kuria
Alphard V ina mstari wa juu wa grill ni chrome inayofuta itakuwa na rangi ya gari na ina grill yenye mistari minne katikati na logo ya alphard inabebwa na mistari miwili ya juu na hii ni zilizotengenezwa kabla ya may 2005
Kwa zilizotengenezwa zaidi ya may 2005 zitakuwa hiviGvsVGrilleNFL.jpgkuna mabadiliko kidogo alpgard G ikawekwa na mistari mitatu ya horizontal wakati V ikawekwa mistari miwiwi ya horizontal kwenye grill na logo kwa zote mbili zikashikwa na line mbili za juu. na alphard V ikawekewa mistari 5 ya kusimama. kutokaka na picha still alphard G kushoto na V kuria
Nadhani nitakuwa nimemjibu alietaka kujua tofauti ya alphard V na G.
GRADE ZA TOYOTA ALPHARD
kama unahitaji kununua toyota alphard ni vizuri ukafaham grade unayotaka kuuziwa, kwa first generation kwa kuangalia kwa nje kuna grade tatu ambazo ni X model/S na Hybrid
katika model ya X kuna AX na kuna MX hizi herufi za mwanzo zinawakilisha ukubwa wa engine kwamba A ikimaanisha 2.4l wakati M ni 3.0l.utaigundua kama hii ni alphard X kwa kuangalia bampa la mbele na shape ya fog light, fog light ya toyota alphard X ni za pembe nneToyota_Alphard_MZMXAX.jpg
Wakati alphard S wakimaanisha sport yenyewe itakuwa na fog light za duara na hata ndani itakuwa ni tofauti na X model kuanzia rangi hadi instrument mfano X haina cruise control wakati S ina cruise controlToyota_Alphard_MSAS.jpg
Na model ya tatu ni hybrid ambapo hii huwa tofauti katika front grill ingawa hybrid zote zinakuja na 2.4lToyota_Alphard_Hybrid.jpg


Mpangililio wa seat katika toyota alphard
1.A
lphard ni gari yenye mpangilio wa siti naweza nikasema nyingi zaidi ya gari nyingine, tukianza na standard ambao watu wote hugeukia mbelePushToEnd.jpg
2.Mpangilio wa pili ni ule ambao third rowseats hujikunja na kupanda juu hivyo kutoa nafasi kwa kupakia mzigo katika nafisi iliokuwa imechukuliwa na siti za mstari wa tatuimages.jpeg
jinsi ya kupandisha third row seat kwenye toyota alphard
-Hatua ya kwanza tafuta alama kama itakavyoonekana kwenye bodi ya gari mbele ya siti za mstari wa tatu, kwani seat itakapokuwa hapa ndio itaweza chomoka kwenye reli yake.SeatMarker.jpg
-Hatua ya pili vuta kishikizo kilicho pembeni mwa seat ili kuifanya seat ilaleLeverToRelease.jpg
baada ya seats kulala zitakuwa na muonekano huuMisc-Jun2010 003.JPG
-baada ya hapo vuta kichuma kinacho zifunga seat chiniPullRailLock.jpg
seats zitatoka kwenye reli na ziinue kwenda juu moja baada ya nyingine
-Kilaze kiplastiki kilichokuwa kinashikilia seats na mwisho hapo utaona kuna mkanda ambao utaisapoti seat kukaa juu kwa kuukoleka kwenye kishikizi kilichopo hapo juu SeatHooked.jpg
3. Mkao wa tatu ni huu ambao mambao setas za kati zitageuka nyuma na kufanya abiria wa seat za mstari wa tatu na wa katikati watakuwa wanatazamanaLargeSpaceBetweenSeats.JPG
4. mkao mwingine ni ule ambao utatoa viegemeo vya seat za mbele na kati na kulaza seat zote na kugeuka kama kitandaAllFlats.JPG
5 mkao mwingine ni ule ambao seats za kati hulala na kugeuka kama meza kwa seats za mstari wa tau

Langi za toyota alphard
2002-2005 model


Kiufupi kunavitu vingi vya kuangaria kabla haujanunua toyota alphard kwani zinatofautiana sana mfano hata X kuna AX hii ni standard model hata milango ya abiria haifunguki kwa button wakati AXL wakimaanisha L luxary milango inafungukakwa button na imewekewa hadi air purifire hivyo hata mtu akichafua hewa unawasha purifire inasafisha hewa NITAENDELEA NIKIPATA MUDA KWA ALPHARD NA MODEL NYINGINE INGAWA NAGUSA JUU JUU
 

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
34,168
Points
2,000

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
34,168 2,000
Wauzaji wa magari bongo wahuni sana. Wanazileta wanaharibu mikanda. Wanashusha mileage etc.
Ila hii gari inafaa sana ukinunua inatosha kabisa
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
Wauzaji wa magari bongo wahuni sana. Wanazileta wanaharibu mikanda. Wanashusha mileage etc.
Ila hii gari inafaa sana ukinunua inatosha kabisa
Nikipata muda nitawawekea site ya kujua gari unayonunua huku japani kwenye auction iliuzwa na mileage kiasi gani
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
Rangi za toyota alphar2002-2005
ColourChart200402.JPGk
wa kuanzia juu kushoto kwenda mstari wa chini kulia :white mica,silver metallic,black mica,bordeux mica(maroon), gold metallic,light green mica metallic,dark blue mica, gray pearl toning hizo ndio rangi za alphard kutokana miaka tajwa hapo juu nje ya hapo imerudiwa rangi
2005-2007
ColourChart200504.JPGkuanzia juu kwenda chini: white mica, gray metallic,silver metallic, black mica,maroon,gold metallic,dark blue mica nje ya hapo imerudiwa rangi
Jinsi ya watu wa seat ya tatu kusogeza seats wanapotaka kushuka
FootLever4MiddleSeat.jpg
watakanyaga hicho kichuma kilichopo seat za kati na kusukuma seat mbele
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
Kwani sisi hatuwezi nunua magari mnadani moja kwa moja?
Inawezeka na kuna website zinatangaza magari moja kwa moja tokea yakiwa mnadani sema sheria hairuhusu wewe kama wewe kwenda mnadani hivyo only registered persons allowed mfano wa web http://auction.pacificcoastjdm.com/manager?p=project/registered tena mnadani ni vizuri maana hadi auction sheet unaiona hivyo kama gari iliwahi pata ajali utaiona kama mileage imefojiwa wataandika ingawa hii auction sheet inahitaji utaalam wa kuitafsiri. Na ukitaka kujua kwa madiller kuna janja janja agiza gari na mwambie akuonyeshe auction sheet kama atatoa
 

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Messages
1,035
Points
2,000

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2018
1,035 2,000
Inawezeka na kuna website zinatangaza magari moja kwa moja tokea yakiwa mnadani sema sheria hairuhusu wewe kama wewe kwenda mnadani hivyo only registered persons allowed mfano wa web http://auction.pacificcoastjdm.com/manager?p=project/registered tena mnadani ni vizuri maana hadi auction sheet unaiona hivyo kama gari iliwahi pata ajali utaiona kama mileage imefojiwa wataandika ingawa hii auction sheet inahitaji utaalam wa kuitafsiri. Na ukitaka kujua kwa madiller kuna janja janja agiza gari na mwambie akuonyeshe auction sheet kama atatoa
Mkuu kwenye minada kuna kuwa na Boat ndogo au Jet ski. Na mtu akihitaji gharama zake zinakuwa vipi kuagiza mpaka Tanzania
 

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Messages
8,248
Points
2,000

Wick

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2012
8,248 2,000
"Fahamu aina mbalimbali za magari" halafu ndani umeiongelea Toyota Alphard mwanzo mwisho!. sikukosoi lakini hiyo sio aina mbalimbali za magari.
Aina mbalimbali za magari ni kama:
1. Saloon/Sedan
2. Hatchback
3. Coupe
4. Multi Purpose Vehicle (MPV) Alphard ipo kundi hili.
5. Sport utility Vehicle (SUV)
6.CrossOver Utility Vehicle (CUV)
7. Trucks
8. Pick-Ups
Kuna aina mpya Mercedes kaileta inaitwa Sport Utility Limousine (SUL) ni Mercedes Maybach: Ultimate Luxury. Hizi ndio baadhi ya aina za magari!.
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
"Fahamu aina mbalimbali za magari" halafu ndani umeiongelea Toyota Alphard mwanzo mwisho!. sikukosoi lakini hiyo sio aina mbalimbali za magari.
Aina mbalimbali za magari ni kama:
1. Saloon/Sedan
2. Hatchback
3. Coupe
4. Multi Purpose Vehicle (MPV) Alphard ipo kundi hili.
5. Sport utility Vehicle (SUV)
6.CrossOver Utility Vehicle (CUV)
7. Trucks
8. Pick-Ups
Kuna aina mpya Mercedes kaileta inaitwa Sport Utility Limousine (SUL) ni Mercedes Maybach: Ultimate Luxury. Hizi ndio baadhi ya aina za magari!.
Sasa mkuu hayo yote ukiyaongelea kwa Mara moja utakuwa huna cha kufanya? Pili lengo nilianza na alieuliza tofauti ya alphard V na G ndio kilikuwa kifaumbele changu, tatu kwani kuna sehemu nimeandika kwamba ndio nimemaliza?
 

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Messages
392
Points
500

analgesic

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2013
392 500
Hi
"Fahamu aina mbalimbali za magari" halafu ndani umeiongelea Toyota Alphard mwanzo mwisho!. sikukosoi lakini hiyo sio aina mbalimbali za magari.
Aina mbalimbali za magari ni kama:
1. Saloon/Sedan
2. Hatchback
3. Coupe
4. Multi Purpose Vehicle (MPV) Alphard ipo kundi hili.
5. Sport utility Vehicle (SUV)
6.CrossOver Utility Vehicle (CUV)
7. Trucks
8. Pick-Ups
Kuna aina mpya Mercedes kaileta inaitwa Sport Utility Limousine (SUL) ni Mercedes Maybach: Ultimate Luxury. Hizi ndio baadhi ya aina za magari!.
Pia gari kama hiyo Benz unadhani ni lini itaonekana tandale? Ni sawa na niongelee jinsi soyuz inavyofanya docking ni wangapi wataelewa?
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
3,094
Points
2,000

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
3,094 2,000
Sasa mkuu hayo yote ukiyaongelea kwa Mara moja utakuwa huna cha kufanya? Pili lengo nilianza na alieuliza tofauti ya alphard V na G ndio kilikuwa kifaumbele changu, tatu kwani kuna sehemu nimeandika kwamba ndio nimemaliza?
Mkuu Kwa niaba yetu tunaomba umsamehe Tu maana hajui analofanya
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
3,094
Points
2,000

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
3,094 2,000
Inawezeka na kuna website zinatangaza magari moja kwa moja tokea yakiwa mnadani sema sheria hairuhusu wewe kama wewe kwenda mnadani hivyo only registered persons allowed mfano wa web http://auction.pacificcoastjdm.com/manager?p=project/registered tena mnadani ni vizuri maana hadi auction sheet unaiona hivyo kama gari iliwahi pata ajali utaiona kama mileage imefojiwa wataandika ingawa hii auction sheet inahitaji utaalam wa kuitafsiri. Na ukitaka kujua kwa madiller kuna janja janja agiza gari na mwambie akuonyeshe auction sheet kama atatoa
Ukiingia Kwenye site za (be forward,tradeview car,any na nyinginezo) utaona maelezo mengi kuhusu gari husika kuanzia manufacturer year, chassis number, engine code number, registration number e.tc
Je hawa wauzaji pia huwa wanadanganya kwa wateja wao?
 

Forum statistics

Threads 1,365,128
Members 521,108
Posts 33,337,376
Top