Facebook imenivunjia ndoa, nitafanyeje jamani?

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,459
4,055
Ndugu, jamaa na Marafiki

Ni siku ya 3 tangu shemeji yenu aseme hanitaki tena na kuondoka kabisa hataki tena majadiliano yoyote na mimi baada ya kufungua simu upande wa Facebook na kukuta muambatano wa picha yangu na ya mdada ambae ni rafiki yangu wa Facebook (photogrid) ambapo mtandao huo wameandika jina langu na la huyo mdada nisiemfahamu na kutupongeza kwa kutimiza miaka mitatu ya urafiki wetu katika Facebook.

Tatizo ni kwamba shemu wenu si mzoefu wala si mtumiaji wa mitandao ya kijamii.

Nimejaribu kumbembeleza na kumwelezea ukweli ila amegoma anadai kuwa hao Facebook wametoa wapi picha zetu hadi kuziunganisha na mdada huyo?

Analia sana ananiuliza kwanini sikuwahi kumwambia kama nilikuwa na uhusiano na mtu takribani miaka mitatu bila kumwambia muda wote nimekuwa namdanganya.

Nimeona nije huku tupate kushauriana nifanyeje kwa hili
 
usimaindi bwana mdogo..haya mambo yapo..tena sio stori za kutunga!!kwa vile shem si mzoefu wa mambo haya wewe tengeneza muambatano wa picha yake na jamaa kisha kamuulize mbona kakusaliti!!..
 
muunge na yeye facebook mtumie request baada ya mwaka mmoja ndoa yenu itarudi Simple....!!!!!!!!!!!!
 
Hahaha maskin embu mtafsirie kistaarabu af mkija kupatana mpeleke ata english course
 
Mchukue huyo huyo mdada mlounganishwa picha zenu na hao fesibuku... Mwambie yeye na fesibuku ndo waliovunja ndoa yako...
 
Ushamba buana !!!
Mueleze vizuri... Tafuta watu wengine waliofanyiwa hivyo na utumie kama mfano kumuelewesha
 
Pole,kwa sasa muache kwanza hasira zitulie.
Baada ya siku Kama 2 mfate face to face and muombe uongee nae. Atakuelewa,I'm sure Hata atakaokuwa anawaelezea watamuelewesha kuhusu hilo..
 
Naomba nicheke kwanzaaaaa,,,,

Hapo lugha gonganaa tuuu.. Juu ya Picha wanaandika maelezo bhana. Mueleweshe tu
 
Back
Top Bottom