Zinatumika sana ndio maana zinapata ajali. Nenda India kawaulize kwanini Migs zao zinapata sana ajali kuliko za Urusi, Egypt au kwingineko. Air Marshall wao mmoja aliwahi sema ni bora apate ajali nyingi kipindi cha amani kuliko kufikia vitani marubani wake hawajui kuzitumia ndege katika extreme conditions.
Urusi huwa inafanya war games na drills kwenye mazingira mazuri kabisa, matokeo yake hawawezi rusha ndege anga la Ukraine kufanya aerial denial na kuweka no fly zone mpaka leo.
Na ajali za ndege zinapimwa kwa vitu vingi, number of flights, idadi ya ndege kwenye operations, flight hours, n.k. Tafuta list ya worst airplanes kwenye safety uone zilivyojazana Tupolev na Antonov za Mrusi.
Safety records zinaonyesha F-35 ni very safe tafuta uzisome data zake. Na tukienda kwenye ratio, Russia ana Su-57 hata kumi hazifiki ukiachana na prototypes ambazo hatuzihesabu, ila Su-57 moja iliwahi anguka, so technically zaidi ya 10% ya Su-57
View attachment 2392835
Wakati F-35 zipo zaidi ya 800 na humohumo zipo B na C version za Marines na Navy ambazo kwa kawaida hupata ajali nyingi kuliko za Airforce. Yani hapo unalinganisha safety standards baina ya ndege ya maonyesho ambayo hakuna hata squadron iko available dhidi ya ndege zinazofanya kazi nchi tofauti duniani kuanzia Japan, South Korea, Israel, UK, US na kwingine