Extremism iko kila mahali

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,635
729,551
Siasa kali au misimamo mikali ya kidini si neno geni masikioni mwetu japo lilikolezwa na kuwa maarufu sana kwenye mifarakano ya mashariki ya kati na wazungu(hayo ni ya kwao na tuwaachie wenyewe)

Msimamo kama huu pia tumeuona kwa wafia imani wengi. Tunakumbuka wale ndugu zetu masalia walioenda kuweka kambi uwanja wa ndege kipindi kile wakitaka kusafiri kwenda ulaya bila ya ticket wala nyaraka zozote na bila kujua wanaenda au wanataka kwenda nchi gani

Mimi nimewahi kukutana na hawa watu wenye imani kali kwenye Buddhism, ndani ya haya mafundisho kuna msingi wake mkuu ambao ni amri tano na mojawapo inasema USIUWE

Sasa hawa ndugu wamekuwa kama wendawazimu (hulka ya mfia imani yeyote au mwenye msimamo mkali)wao wamezidisha huruma kiasi kwamba kwanza hawavai kabisa viatu, imani yao ni kwamba ukivaa viatu unaweza kukanyaga kiumbe kidogo sana na kukiumiza! Sidhani kama ukiwa peku huwezi

Mwendo wao huwa wa taratibu na makini mno muda wote wakiangalia chini ili kuona kama kuna kiumbe chochote wasije wakakikanyaga na kukiuwa
Kuna baadhi ya maeneo hutembea na mifagio laini sana na kufagia kabla hawajashusha mguu ili kuokoa kiumbe chochote kidichoonekana
140afb9f3c40fc6864501d2c212e1d93.jpg

Hii nilijikuta Nashindwa kuendelea na mafundisho yake kwakuwa kanuni moja ya uhai ni kufa kufaana...ili kimoja kiishi ni lazima kingine kife. .hii ni kanuni ya kiasili ya uumbaji

Kinachofanywa na mabudda hawa ni reflection ya watu wenye misimamo mikali ya kiimani, ni watu hatari sana kwakuwa yeye hana tafakuri yeye A ni A na B ni B fullstops

8e42299b55d669c0eb7bfc143f64ca92.jpg
 
Ya dunia yana mengi maajabu...ukistaajabu ya Masalia utacheka ya mabudha!
 
Siasa kali au misimamo mikali ya kidini si neno geni masikioni mwetu japo lilikolezwa na kuwa maarufu sana kwenye mifarakano ya mashariki ya kati na wazungu(hayo ni ya kwao na tuwaachie wenyewe)
Msimamo kama huu pia tumeuona kwa wafia imani wengi. Tunakumbuka wale ndugu zetu masalia walioenda kuweka kambi uwanja wa ndege kipindi kile wakitaka kusafiri kwenda ulaya bila ya ticket wala nyaraka zozote na bila kujua wanaenda au wanataka kwenda nchi gani
Mimi nimewahi kukutana na hawa watu wenye imani kali kwenye Buddhism, ndani ya haya mafundisho kuna msingi wake mkuu ambao ni amri tano na mojawapo inasema USIUWE
Sasa hawa ndugu wamekuwa kama wendawazimu (hulka ya mfia imani yeyote au mwenye msimamo mkali)wao wamezidisha huruma kiasi kwamba kwanza hawavai kabisa viatu, imani yao ni kwamba ukivaa viatu unaweza kukanyaga kiumbe kidogo sana na kukiumiza! Sidhani kama ukiwa peku huwezi
Mwendo wao huwa wa taratibu na makini mno muda wote wakiangalia chini ili kuona kama kuna kiumbe chochote wasije wakakikanyaga na kukiuwa
Kuna baadhi ya maeneo hutembea na mifagio laini sana na kufagia kabla hawajashusha mguu ili kuokoa kiumbe chochote kidichoonekana
Hii nilijikuta Nashindwa kuendelea na mafundisho yake kwakuwa kanuni moja ya uhai ni kufa kufaana...ili kimoja kiishi ni lazima kingine kife. .hii ni kanuni ya kiasili ya uumbaji
Kinachofanywa na mabudda hawa ni reflection ya watu wenye misimamo mikali ya kiimani, ni watu hatari sana kwakuwa yeye hana tafakuri yeye A ni A na B ni B fullstop
Hahah hahah hahha sijui kwanini nimepata picha ya Bi. Mkora wa JF kuwa naye yuko kundi hili la ma exrimist
 
Mshana jr, pengine hawa mabudha wako sahihi kwani moja ya amri kuu za Mungu zilizo katika biblia inasema usiue. Na hiyo "usiue" imejitosheleza na haina ufafanuzi zaidi kwamba usiue nini.

Pengine inamaanisha usiue kiumbe chochote na si kwamba inamaanisha usiue binadamu mwenzako tu bali kiumbe chochote kama mnyama au mdudu.

Kwa hiyo hao mabudha wenyewe wakiwa sehemu wakiumwa hata na mbu kazi yao ni kupunga tu mikono kuwafukuza na siyo kuwaua hata kwa aerosol spray yoyote?
 
Mshana jr, pengine hawa mabudha wako sahihi kwani moja ya amri kuu za Mungu zilizo katika biblia inasema usiue. Na hiyo "usiue" imejitosheleza na haina ufafanuzi zaidi kwamba usiue nini.

Pengine inamaanisha usiue kiumbe chochote na si kwamba inamaanisha usiue binadamu mwenzako tu bali kiumbe chochote kama mnyama au mdudu.

Kwa hiyo hao mabudha wenyewe wakiwa sehemu wakiumwa hata na mbu kazi yako ni kupunga tu mikono kuwafukuza na siyo kuwaua hata aerosol spray yoyote?
Kwenye mafundisho ya ubudha dhana ya kuua imefafanuliwa kwa undani sana kwamba usiue chochote chenye uhai hata kiwe kidogo kiasi gani
Sasa umezungumzia dhana ya mbu kwa mazingira ya Tanzania, tuliwahi kuuliza swali kama hilo kwa mwalimu wetu...akashangaa sana akatuuliza huyo mbu kafikaje au katoka wapi mpaka akufikie (kwa wenzetu mbu ni kitu kisichofikiriwa tena)
Jibu la swali lako kwa mtazamo wangu ni kwamba unamfukuza taratibu aondoke
Zilishawahi kuletwa toka India dawa za kupuliza za mbu lakini baada ya muda watu wakazistukia kuwa haziui bali zinawalevya tu kwahiyo watu wakachukulia kuwa ni feki
Ilikuja kujulikana baadae kuwa dawa haikua feki bali wamiliki wa hicho kiwanda huko India ni waumini wazuri wa imani ya Kihindu ambayo nayo inakataza kuua kwa namna yoyote, hivyo dawa yao haikuwa ya kuua bali kulevya ili mbu asikuume baasi. ..biashara iliishia hapo
 
Lakini hawa sabato masalia hii yao ni kali aisee yaani uende ulaya bila viza,wala hujui nchi unayo enda,au ni wasanii flani??kwanin wasiende somalia kwa miguu?eti wanaenda ulaya bila kujua nchi unayo enda kama sio wehu nini??hawa watakuwa wame wehuka.
 
Extremists ndio wanaosimamisha na kudumumisha ofisi ya taasisi yoyote ama jamii yoyote ile duniani.
Hawa wana dhamira ya dhati kutetea na kupigania dhidi ya wanaotaka kuhujumu utaratibu.

Bila extremists hakuna taasisi ama serikali ingeweza kudumu.
Hawa ndio waliobeba identity ama belief system ya institution yoyote.

Pia ni watu wenye matatizo, linapofika swala la kuhitaji mabadiliko chanya ya fikra.
 
Yaani upo kama mimi tu...Hasa ukisoma vitabu vyao vimejaa Falsafa tupu.
Siri ni moja wanachambua kipengele kimoja kimoja kwa undani sana bilauri ya maji inaweza kuandikiwa kurasa zisizopungua kumi na hata wewe msomaji unajikuta unakubaliana na kila kitu...very deep in phylosophical analysis
 
Wanafalsafa yao moja inasema "Dhambi ni mtizamo wako na kama unaona kutembea na mke au mume wa mwenzio kutakupa furaha, sawa kikubwa usiharibu maisha yako. Huwa naitafakali hii falsafa halafu nashindwa kuielewa ila kiukweli jamaa wako very deep.
 
Kuna moja inasema kama ukifanya jambo na halina madhara yoyote kwako wala kwa wengine basi hilo ni jambo jema
 
Back
Top Bottom