Joeli
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 4,941
- 3,417
Facebook wametangaza kitu kipya kwa
simu za Android walichokipa jina la Home.
Kwa muda mrefu kulikuwa na uvumi kuwa
Facebook wanajiandaa kuja na simu yao
mpya na hata siku za karibuni
ilipotangazwa kutakuwa na tamko toka
Facebook uvumi ulisambaa kuwa
wanatangaza simu yao mpya lakini
haikuwa hivyo.
Mark Zuckerberg, CEO wa Facebook
amesema lengo hasa ni kufanya
unapowasha simu yako kitu cha kwanza
kinachotokea ni watu ulionao Facebook
ambapo zitatokea notification za message
walizokuandikia, comments na hata tags
na utaweza kujibu bila kufungua
application yoyote. Yote hii ni kwa ajili ya
kuingia katika mfumo wa matangazo
kupitia mobile web kwani ni sehemu
pekee ambayo Facebook haijaweza
kuweka ads zake. Android ambayo kwa
siku za karibuni imekuwa na watumiaji
wengi duniani inaonekana kuwa sehemu
pekee ambayo Facebook inaweza
kuanzisha utaratibu wa matangazo kwa
gharama nafuu kulinganisha na kama
wangeamua kuja na simu zao wenyewe.
Nini Utaweza Kufanya
Pamoja na kuwa na uwezo wa kusoma
kila kinachoendelea kwenye account yako
ya Facebook pale unapowasha simu,
utaweza pia kutuma message wakati
ukiendelea kutumia application nyingine
kama Whatsapp au Keek kwa kutumia kitu
kilichopewa jina la Chat Heads. Ikitokea
ukapata message kwa mfano wakati
unatumia Instagram, picha ya
aliekuandikia itatokeza kwa juu na
utaweza kujibu kwa kubofya bila kuacha
ulichokuwa unakifanya.
Utaipataje?
App hii itaanza kupatika katika Google Play
Store kuanzia April 12. Kama tayari unayo
Facebook Messenger au Facebook App
yoyote utaombwa uijaribu Home.
Ukishaiweka na kuanza kuitumia
utagundua kitu kinachoitwa Chat Heads
ambayo inachukua nafasu ya Facebook
Messenger.
Simu Gani Zitakuwa Nayo:
Bahati mbaya Home haitakuwa katika kila
simu yenye Android. Simu zitakazoanza
nayo ni HTC One, HTC One X, HTC One X
+, Samsung Galaxy S3, Samsung Galaxy
S4, na Samsung Galaxy Note II. Simu
nyingine zitaongezwa baadae.
Ili kuondokana na usumbufu wa kuiweka
kwa ku-download kwenye Google Store,
simu zitakazoanza kutengenezwa aadae
zitakuwa tayari zinayo Home moja kwa
moja na kwa kuanza HTC watakuwa wa
mwanzo kuiweka Home katika simu zao
zinazotoka hivi karibuni.