Fadlu badilika ama ubadilishwe

Fadlu badilika ama ubadilishwe

Umejawa hofu ya kufungwa kiasi ni kama unazuia wachezaji kuchakarika.

Imani yako kwa Mohamed Hussein, Fabrice Ngoma inaigharimu Timu.

Kibu D ana maguvu Lakini achezi kitimu. Umeshindwa kumuelekeza kuwa akicheza kitimu Simba itafaidika zaidi?

Ahoua anajua kucheza mpira Lakini hachezi kimpira. Afunzwe kuwa kipaji chake kinatakiwa kiinufaishe Timu . Asicheze kama yupo mazoezi.

Kupoteza muda ni sehemu ya mbinu mojawapo ya kimpira. Lakini sasa kipa Moussa Camara anaitumia vibaya hadi anaua morali ya uchezaji kwa wenzake.

Timu haina Kasi inayotakiwa na ikifunga bao moja tu ndiyo uzingativu hupotea. Yaani Simba ikishinda bao Moja inaanza kujilinda badala ya kutafuta bao jingine.

Kapombe na Mohamed Hussein wafundishwe kurusha mipira Kwa wakati. Mpira ukitoka wao huchukua mpaka sekunde 45 kuurusha, matokeo yake wapinzani hupata muda wa kujipanga!
Wewe si mtu wa mpira kabisa. Unadhani wachezaji ni maroboti? Acheni kukatisha watu tamaa. Tuletee kocha wako atakayefanya uyatakayo.
 
Wewe si mtu wa mpira kabisa. Unadhani wachezaji ni maroboti? Acheni kukatisha watu tamaa. Tuletee kocha wako atakayefanya uyatakayo.
Sasa hoja yako ni uroboti wa wachezaji ama ni nilete kocha mwingine?

Saa 72 kati ya mechi na mechi yanatosha kwa maandalizi kwa Kila mechi.

Kwa ivo unataka kusema na waliopanga rariba ya hizi mechi nao Siyo watu wa mpira?
 
Kocha leo alitaka point 3 iwe kwa goli moja au zaidi...baada ya kuona chances zimepotea nyingi kipindi cha kwanza...kipindi cha pili akawa hana shida ya magoli kwa sbb aliona akifunguka Singida hawana cha kupoteza watakufunga wakupotezee cv yako...kwa sbb hata wangemfunga simba wasingepanda kuifikia simba alipo so ingeharibu tuu malengo ya simba...ndo maana mwalimu akamuingiza kibu na Hamza...kibu awape mikimbio awachoshe tuu na Hamza awazuie...
Kudos komandoo Fadlu...
 
Hivi kwa nini Valentino mashaka kila mechi anakaa benchi Lakini hachezi? Hofu ya kufungwa inamfanya Fadlu kutokuwatumia wachezaji wengine ambao anao na wangempa matokeo chanya.

Hivi ni kweli kuwa kila mechi ni Lazima Mohamed Hussein acheze?
Kwa hiyo unataka apange nani na nani....
 
Umejawa hofu ya kufungwa kiasi ni kama unazuia wachezaji kuchakarika.

Imani yako kwa Mohamed Hussein, Fabrice Ngoma inaigharimu Timu.

Kibu D ana maguvu Lakini achezi kitimu. Umeshindwa kumuelekeza kuwa akicheza kitimu Simba itafaidika zaidi?

Ahoua anajua kucheza mpira Lakini hachezi kimpira. Afunzwe kuwa kipaji chake kinatakiwa kiinufaishe Timu . Asicheze kama yupo mazoezi.

Kupoteza muda ni sehemu ya mbinu mojawapo ya kimpira. Lakini sasa kipa Moussa Camara anaitumia vibaya hadi anaua morali ya uchezaji kwa wenzake.

iTimu haina Kasi inayotakiwa na ikifunga bao moja tu ndiyo uzingativu hupotea. Yaani Simba ikishinda bao Moja awinaanzakujilinda badala ya kutafuta bao jingine.
Kapombe na Mohamed Hussein vizurwafundishwe kurusha mipira Kwa wakati. Mpira ukitoka wao huchukua mpaka sekunde 45 kuurusha, matokeo yake wapinzani hupata muda wa kujipanga!
Sawa, ila ni vizuri pia kuzingatia kuwa wachezaji wamecheza mechi nyingi mfulilizo
 
Sawa, ila ni vizuri pia kuzingatia kuwa wachezaji wamecheza mechi nyingi mfulilizo
Lupweko ndiyo hoja yangu. Presha ya Fadlu kuogopa kufungwa inamfanya asitumie wachezaji wengine hata kama anaowatumia wameonesha kwa uwazi kuwa wamechoka!
 
Unaongea kweli kabisa. Hakuna jambo Huwa linaniuzi kama kutokurusha mpira Kwa haraka. Unakuta Mohamed husein ananafasi ya kurusha mpira Kwa haraka kabla maadui hawaja mark man to man lakini kinachotokea dakika za mwisho anapata tabu amrushie nani mpira wakati maadui washakaba. Kingine kipa ashadaka mpira na mabeki washafungua badala arushe Kwa haraka yeye anaanza kupoozesha Tena.
 
Back
Top Bottom