Fadlu badilika ama ubadilishwe

Fadlu badilika ama ubadilishwe

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,163
Reaction score
48,436
Umejawa hofu ya kufungwa kiasi ni kama unazuia wachezaji kuchakarika.

Imani yako kwa Mohamed Hussein, Fabrice Ngoma inaigharimu Timu.

Kibu D ana maguvu Lakini achezi kitimu. Umeshindwa kumuelekeza kuwa akicheza kitimu Simba itafaidika zaidi?

Ahoua anajua kucheza mpira Lakini hachezi kimpira. Afunzwe kuwa kipaji chake kinatakiwa kiinufaishe Timu . Asicheze kama yupo mazoezi.

Kupoteza muda ni sehemu ya mbinu mojawapo ya kimpira. Lakini sasa kipa Moussa Camara anaitumia vibaya hadi anaua morali ya uchezaji kwa wenzake.

Timu haina Kasi inayotakiwa na ikifunga bao moja tu ndiyo uzingativu hupotea. Yaani Simba ikishinda bao Moja inaanza kujilinda badala ya kutafuta bao jingine.

Kapombe na Mohamed Hussein wafundishwe kurusha mipira Kwa wakati. Mpira ukitoka wao huchukua mpaka sekunde 45 kuurusha, matokeo yake wapinzani hupata muda wa kujipanga!
 
Mkuu naheshimu mawazo yako, lakini umeshindwa kutambua kama kikosi kimechoka sasa hivi kutokana na kucheza mechi ngumu mfululizo... Timu inakata pumzi kwa sababu ambazo zinaeleweka.
Kwani simba imepoteza?
 
Mkuu naheshimu mawazo yako, lakini umeshindwa kutambua kama kikosi kimechoka sasa hivi kutokana na kucheza mechi ngumu mfululizo... Timu inakata pumzi kwa sababu ambazo zinaeleweka.
Hivi kwa nini Valentino mashaka kila mechi anakaa benchi Lakini hachezi? Hofu ya kufungwa inamfanya Fadlu kutokuwatumia wachezaji wengine ambao anao na wangempa matokeo chanya.

Hivi ni kweli kuwa kila mechi ni Lazima Mohamed Hussein acheze?
 
Fatigue ya mechi ya jpili....

Kumbuka pia walicheza pungufu hivyo kazi waliofanya ilikua ni ya hatari......

Kikubwa matokeo yapatikane ......ila Fatigue zinaumiza wachezaji ......na ushindi unahitajika .....Tushukuru point tatu kibindoni ...... baaaaaaaaaaaaaaaaaasi kwa leo

Ila awape nafasi akina Nouma.....Valentino, kijili nk
 
Umejawa hofu ya kufungwa kiasi ni kama unazuia wachezaji kuchakarika.

Imani yako kwa Mohamed Hussein, Fabrice Ngoma inaigharimu Timu.

Kibu D ana maguvu Lakini achezi kitimu. Umeshindwa kumuelekeza kuwa akicheza kitimu Simba itafaidika zaidi?

Ahoua anajua kucheza mpira Lakini hachezi kimpira. Afunzwe kuwa kipaji chake kinatakiwa kiinufaishe Timu . Asicheze kama yupo mazoezi.

Kupoteza muda ni sehemu ya mbinu mojawapo ya kimpira. Lakini sasa kipa Moussa Camara unaitumia vibaya hadi anaua morali ya uchezaji kwa wenzake.

Timu haina Kasi inayotakiwa na ikifunga bao moja tu ndiyo uzingativu hupotea. Yaani Simba ikishinda bao Moja inaanza kujilinda badala ya kutafuta bao jingine.

Kapombe na Mohamed Hussein wafundishwe kurusha mipira Kwa wakati. Mpira ukitoka wao huchukua mpaka sekunde 45 kuurusha, matokeo yake wapinzani hupata muda wa kujipanga!
Tofauti yenu kwenye mechi ya leo na wale Waarabu waliocheza na Yanga Kwa Mkapa, ilikuwa ni rangi tu! Yaani hata sijaamini kama timu kama simba inaweza kukalinda kagoli kamoja dhidi ya timu kama Singida Black Stars!
 
Ungemalizia kwa kuandika "tawi la Yanga" 😆😃😅

Fadlu anawaza zaidi kutofungwa kuliko kupata matokeo kutokana na ubora wa kucheza.

Halafu ni mzito wa kufanya "substitution" kiasi kwamba wakati mwingine mchezaji anaingizwa kucheza bila ya kuleta matokeo chanya.

Mpanzu ni bonge la mchezaji Lakini anacheza kwenye Timu isiyo na muunganiko! Wanamchosha tu!
 
Tofauti yenu kwenye mechi ya leo na wale Waarabu waliocheza na Yanga Kwa Mkapa, ilikuwa ni rangi tu! Yaani hata sijaamini kama timu kama simba inaweza kukalinda kagoli kamoja dhidi ya timu kama Singida Black Stars!
Kama haujui mpango kazi wa Fadlu ni kuwa akijua anacheza na wewe mechi mbili zinazofuatana, anatumia mechi ya kwanza kukuacha ucheze ili akusome ubora wako ulipo na hilo lilikuwa moja ya malengo yake ya leo.
 
Hivi nyie wanaume hamuwaonei huruma wanaume wenzenu?? Yani kwa mtiti mtiti waliopitia bado mnawalaumu?? Kwani wenyewe sio binadamu....wanatumia maji?
Nyie wenyewe majumbani kwenu kimoja chalii...
Si ndiyo achezeshe wengine... Mbona hata majumbani mwetu michepuko hutumiwa kuwapumzisheni nyie wenye uchovu..
 
Si ndiyo achezeshe wengine... Mbona hata majumbani mwetu michepuko hutumiwa kuwapumzisheni nyie wenye uchovu..
Buahahahhaaha.... 😆 😆 😆
Msyuuuu😎😎
Hizi mechi za mwishoni sio za kubeti...anawajua wachezaji wake ndo maana yupo hapo na kafika mpk fainali shirikisho...muacheni Komandoo Fadlu wetu....yani unataka amuingize kijili akatoe boko? Aisee muacheni kocha afanye anayoyaona yanafaa kwa kipindi husika
 
Back
Top Bottom