Exclusive: Mahojiano na Fred Mpendazoe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive: Mahojiano na Fred Mpendazoe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 12, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.

  Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi!
  - Nyerere


  Watanzania bado wana maswali juu ya Chama Cha Jamii (CCJ) hasa kama kweli hiki chama kimekuja kuziba pengo la uongozi nchini au ni geresha tu kama ya vyama vingine. Kabla hata ya kwenda kuomba usajili wa muda tetesi zilishasambaa juu ya ujio wa chama hicho na ndani ya wiki chache tu CCJ kimepata kutangazwa sehemu mbalimbali kwa bure kabisa huku kikivuta mioyo ya wananchi wa kawaida kabisa waliochosha na vyama vya kisiasa vilivyopo ambao kwa muda mrefu wamesubiria kuona matamanio ya Baba wa Taifa kuhusu chama mbadala cha upinzani yakitimia.

  Tetesi kubwa ni uwepo wa vigogo nyuma ya CCJ na wapo ambao hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe au kufikiri wenyewe kuhusu CCJ hadi waone kwanza nani ameondoka CCM. Kwa wale ambao wanasubiri wasikie “majina makubwa” yakitoka CCM ndio waamini basi kutoka kwa Bw. Fred Mpendazoe hakuwatoshi. Ni wazi vile vile hata likitoka kundi jingine ndani ya CCM bado wapo watu ambao hawataamini na wataendelea kutafutua ufafanuzi kwanini hao siyo “vigogo” au kwanini kuondoka kwao “ni nafuu kwa CCM”.

  Vyovyote vile ilivyo, Watanzania wana haki na sababu ya kuipima CCJ kwa katiba yake, malengo yake, mapendekezo yake ya kushughulikia masuala ya taifa na itikadi yake. Itakuwa ni upungufu wa hekima, na uwezo wa kufikiri kama tutajaribu kukipima CCJ kwa kuangalia nani “anatoka CCM”! Mtu mwenye hekima atachukua muda kusikiliza kile ambacho uongozi wa CCJ, mashabiki wake, Katiba na watunga sera wake wanasema juu yake na siyo kile ambacho waathirika wa uwepo wa CCJ wanasema juu yake.

  Hivyo, mahojiano haya ya kwanza na Mhe. Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa CCM wa kuchaguliwa kwa asilimia 81 (kura 64,000) na ambaye ameamua kuondoka CCM “mapema” yatatupa mwanga wa ni watu gani wako nyuma ya CCJ na kama tunaweza kukubali na kukumbatia uwepo wake katika kuendeleza demokrasia nchini na hasa katika kupatia uongozi “bora” ambao taifa limekuwa likiutamani na kuungojea kwa muda mrefu hasa baada ya kukatishwa tamaa na uongozi ulioingia 2005.

  Sikiliza na uamue mwenyewe.

  http://www.zumodrive.com/share/4GHHMjg2Nm
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  CCM yamuonya Mpendazoe
  (Tanzania Daima)

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemuonya aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, ambaye siku za hivi karibuni alijiunga na Chama Cha Jamii (CCJ), kuacha kutoa kauli za kejeli dhidi ya chama hicho. Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Mpendazoe kukabidhiwa rasmi kadi ya uanachama ya CCJ katika viwanja vya Mwembeyanga juzi mjini Dar es Salaam na kuhutubia mkutano wa hadhara.

  Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema:

  “Siwezi kubishana na Mpendazoe; alikuwa mwenzetu, aliondoka… sasa mimi nibishane naye nini? Sina muda huo kwani kazi iliyo mbele yangu ni utekelezaji wa ilani ya chama tu.”

  Alisema kauli zinazotolewa na Mpendazoe kuwa CCM imekuwa kinara wa rushwa na kushindwa kuwapatia Watanzania maisha bora, hazina ushahidi wowote kwani chama chake kinakubalika kwa wananchi.

  “Huyu anasema CCM inakula rushwa… alete ushahidi wake, chama hiki kinakubalika kwa wananchi, utakumbuka mwaka jana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa tuliibuka na ushindi wa asilimia 91… jamani hapa hatukubaliki kweli?!” alihoji Makamba.

  Alisema tafiti za kitaalam zilizofanywa na Taasisi za Utafiti ya Synovet na RIDET zinaonyesha CCM inakubalika kwa wananchi huku Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, bado anakubalika zaidi kwa Watanzania.

  “Nawaomba wana CCM mpuuzeni huyu, madai haya si ya msingi… sisi tunazungumza kwa tafiti zinazofanywa na wataalam wetu jamani,” alisema Makamba.

  Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati, alimtaka Mpendazoe aendelee kuzungumza tu kwa vile hana jambo jipya huko aliko.

  “Yeye aendelee tu kuzungumza hana jambo jipya… hatuwezi kubishana naye tuna kazi moja tu ya kutekeleza-ilani,” alisema Kapteni Chiligati.

  Alisema CCM ilishamtakia kila heri baada ya kujivua uanachama wa chama hicho na kwenda CCJ mwezi uliopita.

  “Hatutaki kuingia kwenye malumbano na mtu, tunakabiliwa na majukumu mengi…aendelee tu hatuna muda wa kumfuatilia mtu muda huu,” alisema Kapteni Chiligati.

  Juzi akihutubia mkutano wa hadhara, Mpendazoe alisema tatizo la matumizi makubwa ya rushwa na kutumia fedha nyingi katika uchaguzi limo ndani ya CCM, hivyo kuweka sheria kwa ajili ya kupunguza gharama hizo ni jambo ambalo haliwezekani.

  Alisema Rais Jakaya Kikwete, siku za nyuma aliwahi kukiri kuwa matumizi ya fedha katika uchaguzi ni makubwa na kwamba ataweka mkakati wa kutafuta mbinu ya kumaliza tatizo hilo, lakini badala yake CCM wanatafuta sh bilioni 40!

  Mpendazoe ambaye alipewa kadi namba 004408, alidai CCM ni chama kinachoongozwa kisanii na kudanganya watu, lakini umefika wakati wa Watanzania kubadilika na kutafuta chama mbadala.

  Alisema kitendo cha kuendelea kutumia fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi ndiyo sababu serikali imekuwa ikishindwa kusaidia kutatua kero muhimu za wananchi na kutumia muda mwingi kuweka mikakati ya kununua uongozi.
   
 3. b

  buckreef JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu Mpendazoe kafulia, bora angeenda CHADEMA. Hao CCJ wanaonekana kabisa ni wasanii kama vyama vingine vya siasa TZ.
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ngoja tusikie na kumamua mkuu. Na-download now.
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Hajaona chama Makini cha upinzani" huu ni wimbo wa CCM, hamna chama makini zaidi ya ccm na yeye anarudia anafikiri baadaye atakuja kusema kuwa CCJ ni makini. Hii ni sawa na jitu kusema kuwa Tanzania hakuna mwanamke mzuri na kesho unaanza kutongoza. Kama hamna chama cha upinzani makini wewe unaenda kwenye upinzani kufanya nini si ungebaki huko na wapiganaji wenzie wakina malecela huko? Au anataka kutuambia kuwa yeye ndio upinzani makini?
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Maajabu ya hii nchi hayaishi jamani? Leo unasikia CCM wanakuambia ulete ushahidi kama wao wala rushwa. Raisi anasign sheria ya udhibiti wa matumizi wakati wa chaguzi (ingawa baadhi ya vipengele vilichomekwa pasipo ridhaa ya bunge). Hujakaa sawa ccm hiyo hiyo inazindua kampeni kubwa ya kutafuta sh. BILION 40 kwa ajili ya shughuli za uchaguzi. Ukichunguza vizuri kuna kampeni ndogo ndogo za kutafuta fedha katika ngazi nyingine mbali na za kitaifa hivyo ukiangalia utagundua ni fedha nyingi sana zinachangishwa na zitatumika ktk uchaguzi.

  Wakati hayo yakiendelea unapata habari/fununu kwamba ile sheria inarudishwa bungeni tena.

  then unachanganyikiwa..
   
 7. s

  skasuku Senior Member

  #7
  Apr 12, 2010
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  MMKJ, good work!!!... nasubiri the next instalment....
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Nimemsikiliza huyu bwana... he has some BIG points.... kweli huu ni mwaka wa uamuzi!
   
Loading...