Facebook hatarini kuvunja ndoa

Facebook hatarini kuvunja ndoa

Sishabikii kushindana na mume .. But lazima hiyo sintofahamu iliyotokea imesabababishwa na kitu.. Either kama alivyosema Asnam huenda bidada anatupia picha za tupaja na nyonyos lakini pia huenda mume nae ana kamchezo ambako sio kazuri .. Kwa hyo hapo kila mtu anawasiwasi na mwenzie.

La muhimu ni waelewane na sio kushurutishana lolz..Akimlazimisha si ataingia kwa jina la bandia na ataendelea kuuza.

BUSARA itumike zaidi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Na picha za bandia?
 
fb napajua vizuri mi huwa siweki picha za mauzo,na pia marafiki alionao watakua ni wale waliokatika vichwa wanacomment vitu wanavyovijua wao,halafu mume akae kimya si itakuwa ubwege huo.
Kweli... Nitupie username nione
 
Wanawake wengi walioolewa wanaupload fb picha ambazo wamekumbatiwa na waume zao. Tena hao wanaume wanakuwa wametumbua jicho sawasawa kwa mpiga picha. Mwanaume ukitaka kukoment unaona kama huyo mume anakuona...

ha..ha..haa! Kazi kwelikweli.
 
ni kweli hata mimi niliombwa nitoke tangu 2008 kipindi hicho facebook haijashika sana, na kwa roho moja nlitoka mpaka leo, ni heshima tu, hakuna haja ya kushindana na mumeo, afterall fb sidhani kama ni muhim sana kivile mpaka ilete ugomvi, ni aibu kwako wewe ambaye ndoa yako itakua na utata au kuvunjika kisa eti fb au unagoma kutoka fb,.otherwise, kama mpo fb na ni wanandoa basi jiheshimuni kwa picha zenu, na status zenu, msivuke mipaka na mkaanza kutongoza na kutongozwa mitandaoni humo na kuisahau ahadi yenu ya ndoa..

Ila tuambiane ukweli kuwa huku JF kwa watu mlioolewa ni Shwari kuliko Facebook? Mh!
 
mke anaweka picha za kuonyesha uumbaji wa Mungu kwann mume asipate wivu,kama fb yuko kwa ajili ya kutangaza biashara za kuingiza kipato simshauri kujitoa wazungumze yaishe,lakini kama ni kuchart tu na marafiki ajitoe sidhani kama atapungukiwa viungo vya mwili,wakati mwingine sio lazima kufanya mashindano kwenye ndoa hasa mwanamke kushindana na mwanaume eti kwa sababu yeye anafanya basi na ww ufanye, unapomheshimu mtu na yy atakuheshimu kwa sababu fb sio moja ya basic needs in life.
Thank you...umemaliza ushauri wangu
 
fb hata uweke picha umevaa baibui na ushungi juu mtu akiamua kukutongoza atakutongoza tu coz kuna mijitu mingine imejiunga kwaajili hiyo so ni wewe mwenyewe tu kuwa na mcmamo.
Kumbuka huwezi kuzuia joto la moto kwa bati....Facebook haina maadili hasa ke sishauri kabisa...Mimi mamaJ aliniomba nimwelekeze namna ya kujitoa baada ya kuona hamna la kumlea/kumfundisha.
 
FB ina matatizo sana. Tulitoka na mke wangu kitambo mno na hatuna hamu ya kurudi maana balaa lililotukuta asikwambie mtu.
 
mimi niliongea na fiancee wangu then we agreed all of us to get out there, we did so
 
Hivi inakuwaje, mume na mke mmejiunga kwenye mtandao wa kijamii kama Facebook then baada ya muda flani mume anampiga marufuku mke wake kutoingia Facebook tena, kisa wanaume wana like na kucomment sana hasa kwenye picha na status za mke, lakini mume huyo yeye bado anapeta kwenye huo mtandao. Mke kapewa onyo akiingia tena basi ajue na ndoa itavunjika.
So wana jamvi wenzangu naomba mnijuze ni haki kwa huyo mume kufanya hivyo? Na kwanini atoke mke tu, wasitoke wote?

Siri ya ndoa kudumu ni kwa mwanamke kumtii mumewe. Ukiwa mtii ndoa haiwezi vunjika. By the way Facebook si muhimu kama ndo

Sent using wireless by wire
 
FB ina matatizo sana. Tulitoka na mke wangu kitambo mno na hatuna hamu ya kurudi maana balaa lililotukuta asikwambie mtu.

poleni sana kwa yaliyowakuta fb na hongereni kwa kujitoa wote, na ninaamini hakuna mwenye wasiwasi na mwenzie sasa, ila mimi tatizo langu ni kwa huyo mume ambaye yeye anaendelea kula maisha ya fb haoni kwamba anamuumiza mwenzie ki hisia na lazima atakuwa na mawazo tele kama; kwa nini mwenzie amebaki humo na ni watu wa namna gani ana chart nao? Ila kwasababu mwanamke hana power kwa mume inambidi atulie tu bt moyoni anaumia
 
Asante mkuu,eti jamaa anashangaa mshikaji kumuonea wivu mkewe na watu wa fb walivyo na maudhi hawakawii kumwita

mkeo hny,luv,swt umekaa tu unaangalia!...

watu wa fb ndio zao hawana maana kabisa hasa wanaume
 
Back
Top Bottom