Facebook wana block account za watu kulikoni ?

Facebook wana block account za watu kulikoni ?

A-town

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2011
Posts
494
Reaction score
169
Habari wadau, Binafsi facebook wame block groups zangu zote na nimejaribu kuwasiliana na watu kadhaa wanasema hata wao profile zao zimekuwa blocked je na wewe hali ikoje kwa upande wako? Je, una taarifa zozote juu ya kinachoendelea kuhusu FB? Tujuzane mapema.
 
ni kweli hata fb yangu nikiifungua inanletea malink ya ajabu! Mhh kumbe sio mimi mwenyewe tu! Ngoja niwasiliane na mark zugerberg.
 
Mi walinifanyia hivyo kama miezi miwili iliyopita. Nikatumia akaunti ya mtu mwingine kuwasiliana nao, wakasema akaunti yangu ina taarifa za uongo ndio maana wamei-suspend, nikasema basi waweke taarifa za ukweli wanazojua wao kwa sababu mi ndio mhusika. Wakasema niwatumie kitambulisho kilichotolewa na sirikali, nikawatumia.

Kufumba na kufumbua wameshabadilisha tarehe ya kuzaliwa. Ile ya kwanza niliandika nimezaliwa 1908 wakati ni 90.
Wasiliana nao, watakurekebishia.
 
Group gani ulikuwa unaendesha?
 
iyo pia nitatzo kuweka taarifa sio sahihi,lakn mkuu mimi washablock 1 nililazmika kufungua nyingne tu ila ukwel sikuwai kuwasliana nao nashkuru umefanya nijue ilo!!
 
Kama magroup yako ni ya ze utamu na watu wakatoa taarifa lazima watablock
 
Wame block ili mmalize mitihani yenu ya Form 4. Nyambaaf nyinyi.. wachora mazombie.:yell:
 
Back
Top Bottom