Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Wataalam kadhaa wa mawasiliano wameonya kuwa application ya Facebook hutumiwa na wadukuzi kusikiliza mazungumzo ya watu muda wote kwa siri kubwa, App hiyo inadaiwa kutumia simu za watu kudukua na kusanya taarifa ya kile wanachokizungumza watumiaji wake.
Udukuzi huo umekuwepo kwa miaka mingi sasa, lakini onyo la hivi karibuni la Kelli Burns, Profesa wa mawasiliano katika chuo kikuu cha South Florida, limetiliwa mkazo.
Profesa Burns amedai kuwa application hio katika simu hukusanya sauti kutoka katika simu ya mtumiaji kwa lengo ambalo halijafahamika ni nini.
Bado kuna mjadala miongoni mwa wataalamu wa mawasiliano kuhusu ni wapi mawasiliano ya simu hizo hupelekwa, lakini imethibitika kuwa sauti hizo hazichukuliwi ili kumsaidia mtumiaji wa simu, lakini wameonya kuwa yawezekana kuwa application hiyo husikiliza mijadala na kuitunza kwaajili ya matangazo.
Amesema ili kuthibitisha uwepo wa udukuzi huo, alijadiliana mada kadhaa karibu na simu yake na kisha kugundua kuwa tovuti hiyo imeonekana kuonesha matangazo yanayohusiana na alichokizungumza.
Kwa upande wake Facebook imethibitisha kuwa ni kweli kuwa inadukua sauti ila inadai kuwa application yake inasikiliza kinachotokea duniani lakini kama njia tu ya kuona nini watu wanasikiiza au kuangalia kwenye mtandao wao.
Madai hayo yanaendana na ripoti zilizopo kuwa mtandao huo huonesha matangazo ya vitu ambavo watu wamevitaja kwenye mazungumzo yao. Facebook imedai kuwa husikiliza sauti na kukusanya taarifa kutoka kwa watumiaji lakini haitumii sauti hizo kuamua kile kinachoonekana kwenye tovuti.
Viongozi wetu wa serikali hasa wa taasisi nyeti mnaoingia na masimu yenu kwenye vikao vyenu kazi mnayo.
Source: The Telegraph