Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 362
- 906
Ebu tujadili kidogo kuhusu Executive Protection ya maraisi, Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).
Sasa twende pamoja......
Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili amebeba begi la mkononi, Je umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?
Hiyo picha hapo juu (Picha No 1), JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole, Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni sasa hilo begi ni la nini?
Nataka uelewe kitu hapa....
Na si yeye tu, siku ukibahatika kuwa mahala ambako Rais SSH yupo, tazama kwa makini wale walinzi wake, hasa ile 'first ring', wale walinzi wenye suti wanaomzunguka, utaona vivyo hivyo pia, kuna maafisa wawili au watatu wana mabegi ya dizaini hii wamebeba mkononi (angalia Picha No 2).
Pia kama ulifuatilia juzi Rais SSH alipokwenda ziarani nchini Burundi.. kwenye 'inner cycle' ya walinzi Idara ya Ujasusi ya Burundi ambao waliokuwa wanawalinda yeye na Rais Ndayishimiye kwenye hasa ile 'first ring' kulikuwa na walinzi kadhaa ambao nao wana mabegi ya dizaini hii, (tazama Picha No 3).
Na mfano mwingine ni Rais Emmerson Mnangagwa, Mara zote akionekana maeneo ya umma lazima baadhi ya walinzi wake pia wana mabegi ya dizaini hii, Kwa mfano tazama Picha No 4 chini, utaona gari yake ikiwa imezingirwa na walinzi, Kuna maafisa kadhaa wana mabegi ya dizaini hiyo pia.
Naweza nikakupa mifano mingine mingi tu wa walinzi wa marais kama vile Paul Kagame, Edgar Lungu, Filipe Nyusi, Cyril Ramaphosa n.k. ambao wote pia walinzi wao kwenye 'first ring' lazima kuna maafisa ambao wanabeba begi la namna hii.
Kwa hiyo narejea swali, hili begi lina nini.?.....
Wakati fulani niliwahi kuona watu mtandaoni wakijadili kuuliza kuhusu haya mabegi enzi za JPM, Na katika mijadala ile kulikuwa na majibu matatu ambayo watu ndio walikuwa wakijadili sana na majibu haya matatu hayakuwa sahihi.
Mosi, Kuna watu walisema mabegi yale ni mabegi ya kawaida tu...
Yani walinzi wanambebea mzee document zake na personal effects za Rais kama vile simu, saa, notebooks n.k.
Jawabu la pili, kuna watu walikuwa wanasema kwamba begi hili ndani yake lina vifaa vya huduma ya kwanza, Yaani kwamba, lina vifaa vya kidaktari ambavyo vyaweza kutumika kutoa huduma ya kwanza kwa dhahrura kama ikitokea Rais amejeruhiwa.
Jawabu la tatu, kuna watu wanasema kwamba begi hili lina silaha ndani yake.
Majibu yote haya matatu hayako sahihi, Hizi sio dhima za begi hizi unazoziona kwa maafisa wa ulinzi wa Rais hasa ile 'first ring' inayomzunguka..
Kabla sijajadili begi hizi zina kazi gani, kwanza tuangalie kwa nini majibu haya matatu sio sahihi.
Tuanze na jibu la kwanza kwamba begi lina personal effect za Rais,
Si sahihi kwa sababu kiprotokali personal effect za Rais zinabebwa na Mpambe wake (ADC), Ndio maana ukitazama Picha No 5 na 6 utaona kwamba Mpambe wa Rais ana begi la mkononi na baadhi ya maafisa wa ulinzi nao wana mabegi ya mkononi.
Hili begi linalobebwa na ADC ndilo lenye vitu binafsi vya Rais wakati mabegi yale mengine ya maafisa wa ulinzi yana shughuli nyingine kabisa.
Jawabu la pili kwamba mabegi haya ya maafisa wa ulinzi wa Rais yana vifaa ya huduma kwanza nalo si sahihi kwa sababu, mahala popote Rais anapokwenda lazima ana daktari wake pamoja na ambulance.
Hii ambulance inakuwa equipped na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya matibabu ya dharura vya Raisi, mpaka akiba ya damu ya blood group la Rais.
Ambulance hii inakuwa equipped kwa capabilities za daktari wake kuweza hata kumfanyia upasuaji mdogo wa dharura ikihitajika kufanyika hivyo.
Kwa hiyo, vifaa tiba vinabebwa kwenye ambulance na sio zile begi, There is an exception though.
Kuna mara chache sana (nasisitiza mara chache sana) kwenye first ring ya ulinzi wa Rais afisa mmojawapo anatakiwa kubeba first aid kit.
Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa ambayo serikali ilitoa, walisema kwamba mpendwa wetu JPM alikuwa akiugua maradhi ya moyo kwa muda mrefu sana.
Sasa basi......
Kuna kitu sijui wangapi wali-notice. Katika miezi sita ya mwisho ya maisha ya JPM (kuanzia Aug 2020 mpaka Feb 2021) kwenye first ring ya ulinzi wake kulikuwa lazima kuwe na afisa amebeba ki-briefcase kidogo kama kibox hivi au cooler (tazama picha No.7 na no 8)
Yaani kulikuwa na maafisa ambao walikuwa wanabeba yale mabegi meusi kama kawaida, Lakini pia kulikuwa na afisa mmoja ambaye muda wote yuko kando ya Rais akiwa na hiki kijibriefcase.
Hii fasiri yake ni kwamba kwenye kipindi hiki hali ya maradhi ya mpendwa wetu ilikuwa mbaya na hivyo daktari wake akaelekeza lazima muda wote kuwe na vifaa vya dharura vya tiba pembeni yake kama ikitokea hali yake imebadilika ghafla.
Kwa hiyo kijibriefcase hiki, kina vifaa mahususi kabisa kwa ajili ya matibabu ya dharura ya maradhi ambayo yalikuwa yanamsibu mpendwa wetu kipindi kile, Hii ni exception.
Ndio maana sasa hivi hauoni mlinzi yeyote wa Mama SSH akiwa na kijibriefcase cha namna ile lakini bado wangali na walinzi wenye yale mabegi meusi kama kawaida
Jawabu la tatu kwamba begi hizi zina silaha si sahihi kwa sababu kadhaa.
Mosi, hao walinzi wote unaowaona wamevaa kaunda suti Wote wana side-arm kiunoni na wengine kiunoni na mguuni.
Pili, pengine wengi hawajui hili, kwamba kwa mfano likitokea shambulio la ghafla kwa Rais, Hii first ring ya ulinzi wa Rais kwa protokali za "Executive Protection" wao hawatakiwa kujibu mapigo, bali kazi yao ni kumuondoa Principal (Rais) kwenye eneo la hatari na kumpeleka eneo salama.
Hawa uniformed officers tunaowaitaga 'makirikiri', hawa wao ndio wanatumika kama CAT (Counter Assault Team), Hawa ndio wanajibu mashambulizi mpaka eidha wa-neutralize hiyo threat au mpaka Principal afike Mahala salama.
Lakini pia kwenye msafara kuna gari ambalo linatumika kama hifadhi ya akiba ya ammunition, mabomu ya kurusha, ballistic shields, gas mask n.k.
Kwa hiyo zile begi nyeusi zinazobebwa na walinzi wa Rais sio kwa ajili ya kuhifadhi silaha.
Kwa hiyo, begi hizi zina nini?......
Kimsingi begi hizi zinazobebwa na walinzi wa Rais zinaitwa "Portable Bulletproof Shield" na zatumika kuzuia risasi (tazama picha No. 9)
Kama likitokea shambulio, begi hizi zinakunjuliwa (zinafikia urefu mpaka mita 2) kisha wanamzunguka Rais, tazama picha No. 10.
Hizi begi zimeundwa kwa aina maalumu ya fiber zinazoitwa Spectra, au kwa jina lingine huitwa UHMWPE(Ultra-high-molecular-weight Polyethylene)
Aina hii ya fiber ina impact streght ya juu kabisa na ndio sababu kwa nini ina uwezo wa kuzuia risasi.
Nitoe mfano halisi.....
Wiki mbili zilizopita, helikopta iliyombeba Rais wa Colombia Ivan Duque ilishambuliwa kwa risasi ikiwa hewani na kulazimu kutua kwa dharura
Helikopta ilipotua, kama uli-notice utaona walinzi wake waliobeba mabegi mikononi, wakiyakunjua yale mabegi na kisha kuyavaa mgongoni (Tazama picha No. 11 na 12)
Huu ni moja ya mifano adhimu ya Portable Bulletproof Shield ikiwa inatumika, Kwa hiyo ukimuona Rais yuko eneo la umma na walinzi waliomzunguka baadhi yao wana mabegi mkononi, basi ujue sio document zile walizobeba, Ile ni sehemu ya mkakati wa dharura wa 'extraction' kama ikitokea Rais anashambuliwa.
Imeandikwa na Habibu Anga (Habibu B. Anga) The Bold
To Infinity and Beyond
Na kuboreshwa kidogo na Comred Mbwana AllyamtuView attachment 1862360View attachment 1862361View attachment 1862359View attachment 1862363View attachment 1862362View attachment 1862366View attachment 1862364View attachment 1862368View attachment 1862365View attachment 1862367View attachment 1862369