SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,836
- 1,845
wakati wananchi wakimshangilia Rais Magufuli kwa matamko yake yasiyoisha, wasomi wasiwasi umetujaa kwa sababu tunaona atafail vibaya ndani ya miaka mitano. Sababu ni zifuatazo
- Mapato ya nchi hayaongezeki kama alivyotegemea, ukizingatia kushuka kwa mapato ya bandari kwa hali ya juu kuwahi kutokea nchini, kupungua kwa mizigo, na kushuka kwa sekta ya Utalii ambayo ndo inaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni (25%). Mpaka sasa sekta imeanguka kwa asilimia 5%
- Kuongezeka kwa matumizi yasiyokuwa ndani ya bajeti, (matumizi mkurupuko) kwa mfano kulazimisha serikali kuhamia Dodoma huku kukiwa hakuna hiyo bajeti. Rais kugawa fedha bila mpangilio wowote wala idhini ya bunge.
- Rais kutofuata mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali yake bungeni. Wakati kilimo ikiwa bado ni sekta ya kipaumbele katika mpango huo, mpaka sasa hatujaona msisitizo wowote katika sekta husika ambayo ndo inaongoza kwa kuajiri nguvu kazi ya taifa , zaidi ya rais kusema wilaya itakayopatwa na njaa atamfukuza mkuu wa wilaya na mkurugenzi (hii inaongezaje tija ya kilimo kwa mkulima??)
- Rais kuingiza siasa katika shughuli muhimu za kitendaji, kwa mfano kuteua wakurugenzi wa wilaya na mikoa wasio weledi na makada wa ccm, wakati akitambua hawa ndo msingi wa usimamizi wa maendeleo na utaalamu katika maeneo yao, kwa
- Wahisani kujitoa katika mipango ya maendeleo, MCC ni mfano mzuri
- kufifia kwa demokrasia kwa wapinzani kuzuiliwa kufanya mikutano na shughuli za kisiasa. Ikumbukwe wapinzani wamekuwa whistle blower wazuri katika ufisadi na ubadhilifu huku skendo zote kubwa katika nchi hii kuwa ziliibuliwa na wapinzani. Kuwafunga midomo ni kuwapa mianya mafisadi kujenga syndicate mpya za kupiga pesa, lakini pia rais anayefanya kazi bila challenge huishia kujisahau na kuharibu
- Rais kuchukiwa na watumishi wa umma, ikumbukwe rais tangu aingie madarakani amekuwa akiwasema vibaya watumishi wa umma huku akiwashushia tuhuma collectively utafikiri wote ni mafisadi. Mpaka sasa preliminary observation inaonyesha rais magufuri ndo rais unpopular among public servants kuliko rais yoyote Tanzania
- Rais kukiri mbele ya wananchi kuwa angejua ugumu wa kazi hiyo asingegombea, hii inaonyesha hakujiandaa au ali underrate kiti hicho, hivyo mpaka sasa hajui namna ya kuji adjust
- washauli wa rais kugeuka washauliwa, hii utachanganua mwenyewe
- Mawaziri kuwa waoga kiasi cha kukurupuka katika kusapoti maamuzi na statement yoyote atakayosema bosi wao hata kama wanajua haifai kwa wakati husika
- Mwisho, Kutokuwa na sera ya kimataifa kama nchi,huku uhusiano wetu na nchi kubwa kiuchumi duniani ukianguka vibaya sana. hatujui mpaka sasa mlengo wetu kidiplomasia ni upi