Rais Magufuli amteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Rais John Magufuli leo amemteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan
=====
=====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.

Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.

Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo Ia Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dares salaam
18 Aprili 2016


f552c5c24d97bf6944f756b9890cddc5.jpg
 
Kweli vijana tutaendelea kuisoma namba kama wazee ambao walitakiwa kubaki kutoa ushauri kutokana na umri wao wa utumishi kuzidi 60yrs wanafanyishwa kazi bado sijui vijana hizo nafasi huko serikaln watazipata lini
 
Saudi Arabia imemuomba Rais Magufuli ampeleke Dr Dau ubalozini Saudi Arabia, kwani wanahitaji ushauri wake katika mradi Wao wa lile Daraja La kuunganisha Asia na Africa.
 
Magufuli alipochaguliwa niliona anaweza kuja na mbinu tofauti ya uongozi ila siku zinavyozidi kwenda mbele naanza kuona mkomo wa kifikra au utendaji wake ukififia kwa mkuu wangu wa nchi! Matatizo mengi tuliyonayo yamesababishwa na wengi wa hawa viongozi na kuna usemi usemao "Problems cannot be solved at the same level of consciousness that created them."
 
Hivi cheo cha ubalozi c cha kiserikali na c cha siasa? Hivi chuo cha kidiplomasia kina fanya nn ..kama wahitimu wenye ujuzi hawawezi kupata nafasi hizi za ubalozi? Basi kifungwe tuu!!
 
Back
Top Bottom