Ex wangu nenda, nakutakia maisha mema

Kichochoro

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,135
1,163
Wakuu wanaJF, ni miaka kadhaa imepita nilikuwa kwenye mahusiano na dada mmoja. Nilionana naye kwenye maeneo hatarishi sana nikamtongoza dada wa watu akaweka tick nikawa nakula mzigo kama kawaida nilinogewa sana. Mpaka nikaamua kumuweka ndani mara tu baada ya kumuweka ndani alibadilika kabisa akawa anasema niende kwao kujitambulisha.

Na mimi kwa kuwa nilikuwa namkubali nilienda hadi nikatoa mahari baada ya hapo tuliendelea kuishi vizuri wakati huo nikiwa nafanya kazi zangu kama kawaida. Kuna siku aliniaga anaenda kumuona mama yake mgonjwa na mimi nilimruhusu kwenda.

Kesho yake aliamka asubuhi na mapema nikamsindikiza hadi sehemu niliyoishia nikamkubatia nakumtakia safari njema.
Sitaki kuamini sitaki kuamini! Kumbe mke wangu siku hiyo hakwenda nyumbani kama alivyoniaga alienda kwa bwana wake mwingne yaani X wake.

Ilipofika usiku nilimpigia simu mke wangu nikashangaa sauti ya kiume inapokea simu, niliposikiliza kwa makini wanazozana nilikata simu na kumpigia simu mama mkwe ili nijue mgeni kafika mama mkwe alisema hajafika.

Kesho yake niliamua kwenda hadi kwao nilipofika nikakaa hapo kwao ilipofika jioni mke wangu alikuja nyumbani kwao na kunikuta mimi nimeshafika, nilipomuuliza ulilala wapi akadai alilala njiani gari iliharibika.

Okay ilinibidi niamini lakini wakati tukiwa pale niliomba simu yake nilichokikuta ni aibu nilikuta video za yeye mke wangu na na jamaa wakiwa kitandani na picha wakiwa uchi! Niliumia sana na niliondoka kwao bila kuaga. Leo ni miezi 6 sijawahi kumtafuta.

Juzi nilipigiwa na namba ngeni nilipopokea nikasikia sauti yake nilikata simu. Kilichofuata ni sms akisema naomba unisamehe sana mume wangu nilikosea nisamehe sana najutia kosa langu. Sikujibu chochote.

Je, hapa kuna mke kweli au chuma ulete?

Ushauri ukitaka kuoa usioe kwa kumuangalia mtu kwa muda mchache kilichonikuta mimi hakika sitokisahau.
 
Buraza achana naye wewe story yake kidogo inaelekea na yangu 87%. Na halhamsi nimepigiwa simu kama wewe nilipogundua ni yeye nilizungumza naye vizuri tu baada ya hapo nikabadiri namba
 
Buraza achana naye wewe story yake kidogo inaelekea na yangu 87%. Na halhamsi nimepigiwa simu kama wewe nilipogundua ni yeye nilizungumza naye vizuri tu baada ya hapo nikabadiri namba
Inauma sana afu mzigo unakuta unaukubali kishez dah nenda x wang nenda siwez kurudiana naye kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom