Exclusive: Video za wanamuziki wa Afrika 2015 zilizotazamwa zaidi Youtube

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Hii ni TOP 10 kati ya video za wanamuziki wa Afrika 2015 zilizotazamwa zaidi Youtube.. Na kati ya mafanikio anayoweza kujivunia mwanamuziki, ni suala la youtube ambapo inaonyesha;-

+ Ni jinsi gani kazi yako imekubalika na mashabiki
+ Ni jinsi gani una mashabiki wengi walio active kukupa support na wanaopenda kufuatilia kazi zako
+ Na ni jinsi gani unaingiza pesa kupitia video zako, hata bila ya kufanya shows, mikataba, au hatimiliki..

Hayo yote amezidi kuyadhihirisha nguli wa Bongo fleva diamond platnumz licha ya kuwepo mashabiki wachache wasiopenda maendeleo yake, lakini amezidi kuwatia pilipili na mchanga machoni kwa juhudi na mafanikio anayozidi kuyapata kila siku..

Na ukijaribu kuitazama list hii utagundua nyimbo 8 ni za wasanii wa Nigeria na mbili tu sio za Nigeria ambapo ni za Diamond, na Tanzania na Afrika mashariki kiujumla kwa mtu anaejitambua na mpenda burudani hana budi kujisifu kwa uwakilishi mzuri wa kichwa hiki cha bongo fleva, ambapo wasanii wenzake pia wamekuwa wakijifunza na kuiga mengi kutoka kwake na kuwa role model wao licha ya wao kukataa kuliweka hilo wazi, kiufupi amekuwa kama chuo cha bongo fleva

Hii ni mpaka leo tar 08, september
1. Psquare ft. Don jazzy - collable
11,076,652 views

2. Mr Flavour ft. Chidinma - Ololufe
4,796,162 views

3. diamond platnumz ft. Mr Flavour - Nana
4,550,423 views

4. diamond platnumz ft. Khadija Kopa - Nasema nawe
3,978,387 views

5. Wizkid - Ojuelegba
3,630,991 views

6. Davido ft. Uhuru + Dj Buckz - The sound
3,248,037 views

7. Kiss Daniel ft. Davido + Tiwa Savage - Woju
3,070,540 views

8. Davido ft. Meek mill - Fans mi
2,737,313 views

9. Olamide - Bobo
2,577,288 views

10. Korede bello - Godwin
2,405,917 views
 
acha ujinga wewe
Caapture.PNG
 
Hiyo nasema nawe watu wanapenda kuona ile miuno, yani kila nkiiangalia ile video najiona badoooo sanaaa....Weee Dai wenzio tutateguka hukuuu
 
Hiyo nasema nawe watu wanapenda kuona ile miuno, yani kila nkiiangalia ile video najiona badoooo sanaaa....Weee Dai wenzio tutateguka hukuuu

Lazima wanyooke, na vicampaign vyao vya kusema mi nimemunfollow na kura sipigi, sahv kapata followers milioni insta

wanafikiri kuchota maji kwenye kijiko baharini kunapunguza kitu hahahahaha
 
Umepashwa kwamba moja ya kanuni nyingi za siku hizi ili kujua nani ni mwanamuziki bora hii ni moja wapo ya kanuni hizo

Kuelewa naelewa saaana, kama unakumbuka chekechua ilivofikisha views laki moja alifungulia thread akisahau kuwa wengi wengi waliangalia video kwa shauku tu kutokana na kiki zake, baada ya kuona hata ya mziwanda bilima ni kali kuliko wakaikacha sahivi imedoda huwezi kuon hta wanaongelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom