Ex wangu anataka kuja kwangu

Ex wangu anataka kuja kwangu

jogijo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
260
Reaction score
500
Habari ya mda wadau,
Huyu dada aliniacha mwaka 2014 tena kwa nyodo mno, alikuwa Dar na mimi nikiwa Dodoma. Niliumia sana maana nilikuwa nampenda, na mwezi huu kapata kazi wilaya moja na mimi nilipo na kwa sababu anajua niko hapo kanipigia simu tukapiga story akaniambia maneno haya ninanukuu

"Rafiki angu kumbe Mungu alijua wewe ulikuwa mume wangu lkn mimi nilikuzingua, nitakuwa nakuja kwako kupoza nyege then tunaendelea na maisha"

Anaomba wikendi hii aje kunisalimia.

Ugumu ni kuwa mimi nimeoa na nina familia sasa japo siishi na mke wangu.

Ushauri wenu wadau nisije kuvunja ndoa yangu maana nikimruhusu aje then tukajikuta tunapiga mechi itakuaje kwa familia yangu?

Then mke wangu akijua kuwa kuna mgeni tena wa kike alikuwa kunisalimia nyumbani kwetu itakuaje?
 
Kila jambo unajibu lake tu sema hutaki kumwambia ukweli unataka kutenda dhambi sema hivi mimi hapana nimeoa kapoteze hamu zako kwa mtu mwingine because i love my family so much .
Basi mmblock asikupate naumkanye asilete mazoea
mpaka na sasa utakuwa na wanjee baki naye huyo uache tamaa .
 
Usiruhusu aje akanyage kwako. Majirani ni wambea.Watamnyetisha mkeo afu iwe noma. Ni bora mkutane huko 'machakani'.
 
Naona utoto umekua mwingi mno, kuna vitu huwa vinashangaza. Mwanaume kuomba ushauri kama atoke nje ya ndoa ama la! Why should it be this way... Haya mambo tuliomba ushauri enzi tuko O'level, ila sio sasa uko na mke na watoto.

Kizazi hiki kimekuwa tegemezi sana kwa social media, unajua kuna watu anaamini kuwa katika hii mitandao ndio atapata maelekezo yote ya kundesha maisha yake. Ni hatari sana, watu hawafikirii kabisa, kila kitu anapeleka mtandaoni, anasifiwa kidogo, analia lia basi anaona maisha yake yanaenda.
 
Nani akushauri sasa? Kasome kitabu chako cha dini unayoiamini kina maelelezo ya nini cha kufanya
 
Back
Top Bottom